Mto Tocantins ni mto ambao unapita katika mashariki mwa nchi ya Brazil. Chanzo chake kinapatikana kwenye milima ya jimbo la Goiás upande wa magharibi wa mji mkuu Brazilia.

Beseni la Tocantins
Mdomo Rio Para, Atlantiki
Nchi Brazil
Urefu km 2,450
Mkondo wastani m3/s 11,796
Eneo la beseni km2 749,200

Mto unaishia kwenye Rio Para ambayo ni hori ya Atlantiki ambako maji ya Tocantins yanakutana na maji ya mkono wa kando wa Amazonas.

Jina la mto limetokana na lugha ya Maindio wenyeji na neno lao kwa ndege wa tukani. Jina la mto limekuwa pia jina la jimbo la Tocantins nchini Brazil linalopitiwa na mto huo.

Nguvu ya mto hukamatwa kwa njia ya malambo na vituo vya umememaji.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Brazil bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Tocantins kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.