Mlima Chebon
Mlima Chemnirot, ukiwa na kimo cha mita 3,375 juu ya usawa wa bahari, ni kilele cha nne[1] katika safu ya milima ya Cherang'any, iliyopo katika nyanda za juu magharibi mwa Kenya.
Vilima vya Cherangany huvuka kaunti tatu: kaunti ya Trans-Nzoia, kaunti ya Elgeyo-Marakwet na kaunti ya West Pokot na ni makazi ya jamii ya wawindaji-wakusanyaji iitwayo Wasengwer.
Vilima hivyo vina mmojawapo kati ya misitu mikubwa mitano ya Kenya na ni chanzo muhimu cha maji.
Tambarare yake kubwa ya kati imetenganishwa na mwambao wa Mau unaoinuka kuanzia kwenye mpaka na Tanzania mpaka Vilima vya Cherang'any. Mwambao huo unaonesha mwisho wa tambarare inayoinuka kwenye mteremko wa Mlima Elgon. [2]
Jiolojia
haririVilima vya Cherang'any viliundwa kutokana na mpasuko. Safu hizi huunda ubavu wa magharibi wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki lianzialo Jibuti kwa upande wa kaskazini hadi Msumbiji kwa upande wa kusini. Vilima vya Cherang'any vinapatikana kwenye mwambao wenye misitu na vimezingirwa na kuta za majabali kwenye pande tatu. Vilima hivyo vimeundwa kwa miamba na madini mbalimbali yakiwemo Chromite yaliyopatikana hapo na wanajiolojia kipindi cha ukoloni.[3][4]
Ekolojia
haririVilima vya Cherang'any vinasimamiwa na programu ya mazingira ya Umoja wa Mataifa kama mojawapo ya vyanzo muhimu vitano va maji nchini Kenya.[5] Kwa mujibu wa ripoti ya mwisho, iliyoonesha mabadiliko ya misitu katika vilima hivyo kati ya mwaka 2002 na 2003, ilionesha kuwa eneo hilo ni la mwisho kwa kuathirika kwa ukataji miti kati ya maeneo yote yaliyokuwa chini usimamizi. Huku ekari 174.3 zikiwa zimeharibiwa na ukataji miti, hasa katika kaunti za Elgeyo-Marakwet na Pokot Magharibi. Kwa sababu misitu hii ni ya uoto wa asili, ripoti hiyo inapendekeza paangaliwe kwa ukaribu ili kuepusha uharibifu zaidi.[6] Hifadhi hizo kumi na tatu za misitu huitwa Misitu ya vilima vya Cherang'any.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Paul Clarke (1989). The Mountains of Kenya: A Walker's Guide. Mountain Club of Kenya, 1989. uk. 191. Iliwekwa mnamo 2020-03-02.
- ↑ "Kenyalogy: Geography - Rift Valley and Highlands". www.kenyalogy.com. Iliwekwa mnamo 2008-03-18.
- ↑ "Mountains>Western Highlands". www.magicalkenya.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-03. Iliwekwa mnamo 2008-03-18.
- ↑ Joseph Bindloss, Tom Parkinson & Matt Fletcher (2003). Kenya - Google Book Search. uk. 328. ISBN 9781864503036. Iliwekwa mnamo 2008-03-18.
- ↑ "- Changes in Forest Cover in Kenya's". www.africanconservation.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 1, 2007. Iliwekwa mnamo 2008-03-18.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Changes in forest cover in Kenya's five "water towers" 2000–2003". United Nations Environment Programme (UNEP). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Juni 2006.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mlima Chebon kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |