Modoaldi (Akwitania, leo nchini Ufaransa, 584/590 - Trier, leo nchini Ujerumani, 12 Mei 645/648) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 620 hivi[1].

Kabla ya kuchaguliwa alifanya kazi ikulu bila kupendezwa na maadili mabovu ya huko[2].

Baadaye alijenga na kupamba makanisa na kuanzisha monasteri mbalimbali na jumuia za mabikira kwa kusaidiana na dada yake Severa, ambaye hatimaye alizikwa karibu naye [3] [4].

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 12 Mei[5].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92772
  2. Monks of Ramsgate. "Modoald". Book of Saints, 1921. CatholicSaints.Info. 10 January 2016
  3. ""St. Severa of Villeneuve, France", Antiochian Orthodox Christian Archdiocese". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-02-05. Iliwekwa mnamo 2021-05-10.
  4. Schulenburg, Jane Tibbetts. Forgetful of Their Sex: Female Sanctity and Society, ca. 500–1100, University of Chicago Press, 1998
  5. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.