Mti wa uzima (kwa Kiebrania עֵץ הַֽחַיִּים, Etz haChayim,) ni mfano unaotumiwa na Biblia.[1]

Anguko la mtu lilivyochorwa na Lucas Cranach katika karne ya 16, mti wa uzima ukiwepo upande wa kushoto karibu na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Katika kitabu cha Mwanzo, mti wa uzima unapatikana katika mstari 2:9 kama mti uliopandwa na YHWH Elohim (יְהוָה אֱלֹהִים) karibu na mti wa ujuzi wa mema na mabaya (עֵץ הַדַּעַת) "katikati ya bustani ya Eden".[2]

Katika 3:24 imeandikwa kwamba baada ya dhambi ya asili kerubi analinda njia inayofikia mti wa uzima.

Kitabu cha Mithali kinatumia jina hilo mara nne (3:18, 11:30, 13:12 na 15:4).

Hatimaye Kitabu cha Ufunuo kinatumia usemi wa Kigiriki ξύλον (τῆς) ζωής, xylon (tēs) zōës, mara nne vilevile (2:7, 22:2, 22:14 na 22:19.

Milango ya kifalme iliyochongwa kudokeza mti wa uzima, Chotyniec, Poland.

Kwa kawaida Wakristo wamechukua usemi huu kama wa fumbo kwa msalaba wa Yesu.

Tanbihi hariri

  1. Encyclopaedia Britannica. Encyclopaedia Britannica Online (2013). "world tree". Encyclopædia Britannica Inc. 
  2. Mettinger 2007, pp. 5–11

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mti wa uzima kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.