Mkoa wa Sikasso
Mkoa wa Sikasso (kwa Kibambara: Sikaso Dineja) ni mkoa uliomo kusini mwa Mali. Unapakana na nchi za Guinea, Cote d'Ivoire na Burkina Faso.
Mkoa huo una eneo la kilomita za mraba 70,280. Wakati wa sensa ya mwaka 2009 ulikuwa na wakazi 2,625,919.
Mji mkuu wa mkoa huo ni Sikasso ambayo ni mji wa pili kwa ukubwa nchini humo. Sikasso inazidi kukua kwa kasi kutokana na watu wanaokimbia ghasia huko Cote d'Ivoire upande wa kusini.
Makabila makubwa ni pamoja na Wasenufo wanaojulikana kwa vinyago vyao, Wasamago wanaojulikana kwa kuwa wakulima bora wa Mali, na kabila kuu nchini Mali ambao ni Wabambara.
Uchumi wa eneo hilo unategemea kilimo na Sikasso inajulikana kwa matunda na mboga. Mkoa wa Sikasso hupokea mvua nyingi kuliko eneo lingine lolote la Mali.
Mgawanyiko wa kiutawala
haririMkoa wa Sikasso umegawanywa kwa wilaya (cercles) saba : [1] [2]
Jina la Cercle | Eneo (km2) | Idadi ya watu
Sensa ya 1998 |
Idadi ya watu
Sensa ya 2009 | |
---|---|---|---|---|
Bougouni | 20,028 | 307,633 | 459,509 | |
Kadiolo | 5,375 | 130,730 | 239,713 | |
Kolondiéba | 9,200 | 141,861 | 202,618 | |
Koutiala | 8,740 | 382,350 | 575,253 | |
Sikasso | 15,375 | 514,764 | 725,494 | |
Yanfolila | 9,240 | 163,798 | 211,824 | |
Yorosso | 5,500 | 141,021 | 211,508 |
Sehemu ya kusini-magharibi ya mkoa wa Sikasso inajulikana kama Wassoulou . Eneo hili ni maarufu kwa muziki wake wa kipekee na utamaduni wa uwindaji. Mji mkuu wa Wassoulou ni Yanfolila .
Koutiala katika sehemu ya kaskazini ya Mkoa wa Sikasso ni kitovu cha tasnia ya pamba nchini Mali.
Marejeo
hariri- ↑ Loi N°99-035/ du 10 Aout 1999 Portant Création des Collectivités Territoriales de Cercles et de Régions (PDF) (kwa Kifaransa), Ministère de l'Administration Territoriales et des Collectivités Locales, République du Mali, 1999, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-03-09, iliwekwa mnamo 2022-01-11
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help). - ↑ Communes de la Région de Sikasso (PDF) (kwa Kifaransa), Ministère de l’administration territoriale et des collectivités locales, République du Mali, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 3 Desemba 2013
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link).
Viungo vya nje
hariri- Site Officiel de la Région de Sikasso (kwa Kifaransa), Ministère de l'Administration Territoriale et des Collectivités Locales, République du Mali, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-25, iliwekwa mnamo 2022-01-12
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help). - Synthèsis des Plans Communaux de Securité Alimentaire de la Région de Sikasso 2007-2011 (PDF) (kwa Kifaransa), Commissariat à la Sécurité Alimentaire, République du Mali, USAID-Mali, 2007, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-07-22, iliwekwa mnamo 2022-01-11
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help).