Mkataba wa Schengen

Mkataba wa Schengen (kwa Kiingereza: Schengen Agreement; kwa Kifaransa: Accord de Schengen) ni makubaliano ya kimataifa huko Ulaya ambayo yanalenga kukomesha udhibiti wa mpaka uliopo kati ya nchi na nchi na pia ushirikiano katika mipaka ya nje kwenye ardhi kavu na majini[1]. Haiathiri udhibiti wa forodha: hizo zinasimamiwa na Umoja wa Forodha wa Ulaya.

     Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU)      Wanachama wa EU katika maandalizi ya kujiunga na makubaliano      Wanachama wa EU katika maandalizi ya kujiunga na makubaliano      Wanachama wa Mkataba wa Schengen, si wanachama wa EU      Si wanachama wa EU, lakini wanachama wa Mkataba wa Schengen      Si wanachama wa Mkataba wa Schengen, lakini bado hakuna udhibiti wa kawaida wa mpaka

Jina linatokana na mji wa Schengen nchini Luxemburg ambako mapatano yale yalitiwa sahihi.

Raia wa nchi za wanachama wanaweza kusafiri bila vizuizi ndani ya eneo la Schengen bila kuomba visa au idhini ya makazi[2]. Raia wa nchi zilizo nje ya eneo la Schengen kwa kawaida hupokea "Viza ya Schengen", ambayo pia inawapa haki ya kukaa katika nchi zote wanachama.

Wakati wa kuvuka mipaka ndani ya eneo la Schengen, inahitajika pia kuwa na kitambulisho. Kwa raia wa eneo la Schengen ni kitambulisho halali au Pasipoti, kwa raia kutoka nchi zilizo nje ya eneo la Schengen pasipoti halali na, ikiwa ni lazima, viza.

Eneo la Schengen

hariri

Nchi wanachama zote za Umoja wa Ulaya zinashiriki katika mkataba wa Schengen isipokuwa tano ambazo ni Bulgaria, Kipro, Romania na Eire. Kuna pia nchi ambazo si wanachama wa Umoja wa Ulaya zilizojiunga kama vile Iceland, Liechtenstein, Norwei na Uswisi, pamoja na nchi ndogo ambazo ziko ndani ya nchi wanachama yaani Monako, San Marino na Mji wa Vatikani zinazotendewa kama wanachama.

Kwa jumla kuna nchi wanachama 27 za mkataba wa Schengen.

Baada ya Uingereza kuondoka katika Umoja wa Ulaya tarehe 31 Desemba 2020, Gibraltar (eneo la ng'ambo la Uingereza ndani ya Rasi ya Iberia) iliungwa na mkataba wa Schengen mnamo 2021 ili kuepukana na vizuizi kwa wakazi wake wanaovuka mpaka na Hispania kila siku. [3]

Udhibiti wa muda mpakani

hariri
 
Mahali pa kusaini "Schengen" huko Luxemburg.

Hata kama udhibiti wa mpaka wa kawaida ulifutwa, udhibiti wa mpakani unaweza kurudiwa kwa muda kama nchi ni mwanachama na kuna sababu maalumu ya kufanya hivyo.

Mifano ni:

  • Wakati wa Mashindano ya Soka ya Ulaya mnamo 2008, Austria na Uswizi zilirudisha udhibiti wa mipaka mara kwa mara.
  • Wakati wa mkutano wa G20 huko Ujerumani, udhibiti wa kawaida kwenye mipaka ya Ujerumani ulirejeshwa tena.
  • Wakati wa janga la Covid19, udhibiti wa mipaka karibu katika nchi zote za Ulaya ulirejeshwa mnamo mwaka 2020.
 
Hata pasipo kituo cha ukaguzi wa hati za usafiri, mipaka bado huonyeshwa kwa vibao kama hivi (mpaka wa Ujerumani).

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri