Nyanda za Juu za Adamawa

(Elekezwa kutoka Milima ya Adamawa)

Nyanda za juu za Adamawa (kwa Kiingereza: Adamawa Plateau; Kifaransa: 'Massif de l'Adamaoua') ni eneo la Afrika ya Kati linalopatikana kuanzia kusini-mashariki mwa Nigeria kupitia kaskazini mwa Kamerun (mikoa ya Adamawa na Kaskazini) hadi Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mazingira ya karibu na Ngaoundal katika Mkoa wa Adamwa wa Kamerun.

Jina la nyanda za juu hizo lilitolewa kwa kumbukumbu ya kiongozi Mwislamu wa Wafulani, Modibo Adama. Sehemu yake nchini Nigeria inajulikana pia kama Milima ya Gotel.

Nyanda za Juu za Adamawa ndizo chanzo cha mito mingi, pamoja na Mto Benue. Ni muhimu kwa madini yake ya boksiti. [1] Mwinuko wa wastani ni kama mita 1,000, [2] lakini mwinuko unaweza kufikia urefu wa mita 2,650. Uoto ni hasa savana, watu wanaoishi hapa ni wachache. Ufugaji wa ng'ombe ni kazi kuu katika eneo hilo.

Marejeo

hariri
  1. "Encyclopædia Britannica - Adamawa Plateau". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Oktoba 2007. Iliwekwa mnamo Septemba 15, 2007.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "MSN Encarta - Adamawa Plateau". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-31. Iliwekwa mnamo Septemba 15, 2007. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |https://www.webcitation.org/5kwDQCNco?url= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za Juu za Adamawa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.