Moto wa Pasaka
Moto wa Pasaka au Moto mpya unawashwa hasa wakati wa kesha la Pasaka ukimaanisha mwanzo mpya wa uhai uliosababishwa na ufufuko wa Yesu.
Katika moto huo, unaotakiwa kuondoa giza la ulimwengu, unawashwa mshumaa wa Pasaka ambao unamwakilisha Yesu mfufuka ambaye anaongoza waamini kama vile mnara wa nuru ulivyowaongoza Waisraeli jangwani wakati wa Musa.
Mbali na liturujia, katika nchi mbalimbali kuna desturi za kuwasha moto wa namna hiyo, hata siku moja kabla au baada ya Pasaka.
Huko Uholanzi kati ya vijiji kadhaa kuna mashindano kuhusu nani atawasha moto mzuri zaidi. Ule mrefu zaidi ulifikia mita 45.98.
Tanbihi
haririViungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Paasvuursite (Easter Fire Site) (Dutch)