Kesha au Mkesha (kwa Kiingereza Vigil, kutoka Kilatini vigilia, yaani hali ya kuwa macho)[1] ni kipindi cha kutolala kwa makusudi, hasa kwa lengo la kidini, kama vile kusali kirefu.

Kesha katika mchoro wa karne ya 14.
"Kesha la Askari" kadiri ya John Pettie.

Mara nyingi kesha linafanyika kabla ya adhimisho maalumu, kama vile sikukuu fulani,[2][3] lakini kuna waumini, hasa watawa, wanaokesha kila usiku walau kwa muda fulani.

Nje ya dini, makesha yanafanyika hasa kandokando ya mgonjwa aliye mahututi na ya maiti ya marehemu.

Katika Ukristo

hariri
 
Wakristo Waorthodoksi wakiwasha mishumaa yao katika na mwali mpya kutoka altareni, Adelaide, South Australia, Australia.
 
Askofu akishika trikiron na mashemasi wakiwa na mishumaa ya Pasaka wakati wa kuadhimisha usiku wa ufufuko kwenye monasteri ya Msalaba mtakatifu huko Wayne, West Virginia, Marekani.

Katika Ukristo, kesha muhimu kuliko yote ("mama wa makesha yote") ni lile la usiku wa Pasaka, unapoadhimishwa ufufuko wa Yesu ambao kadiri ya Injili zote ulitokea usiku kati ya Jumamosi na Jumapili.

Katika kesha hilo yanafanyika masomo mbalimbali kutoka Biblia, yakifuatana na Zaburi na nyimbo nyingine pamoja na sala. Baada ya hapo unaadhimishwa ubatizo ambao ni sakramenti ya kufa na kufufuka pamoja na Yesu Kristo, na pengine kipaimara na ekaristi pia.

Duniani kote linaheshimika sana kesha la Noeli pia, kwa sababu kadiri ya Injili ya Luka Yesu alizaliwa usiku.

Makesha yasiyoendana na sikukuu fulani yanafanyika hasa kwa kuimba Zaburi, tenzi na nyimbo nyingine, na kwa kusoma maandiko matakatifu na mengine ya Kiroho pamoja na kutoa sala maalumu.

Tanbihi

hariri
  1. Cross, F. L. Cross; Livingstone, E. A., whr. (2005). The Oxford Dictionary of the Christian Church. Oxford University Press. Available (limitedly) online at the Oxford Reference.
  2. Eve of a Feast, Catholic Encyclopedia
  3. UMC.org

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: