Mfululizo wa sheria kuhusu ajira ya watoto, kinachojulikana kama Sheria za Kiwanda, zilipitishwa nchini Uingereza katika karne ya 19. Watoto walio na umri wa chini ya miaka 9 hawakuruhusiwa kufanya kazi, wale wenye umri wa miaka 9-16 wangeweza kufanya kazi saa 12 kwa siku kulingana na Sheria ya Kiwanda cha Pamba . Mnamo mwaka 1856, sheria iliruhusu ajira ya watoto zaidi ya umri wa miaka 9, kwa masaa 60 kwa wiki, usiku au mchana. Mnamo mwaka 1901, umri ulioruhusiwa wa kuajiriwa kwa watoto uliongezwa hadi 12.[1][2]
Mtoto wa Kichina akitengeneza viatu, mwishoni mwa karne ya 19
Ajira ya watoto nchini Nigeria

Ajira Kwa watoto hariri

Ajira kwa watoto inarejelea unyonyaji wa watoto kupitia aina yoyote ya kazi ambayo inawanyima watoto utoto wao, inaingilia uwezo wao wa kuhudhuria shule ya kawaida, na inawadhuru kiakili, kimwili, kijamii na kimaadili.[3] Unyonyaji kama huo umepigwa marufuku na sheria duniani kote,[4]ingawa sheria hizi hazizingatii kazi zote za watoto kama ajira kwa watoto; isipokuwa ni pamoja na kazi za wasanii watoto, majukumu ya familia, mafunzo yanayosimamiwa, na baadhi ya aina za kazi za watoto zinazofanywa na Amish children, pamoja na watoto wa kiasili katika Amerika.[5] [6]

Ajira kwa watoto imekuwepo kwa viwango tofauti katika historia. Wakati wa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20, watoto wengi wenye umri wa miaka 5-14 kutoka familia maskini walifanya kazi katika mataifa ya Magharibi na makoloni yao. Watoto hawa walifanya hasa kazi za kilimo, shughuli za mikutano ya nyumbani, viwandani, uchimbaji madini na huduma kama vile news boys- wengine walifanya kazi za usiku za masaa 12. Kwa kuongezeka kwa mapato ya kaya, upatikanaji wa shule na kupitishwa kwa sheria za ajira kwa watoto, viwango vya matukio ya ajira ya watoto vilipungua. [7] [8] [9]

Katika nchi maskini zaidi duniani, karibu mtoto mmoja kati ya wanne wanajishughulisha na ajira kwa watoto, idadi kubwa zaidi kati yao (asilimia 29) wanaishi nchi za Afrika pembezoni mwa Jangwa la Sahara . [10] Mnamo mwaka 2017, mataifa manne za Afrika (Mali, Benin, Chad na Guinea-Bissau) walishuhudia zaidi ya asilimia 50 ya watoto wenye umri wa miaka 5-14 wakifanya kazi. [10] Kilimo duniani kote ndio mwajiri mkubwa zaidi wa ajira kwa watoto. Idadi kubwa ya ajira kwa watoto hupatikana vijijini na katika uchumi usio rasmi wa mijini; watoto huajiriwa zaidi na wazazi wao, badala ya viwanda. [11] Umaskini na ukosefu wa shule vinachukuliwa kuwa sababu kuu ya ajira kwa watoto. [12]

Matukio ya ajira kwa watoto yalipungua ulimwenguni kutoka 25% hadi 10% kati ya mwaka 1960 na 2003, kulingana na Benki ya Dunia . [13] Hata hivyo, jumla ya idadi ya watoto wanaotumikishwa bado ni kubwa, huku shirika la Mfuko wa Kimataifa wa Watoto (UNICEF) na Shirika la kimataifa la kazi (ILO) zikikubali wastani wa watoto milioni 168 wenye umri wa miaka 5-17 duniani kote walihusika katika ajira kwa watoto mwaka 2013. [14]

Historia hariri

Ajira kwa watoto katika jamii za kabla ya viwanda

Ajira kwa watoto ni sehemu ya ndani ya uchumi kabla ya viwanda. [15] Katika jamii za kabla ya viwanda, ni nadra sana kuwa na dhana ya utoto katika maana ya kisasa. Watoto mara nyingi huanza kushiriki kikamilifu katika shughuli kama vile kulea watoto, uwindaji na kilimo punde tu wanapokuwa na uwezo. Katika jamii nyingi, watoto walio na umri wa miaka 13 wanaonekana kuwa watu wazima na wanashiriki katika shughuli sawa na watu wazima. [15]

Kazi ya watoto ilikuwa muhimu katika jamii za kabla ya viwanda, kwani watoto walihitaji kufanya kazi iliwaweze kuishi na ya kikundi chao. Jamii za kabla ya viwanda zilikuwa na tija ndogo na maisha mafupi; kuwazuia watoto wasishiriki katika kazi yenye tija kungekuwa na madhara zaidi kwa ustawi wao na wa kikundi chao kwa muda mrefu. Katika jamii za kabla ya viwanda, kulikuwa na haja ndogo ya watoto kuhudhuria shule. Hii ni kesi hasa katika jamii zisizojua kusoma na kuandika. Ujuzi na maarifa mengi ya kabla ya viwanda yaliweza kupitishwa kupitia ushauri wa moja kwa moja au mafunzo na watu wazima wenye uwezo. [16]

Marejeo hariri

  1. Laura Del Col (West Virginia University). "The Life of the Industrial Worker in Nineteenth-Century England". victorianweb.org. 
  2. "The Factory and Workshop Act, 1901". Br Med J 2 (2139): 1871–2. 1901. PMC 2507680. PMID 20759953. doi:10.1136/bmj.2.2139.1871. 
  3. "What is child labour?". International Labour Organization. 2012. 
  4. "International and national legislation - Child Labour". International Labour Organization. 2011. 
  5. Larsen, P.B. Indigenous and tribal children: assessing child labour and education challenges. International Programme on the Elimination of Child Labour (IPEC), International Labour Office. 
  6. "Council Directive 94/33/EC of 22 June 1994 on child labour". EUR-Lex. 2008. 
  7. Cunningham and Viazzo (1996). Child Labour in Historical Perspective: 1800-1985. UNICEF. ISBN 978-88-85401-27-3. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 November 2015.  Check date values in: |archivedate= (help)
  8. Prügl, Elisabeth (1999). The Global Construction of Gender - Home based work in Political Economy of 20th Century. Columbia University Press. ku. 25–31, 50–59. ISBN 978-0231115612. 
  9. Hindman, Hugh (2009). The World of Child Labour. M.E. Sharpe. ISBN 978-0-7656-1707-1. 
  10. 10.0 10.1 "UNICEF Data – Child Labour". UNICEF. 2017. Iliwekwa mnamo 18 April 2018.  Check date values in: |accessdate= (help)
  11. Eric V. Edmonds; Nina Pavcnik (Winter 2005). "Child Labour in the Global Economy". Journal of Economic Perspectives 19: 199–220. doi:10.1257/0895330053147895.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help); Check date values in: |date= (help)
  12. "Child labour - causes". ILO, United Nations. 2008. 
  13. Norberg, Johan (2007), Världens välfärd (Stockholm: Government Offices of Sweden), p. 58
  14. "To eliminate child labour, "attack it at its roots" UNICEF says". UNICEF. 2013. 
  15. 15.0 15.1 Diamond, J., The World Before Yesterday
  16. Diamond, J., The World Before Yesterday