Nyegere

(Elekezwa kutoka Mhilu)
Nyegere

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha watoto wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Caniformia (Wanyama kama mbwa)
Familia: Mustelidae (Wanyama walio na mnasaba na chororo)
Jenasi: Mellivora
Storr, 1780
Spishi: M. capensis
(Schreber, 1776)
Ngazi za chini

Nususpishi 12:

Nyegere, melesi au mhilu (jina la kisayansi: Mellivora capensis) ni mnyama mdogo wa familia Mustelidae anayetokea Afrika, Mashariki ya Kati na Uhindi.

Nyegere huishi peke yake kwenye shimo analolichimba yeye mwenyewe. Ni wachimbaji wazuri sana. Vile vidole vyao vyenye kucha ndefu na ngumu humsaidia sana kwenye kazi hii. Hata kama ardhi ni ngumu sana, ana uwezo wa kuchimba shimo linalomtosha kujificha katika kipindi kinachokadiriwa kuwa ni dakika kumi tu. Ni mvivu katika masuala ya nyumba yake hivyo basi anapojisikia uvivu hujilaza sehemu yoyote inayomfaa. Alikwishaonekana akiwa kajiliza katika pango la mbwamwitu kama kwake.

Ni mnyama mdogo anayekula kila kitu: nyoka wenye sumu, kenge, majani, matunda, maiti ya binadamu, mizoga ya chui, simba, duma, ndege n.k. Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe.

Katika Guiness World Book of Records yeye ndiye kiumbe asiye na hofu kuliko wote duniani. Alishawahi kukutwa akipigana na chui, simba na hata tembo na vifaru katika nyakati tofauti[1].

Ngozi yake ni ngumu sana kiasi kwamba mishale na mikuki au risasi ni ngumu kupenya. Ukitaka kumwua ni kumpiga kwa kitu kizito au risasi katika fuvu la kichwa. Mwili wake haudhuriki na sumu ya nyoka wa kawaida na ikitokea ameumwa na nyoka mwenye sumu kali na hiyo sumu ikapenya kwenye damu yake itamfanya alale kwa saa chache tu, kisha ataendelea na mambo yake.

Nususpishi za Afrika

hariri

Nususpishi za Asia

hariri

Hadithi za kitamaduni za Tanzania

hariri

Inasemekana nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake. Hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike. Hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike, litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari, maana wivu wa dume ni kuwa jani litakuwa "limefaidi utamu" wa jike.

Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, warina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za nyegere. Anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke. Mrina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo wa kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu kadhaa wameuawa kwa namna hiyo. Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyerina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimyakimya.

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyegere kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Marejeo

hariri