Mtumiaji:Muddyb/Archive 1
Ndugu Muddy, karibu kwenye wikipedia ya Kiswahili! Kuna kazi nyingi. Naomba uangalie makala ya "Msaada wa kuanzisha makala" (utaipata pia kwa kubonyeza "msaada" hapo upande wa kushoto). Ukiwa na swali lolote uliza tu. Wakati huu ni hasa Oliver, Ndesanjo pamoja nami walio tayari kusaidia. --Kipala 17:17, 24 Agosti 2007 (UTC)
Asante kwa jibu lako. Naona umeandika machache kuhusu habari za musiki ya TZ. Je unawajua wanamuziki walioonekana tangu juzi hapa sw-wiki? Mara nyingi makala zao zina kasoro ya kukosa habari za kimsingi. Yaani kwenye ukurasa wa binafsi (user-page) si kitu, kila mtu anaamua mwenyewe. Lakini kama ni makala kuhusu mtu lazima kuwa na jina raia na habari kama tarehe/mwaka ya kuzaliwa, anakotoka, elimu na tarehe kadhaa kuhusu maisha au kazi. Nahisi ya kwamba wale wanamuziki walipeana habari "twende wikipedia" sasa naona ni vizuri ila tu wapi tumpate mtu wa kuwasiliana nao na kuwaomba wasahihishe au kuongeza makala zao? Je unaweza kusaidia? --Kipala 06:21, 28 Agosti 2007 (UTC)
Muundo wa makala
Ndugu Muddy, asante kwa jitihada zako za kuendelea. Naomba kukupatia mapendekezo kadhaa yanayosaidia kuboresha kazi. Mfano makala ya Lipumba. Ni vizuri ya kwamba uliorodhesha elimu yake pamoja na tarehe ya kuzaliwa. Tarehe hizi zinapaswa kuwepo kila makala au kama hazijulikani kutaja angalau takriban mwaka (katika historia: karne) wa kuzaliwa.
Lakini ni vema kukumbuka ya kwamba watu wasiokaa Tanzania hawamjui kabisa. Hii ni sababu kutaja katika sentensi ya kwanza kwa kifupi: huyu mtu ana umuhimu gani? Kwa mfano:
Ibrahim Lipumba ni mwanasiasa nchini Tanzania na mwenyekiti wa chama cha upinzani wa Civic United Front. Alizaliwa.....
Halafu: Ukitaja mahali pa kuzaliwa ni vema kutaja pia nchi. Wasio WaTZ labda hawajui Tabora. Bado kimoja: Unapenda kuanzisha makala ya mtu kwa kutaja JINA halafu NUKTA na sentensi mpya. Hii si fomati yetu hadi sasa ni kawaida kuingiza jina la makala mwanzoni wa sentensi ya kwanza na kuitilia alama za ''' mbele na nyuma.
Kuhusu viungu ni kitu kingine, labda tujadili siku nyingine ukipenda. Naomba uendelee na michango yako! --Kipala 19:49, 6 Septemba 2007 (UTC)
Hongera kwa makala ya ndege
Ndugu Muddy, asante kwa hongera zako, lakini mimi sikutohoa ile Template kwa wikipedia ya Kiswahili. Bwana Marcos ameitohoa na mimi nimeibadilisha kidogo tu. Salamu nyingi. ChriKo 10:18, 7 Septemba 2007 (UTC)
Makala ya Mh Temba
Ndugu Muddy, sijaelewa vizuri kwa nini makala ya Temba inaitwa Mh Temba? Yaani jina lake ni Amani James Pausen Temba sivyo? Kwa nini isiwe Amani Temba? Halafu: nimeongeza interwiki huko katika makala ya John Woo. Maana yake ni vizuri kuonyesha makala kuhusu mtu yuleyule au jambo lile katika lugha nyingine kama yapo hasa Kiingereza na Kifaransa kwa wasomaji wetu--Kipala 11:29, 8 Septemba 2007 (UTC)
- Asante kwa jibu na maelezo. Utaona ya kwamba nimefanya mambo mawili:
- kuhamisha makala kwenda "Amani Temba"
- kuunda ukurasa wa kusogeza "Mheshimiwa Temba"
- Ni kawaida tena vizuri katika kamusi elezo kuandika makala za watu chini ya jina la kiraia. Maana yake vyeo au majina ya kisanii huweza kubadilika au kusahauliwa. Hata kama marafiki waote wanamjua mtu kwa jina la utani tu bado mtu wa mbali zaidi anaweza kumtamtafuta kwa jina la kawaida. Kwa sababu hiyo unampata hata Mwalimu katika makala ya "Julius Nyerere".
- Ila tu tunatumia mbinu ya kurasa hizi za kusogeza (#REDIRECT). Maana yake kama uwezo ni mkubwa ama mtu anajulikana kwa majina mbalimbali au watu wamezoea kumtaja kwa majina mbalimbali tunaunda kurasa hizo kwa kila umbo la jina. Temba apatikana sasa kwa njia tatu ama "Mh Temba" au "Mheshimiwa Temba" na zote mbili zaelekeza kwenda "Amani Temba". Hivyo kwa mfano Nyerere anapatikana kwa "Mwalimu Nyerere", "Julius Kambarage Nyerere" pia "Mwalimu Julius Kambarage Nyerere" na zote zaelekeza kwenda "Julius Nyerere".
- Halafu naomba sana tuendelee bila samahani kujenga wiki yetu tukisaidiana. --Kipala 18:29, 10 Septemba 2007 (UTC)
- Asante kwa jibu na maelezo. Utaona ya kwamba nimefanya mambo mawili:
Sanduku ya waimbaji
Basi jaribu yale yanayofuata ukifungua hapohapo juu ukurasa wa "kuhariri". Badala ya sanduku lenye XXX utaona maandishi. Uyanakili na kuiweka mwanzo wa makala kabla ya kila andishi. Baada ya alama ya = andika yale unayotaka badala ya XXX. Pale usipoandika na kufuta XXX haionyeshi mstari wote. Kwa picha fuata maelezo. Angalia mfano wa Shenazi. Rudia kunakili sehemu hii ya chini (katika hali ya "hariri") kwa kila makala. Usisahau mabano aina ya { na } mwanzo na mwishoni.
XXX | |
---|---|
| |
Jina Kamili | {{{jina kamili}}} |
Jina la kisanii | XXX |
Nchi | XXX |
Alizaliwa | XXX |
Alikufa | XXX |
Aina ya muziki | XXX |
Kazi yake | XXX |
Miaka ya kazi | XXX |
Ameshirikiana na | XXX |
Ala | XXX |
Kampuni | XXX |
--Kipala 15:49, 11 Septemba 2007 (UTC)
- Muddy, nimeongeza hii ya rangi natumaini ya kwamba itafanya kazi nimejaribu kwa Professor Jay. Sasa naomba kwa matumizi ya wikipedia hii jaribu muundo: jina la makala kuwa jina raia; makala inaanza kwa jina hili ukiongeza jina la kisanii baadaye (tazama nilivyomweka P.Jay). Halafu endelea unavyoona. ---- Kwenye sanduku uwe huru kuandika juu unavyoona jina la kisanii au jina la kiraia.
- Halafu ombi kwa mawasiliano: utaratibu wa kawaida ni ukiandika habari kwenye ukurasa wa majadiliano unaandika chini si juu (sijui kwa nini lakini hivyo ndivyo). Halafu tia sahihi. Njia rahisi ni kutumia katika dirisha la "hariri" alama ya tatu juu kutoka upande wa kulia ukibofya tu. Unaingiza alama za --~~~~ hata unaweza kuzichapa moja kwa moja zinabadilika kuwa jina lako na tarehe. Inrahisisha mawasiliano kwa sababu inaweka kiungo na ukurasa wako.
- Kuhusu rangi: jaribu majina ya Kiingereza na utaona yapi yatapokelewa - nafikiri hapa ni orodha ya rangi. Nimenakili majina jinsi yanavyoonekana katika nguzo "HTML name" - heri nakili usitaipi
- Ushauri: amua kutumia rangi moja kwa aina ya sanii- menginevyo tunapata mchanganyiko mkali. Ukiamua nitaingiza utaratibu katika templeti na kuukinga. Kwanza uchezee kidogo mpaka umeridhika. --Kipala 16:39, 12 Septemba 2007 (UTC)
- Muddy, kuhusu redirect: nikupe mfano. Ukiwa na habari juu ya "Ray C" (simjui, tuseme jina lake kiraia ni Hamed Mhindi, sawa?) unaweza kuanzisha makala hivyo. Sasa una njia mbalimbali:
- A) unafungua dirisha yoyote, tusema ya Mwanzo ukiona mstari wa anwani juu kabisa dirishani "http://sw.wikipedia.org/wiki/Mwanzo" sasa unafuta neno "mwanzo" badala yake unaandika "Ray C" na kugonga ENTER. Tayari unapata ukurasa mpya unaosema "Ray C (Ukurasa huu haujaandikishwa bado)". Sasa unabonyeza "kuhariri" na kuandika "#redirect [[Hamed Mhindi]]" halafu "weka ukurasa".
- B) Tokeo lake ni ukurasa unaosema juu: Ray C, chini yake "Redirect page" na kwa maandishi nyekundu mshale na "Hamed Mhindi".
- C)Ukibonyeza maandishi unafungua ukurasa mpya wa "Hamed Mhindi" unapoandika mambo yako na kuhifadhi.
- D) Badala ya hatua A) unaweza kuanzisha ukurasa pia kwa kufungua ukurasa wa "Amani Temba", kugonga "hariri", na kuweka jina "Ray C" ndani ya sanduku la msanii katika mabano ya mraba - hifadhi na utaona jina hili laonyesha rangi nyekundu. Sasa unaendelea kwa hatua C)
- Bado swali: jina lako laonekana kwangu bila kiungo ukisaini. Je unaitaipu kila mara au unatumia alama ya --~~~~ inayokuwa kiungo cha ukurasa wako pamoja na tarehe ?? ama kwa kuandika alama hizi au kwa kubofya huko juu nafasi ya tatu upande wa kulia? --Kipala 14:21, 13 Septemba 2007 (UTC)
Templeti mwanasiasa
Tafadhali waangalie Zitto na Lowassa. --Kipala 22:24, 14 Septemba 2007 (UTC)
Hongera ya makala 6,000
Oliver na Muddy, hongereeni kwa kusukuma wiki yetu juu ya kiwango cha makala 6,000! Sijui nani kati ninyi wawili aliandika na. 6,000 kwa hiyo hongera kila mmoja! Wakati uliopita nilijatahidi mimi mwenyewe kuandika makala ya kuruka "elfu" ijayo nadhani nilifaulu mara nyingi. Ilikuwa rahisi zaidi kwa sababu hatujakuwa na mashindano sana - kumbe naona itakuwa vigumu zaidi safari ijayo! Kweli nilipoanza disemba 2005 tulipokuwa na makala 140 nisingeota ndoto kufikia hata 2000. Basi tuendelee kushauriana na kuvumiliana ! --Kipala 15:14, 26 Septemba 2007 (UTC)
Hujambo Muddy, ninafurahi kwamba umchangiaji mzuri katika wikipedia ya kiswahili, na kwakufanya hivyo utaongeza nguvu katika kuindeleza.
Nafikiri umeniuliza kuhusu kuandika makala fupi na kutoweka muendelezo wa makala, nikwamba unapoona imekuwa hivyo ujuwe niliandika kwa kutumia simu ya mkononi na uwezo wake ni alfabeti 450 na haina options kwa kuweka viungo. Na hata hivyo huwa ninapenda zaidi ninapoandika makala iwe inachangiwa na watu wengi, sipendi makala ya kuandika pekeyangu sababu ninaamini ya kwamba; Penye wengi pana mengi.
Tazama, mimi nimeandika wewe umetia picha labda na Ndesanjo ataweka kiungo kwenye mji wa Vinci pengine kipala akaandika makala ya mji wa Vinci. Ahsante, tukazemwendo kuendeleza wiki yetu!--User:Joel Niganile 10:57, 26 Septemba 2007
Asante kwa kunihamasisha
Bwana Muddyb, salamu nyingi kutoka Uswidi ambapo nahudhuria mkutano wa lugha za Kibantu mjini Gothenburg. Hasa nakushukuru sana tena sana kwa maneno yako matamu ya kutuhamasisha mimi na Bwana Kipala katika bidii zetu za kukuza wikipedia ya Kiswahili. Siku hizi tumepata msaada mkubwa kutoka kwako; umeshaongeza na kuboresha makala nyingi. Asante sana! Ni tumaini letu la kwamba Waswahili wengi wengine watatuunga mkono katika kazi hiyo ili kamusi elezo kubwa tena yenye manufaa ipatikane wakati mtandao utakapotumiwa na watu wengi Afrika Mashariki. Kwa sasa sina mengi mengine ila kukutakia kila la kheri. --Oliver Stegen 13:46, 3 Oktoba 2007 (UTC)
Templeti "Filamu"
Naomba uangalie templetisasa na ukurasa wake wa majadiliano. Nimenakili maandishi kutoka ukurasa wa Kiingereza. Sasa inatakiwa kubadilisha maneno ya Kiingereza kuwa Kiswahili.
Mfano:
{{#if:{{{producer|}}}| ! Produced by {{!}} {{{producer}}}
kuwa:
{{#if:{{{mtoaji|}}}| ! Imetolewa na {{!}} {{{mtoaji}}}
Jaribisha kidogo ni maneno yapi katika mfumo huo yanayotakiwa kuonyeshwa katika sehemu ya juu penye
| mtoaji =
Kwa jumla sehemu ya juu na ya chini yalingane. --Kipala 12:22, 8 Oktoba 2007 (UTC)
Muundo wa mistari
Salaam, Muddy! Umeona ya kwamba nimepitia makala kadhaa ulizoandika. Nimeona umeanza kutumia sana alama hii ya <br>. So kosa lakini yaleta ugumu kidogo. Ushauri wangu ni usitumie mno <br> ila tu ndani ya masanduku au chini ya picha. Inaleta ugumu kidogo wakati wa kuhariri kwenye dirisha la "hariri". Unapata tokeo unalotaka pia kwa kugonga ENTER mara mbili. Ukifanya hivyo dirisha la "hariri" lasomeka kirahisi zaidi.--Kipala 05:42, 16 Oktoba 2007 (UTC)
Ahsante
Habari Nd. Muddyb, Ahsante kwa kunikaribisha katika wikipedia --SideMontero 14:09, 18 Oktoba 2007 (UTC)
Templeti
Muddy, umeniuliza kuhusu templeti mpya uliyotengeneza. Je umeshaingiza katika makala? Ni rahisi zaidi kuiangalia kazini. --Kipala 10:46, 22 Oktoba 2007 (UTC)
- Sija jaribu bado kwasababu sijaimalizia vizuri. Ile template inataka utulivu sana ili uweze kuifanya makini, Ila kama unataka tuifanyie kazi basi hata sasa hivi tunaweza kujaribu je upo tayari wa hilo?--Muddyb Blast Producer 11:19, 22 Oktoba 2007 (UTC)
- Sawa twende tu. --Kipala 12:13, 22 Oktoba 2007 (UTC)
- Hongera naona ni safi. Nimesahihisha kitu kidogo tu: maelezo ya picha uliandika na mistari ya chini ndani ya mabano lakini bila kwenye jedwali la juu. Lazima jedwali kufuata kila nukta tahajia ya mabano ya tatu ndani ya kipengele. Natumaini minesahihisha kwenye templeti, kwa Angelina na pia Bud Spencer. --Kipala 14:46, 22 Oktoba 2007 (UTC)
- Sawa twende tu. --Kipala 12:13, 22 Oktoba 2007 (UTC)
- Sija jaribu bado kwasababu sijaimalizia vizuri. Ile template inataka utulivu sana ili uweze kuifanya makini, Ila kama unataka tuifanyie kazi basi hata sasa hivi tunaweza kujaribu je upo tayari wa hilo?--Muddyb Blast Producer 11:19, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Tuzo
Naona templeti ni sawa tu. Unaona nji ya kufupisha habari ya kwanza iwe msatri mmoja tu? Labda: Tuzo kwa ajili ya (kama inaingia mstari mmoja; menginevyo kujaribu 80% ingawa sijafanya bado mwenyewe); halafu: Hutolewa na; na "nchi" ingefika nafasi ya pili. --Kipala 07:53, 2 Novemba 2007 (UTC)
- Tuendelee kwa Angelina Jolie --Kipala 14:59, 22 Oktoba 2007 (UTC)
Sawa.--Muddyb 04:49, 23 Oktoba 2007 (UTC)
Templeti Filamu
Naona umehariri mle. Sielewi maelezo yako kuhusu maandishi. Lakini jinsi inavyoonekana katika Makala Bruce Lee - tazama hapa. Naomba uangalie - mimi naondoka sasa karibuni. --Kipala 08:41, 23 Oktoba 2007 (UTC)
- Naomba angalia Template talk:Muigizaji --Kipala 09:42, 24 Oktoba 2007 (UTC)
- Haya Nd Muddy hongera nona umeshafaulu misingi ya screenshot (picha ya kiwamba) sasa mimi naondoka nitaangalia baadaye. --Kipala 15:00, 24 Oktoba 2007 (UTC)
Kompyuta
Naomba anagalia tarakishi na picha niliyoweka. Angalia maandishi ya mchoro ukasahihishe jinsi unaovyoona sawa. Maarifa yangu kuhusu kamusi ni ya kwamba katika mambo ya teknolojia mara nyingi ni bure kwa sababu wanatunga maneno mapya ambayo mara nyingi hayapokelewi badala yake kuna maneno mapya. Hapo ni sharti tufuate kawaida ya watu au hatueleweki. Kama hakuna matumizi bado badi twayaunda hapa wikipedia. Kwa mfano wataalamu wa TUKI wameandika katika KAST "diski ngumu" kwa "hard drive". Usiponiambia ni kweli mnavyosema naendelea kucheka. --Kipala 13:34, 25 Oktoba 2007 (UTC)
Picha
Muddy salaam, napita tu naona waweka picha. Nataka kudokeza tu ya kwamba kuna moto kidogo. Kwa sasa hatunaye kati yetu anayefuatilia sana lakini usishangae kama picha hizi zitafutwa siku moja. Sababu yake ni ya kwamba wikipedia ya kimataifa inayotawala komyuta ambako data zote zatunzwa inataka kuheshimu sheria za hakimiliki. Kuhusu picha maana yake ni ya kwamba kama kuna haki ya yeyote picha isionyeshwe hadi mwenye haki amekubali. Yale yote usome mwenyewe -ukitaka- http://commons.wikimedia.org/wiki/Category:Copyright_statuses
Hali halisi haikubaliki kuchukua picha yoyote inayoonekana mtandaoni bila kuhakikisha una haki ya kuionyesha kwenye wiki. Kwa hiyo njia rahisi ni kuchungulia wiki za lugha mbalimbali na kuchukua huko. Sehemu kubwa ya picha ziko commons, zingine lazima kupakua kutoka wikipedia nyingine. Kila picha katika wikipedia yoyote ni huru kwa matumizi yoyote. --Kipala 13:14, 26 Oktoba 2007 (UTC)
- Mfano ukichukua picha ya :abangida: haiko commons bali katika en:wiki tu. Hii ni sababu haionyeshwi kwetu. Hapa huna budi kufungua picha huko en:wiki, kuhifadhi kwenye PC yako, halafu kuipakia (kuchoto "pakia faili") kwa sw:wikipedia kwa jina unalochagua. Wakati wa kupakia unaingiza URL wa picha katika en:wiki dirishani.--Kipala 13:33, 26 Oktoba 2007 (UTC)
- Muddy naomba usiwe na wasiwasi. Sioni sababu kwako ya kuomba radhi au nini. Ulitamka wasiwasi zako na hii inasaidia kuelewana vizuri zaidi. Mimi niliona vema kushirikiana wewe maarifa yangu yasiyo nzuri sana kuhusu picha - kwa kusudi usikate tamaa kama kitu chatokea baadaye. Kwa hiyo nimefurahia sana kuingia na kuchangia kwako naomba tuendelee! --Kipala 16:15, 27 Oktoba 2007 (UTC)
Maendeleo
Muddy umeniuliza kuhusu Upangaji wa makala, Kueleweka n.k.. Sina budi kusema ya kwamba naona maendeleo makubwa kabisa. Nikitazama makala za karibuni vile Abacha au Shonekan naona ni vizuri. Bado kasoro wakati mwingine katika muundo wa sentensi na tahajia (kwa mfano matumizi ya herufi kubwa baada ya koma). Lakini nakubali unazidi kuendelea bila shaka ni uzoefu wa kuandika Kiswahili unajengwa mara kwa mara. --Kipala 14:23, 29 Oktoba 2007 (UTC)
Bot
Salaam Muddy, akina bot ni watu au zaidi programu zinazofanya uhariri kimachine. Hatuna bot ya sw. Bots zinazofika kwetu kwa kawaida huongeza viungo (links) za interwiki, yaani programu inataka kuingiza viungo katika makala zote za "Dar-es-Salaam"; kwa mfano katika lugha fulani tuseme Kihaussa wameandika makala hii na sasa wanataka kuingiza katika makala za lugha nyingine ya kwamba kuna makala hau:Dar-es-Salaam. Hii unaweza kufanya kwa mkono ukifungua kila ukurasa moja-moja na kuiandika katika orodha ya interwiki au una bongo ya kutunga programu inayofanya kazi hii. (Mimi sina). Bots zingine zinaondoa picha zilizofutwa pale ambako zilipakuliwa mara ya kwanza; kwa mfano kama tatizo letu la hakimiliki limejitokeza picha imefutwa huko en:wiki au commons halafu bot inatafuta picha hii katika wikipedia zote (isipokuwa kama tumebadilisha jina la picha haitapatikana kwa bot, nafikiri). Katika wiki kubwa kuna pia bot zinazosahihisha tahajia lakini sina uhakika.
Menginevyo makala ya Halima James nimependa. Waona utaratibu wa sentensi nakumbuka utaratibu kuwa herufi KUBWA huandikwa majina na mwanzoni wa sentensi baada ya nukta. Hizi koma ni njia ya kupanga ndani ya sentensi kwa hiyo hakuna herufi kubwa (kama si jina). --62.154.201.129 08:42, 30 Oktoba 2007 (UTC)
Mambo
Hi, dear how ? i want to know kiswahili please can you teeach me im very intrested to learn kiswahili. --Suresh Kumar 05:56, 31 Oktoba 2007 (UTC)
Salam Nd. Kumar, Even my self i use learn Kiswahili through Kipala whta's shame it is, i am swahili person but i don't know speak or wtrite swahili gramma, so i'll try my best and i can't promise anything especially training. Thanks--Mwanaharakati 06:02, 31 Oktoba 2007 (UTC)
Rangi
Muddy, salaam! Kuhusu rangi angalia hapa: Webcolors. Ninavyoelewa unaandika majina yale ya juu ya "HTML color names" si nyingine.
Njia nyingine ya kukupa rangi nyingi ni kutumia makala List of colors na kutumia zile namba za Hex triplet zinazoanza kwa alama ya #. (Unaweza kutumia pia namba za hex kutoka makala Webcolors LAKINI hapa ni lazima a) kuongeza alama ya # kabla na kuondoa nafasi kati ya herufi na namba ziwe mfululizo)
Kuhusu jedwali kwa bahati mbaya sitakuwa na muda karibuni. --Kipala 08:28, 31 Oktoba 2007 (UTC)
Muundo makala
Muddy, salaam. Makala mbili ulizotaja naona sarufi (grammar) imesogea mbele kabisa ni safi. Kuna typo kidogo (jinsi ilivyo kwangu pia). Sentensi moja kwa Fonda haieleweki: "mke wa Fonda ambaye ni Seymour mama yao na kina Peter alijinyonga, ndipo Fonda akaamua kuoa mke mwingine" - usingesema kablaya alikuwa mama wa Peter ningefikiri amezaa tena na Peter.
Swali sasa ngazi tofauti:
- tukichukua habari katika en-wiki na kutafsiri - je tuandae viungo kweli kwa majina yote yaliyowekwa huko katika mabano ya mraba? Maana yake unafikiri weli ya kwamba mtu kwetu ataandika juu ya wake wote wa Fonda? Ni swali langu pia mara kwa mara huwa naona mara nyingi niache mabano kama si habari muhimu pia inayotakiwa kuelezwa baadaye. Sipendi makala kuwa nyekundu mno - lakini hii ni swali la kujiamulia.
- Pia ni swali la mara kwa mara tuchague habari gani. Hii ni juu ya kila mtu. Moyo wangu inasema: Habari ya wake 5 sawa, kumtaja mama wa watoto sawa, kumtaja kama mmoja alimgusa hasa - menginevyo mstari moja yenye majina yote ingetosha. Lakini hapa ni swali la kujiamulia kila mmoja wetu.
Ni yale tu, hongera na mandeleo - sasa sipo kwa leo - --Kipala 08:06, 1 Novemba 2007 (UTC)
- HAya, nikinakili orodha katika wiki nyingine na kutaka kuondoa yale mabano ya mraba kuna mbinu labda unatumia tayari; nafungua "edit", nakili sehemu ya orodha katika word. Halafu natumia edit-replace-all mara mbili; kwanza kwa ]] halafu kwa [[. Upande wa replace siandiki kitu hivyo ni kufuta tu. Baadaye nakili katika word na kurudisha katika dirisha la edit. Hii ni njia ya haraka. Badala ya "all" unaweza pia kuthebitisha moja-moja. Haya, wikendi hii niko mkutanoni nakutakia kila la heri --Kipala 22:08, 2 Novemba 2007 (UTC).
Poa Mtu Mzima
Nimekubali maneno yako na nitayafanyia kazi kwani mimi bado mgeni katika wikipedia. Kuelekezana ndio wajibu wetu sisi binadamu. Na nakuomba uendelee kunipa muongoza pale panapo bidi kaka usichoke kwani ndio ukubwa huo. Nakutakia kila la heri -- SideMontero 13:47, 3 Novemba 2007
Asenia / arsenic
Muddy, hii makala iko. Angalia asenia.--Kipala 21:29, 3 Novemba 2007 (UTC)
Makala ya miaka
Salaa, kwa ufupi: haya ni makala ya miaka. Tuna bado idadi kubwa bila kitu ndani yake isipokuwa mpangilio "Matukio - Waliozaliwa - Waliofariki". Oliver alifanya kazi hii kuweka nakala tupu hizi zote za miaka ya BK. Sehemu zimeshapata yaliyomo nyingine bado. Hatuwezi kuingiza kila kitu; mfano: Spaghetti Western ya kwanza (kama inawezekana kuitaja) ingekuwa kitu kinachofaa kuweka kwenye mwaka wa kutokea; filamu yoyote kama si filamu ya pekee kabisa hapana. Filamu ya kwanza yenye sauti au filamu ya kwanza ya rangi au ya Kiswahili - haya yote yafaa. Katika miaka ya kale naona matata kidogo kwa sababu mara nyingi tunaona habari za Ulaya au Asia tu si ya Afrika nje ya Misri kwa sababu sehemu kubwa ya watu wa Afrika hawakuwa na historia ya kimaandishi hivyo si rahisi kusema: jambo fulani lilitokea mwaka fulani.
Miaka ya KK iko pia kwa mfano 333 KK. Lakini si vingi hivi kwa sababu katika historia ya kale kabisa si rahisi tena kutaja jambo lilitokea mwaka ule hasa haiwezekani wka kila mwaka. --91.62.15.156 10:13, 5 Novemba 2007 (UTC)
Ucheki - Czech
Muddy, sielewi vizuri ulikuwa na tatizo gani? Ukiandika "Czech" kwenye dirisha la "tafuta" unafikia mahali pake mara moja bila tatizo.
Nakubali ya kwamba magazeti yanaweza kuandika mara nyingi "czech" lakini sijui watu wanaisoma na kutamka namna gani? Asiyejua atakosa au sivyo? Kwa sababu herufi za Kiswahili yana matamshi tofauti kuliko yale matamshi ya Kiingereza yaliyokuwa kawaida.
Pendekezo la TUKI ni "Cheki au Jamhuri ya Cheki". "Ucheki" ilikuwa njia yangu ya kuifupisha. Nimeongeza tahajia ya "czech" kwenye mwanzo wa makala pia kiungo kwa "Jamhuri ya Czech". Sijui kuna bado njia nyingine kutaja nchi hii? Kwa sasa ukitafuta Czech, Jamhuri ya Czech, Cheki, Jamhuri ya Cheki unafika kwenye makala ileile. --Kipala 18:50, 7 Novemba 2007 (UTC)
Shaaban Robert
Muddy, nimetembelea makala husika na kichwa hapo juu katika wikipedia (kiongozi) ya kiingereza. Kuna makosa yametendeka sasa unaonaje nikiiandika tena upya na kuwapelekea? Au tushirikiane katika hili ili angalau tumjengee heshima muasisi huyu wa lugha yetu tukufu. --Mwanaharakati
Templeti
Naomba uangalie Snoop Doggy - rangi jinsi unavyopenda sasa. Kuhusu jedwali: labda uangalie ulitumia ipi katika makala ya nyuma. Ni kweli ya kwamba jedwali lilikuwa lilelile tangu Oktoba nisipokosei. Kama umenakili jedwali bila kuitambua ingefaa kuibadilisha sasa. Nimerudisha. --Kipala 07:35, 14 Novemba 2007 (UTC)
Kuanzisha makala - interwiki kutoka simple.wiki
Mara nyingi nikianzisha makala natumia simple.wikipedia. Haya ni makala yanayoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kisicho kigumu (angalau hivyo ndivyo inavyokusudiwa). Nafanya hivyo hasa kwa sababu ya kiungo cha en.wiki. Nikinakili interwiki kutoka simple kumbe en:xyz imo ndani; nikinakili interwiki kutoka en.wiki nakosa kiungo cha makala ya en.wiki yenyewe nahitaji kuiongeza kwa mkono.
Sababu ya pili ni ya kwamba mara nyingi napata picha ya makala mafupi yawe na habari gani. Yaani makala ya en.wiki yanaweza kuwa marefu sana na kuna swali kuifupisha namna gani. Hapa simple inaweza kusaidia ingawa mara nyingi sipendi jinsi walivyofanya. Basi angalau napata picha. --Kipala 16:11, 14 Novemba 2007 (UTC)
Barnstar
Muddy, wauliza swali gumu. Sijui maana ya barnstar lakini naweza kusoma haya: en wiki khusu barnstar. Naona ni alama ya kumpomgeza mwanawikipedia kama mtu anataka kumsifu. Ila tu ni desturi ya kiamerika kabisa kwa hiyo sidhani ingekuwa hoja zuri kuipokea katika sw:wiki moja kwa moja. Tukiwa watu wasiozidi kumi wanaochangia mara kwa mara tunaweza kuendelea bila tuzo au nini.
Wengine wamecheza kidogo na hoja la barnstar kwa mfano Wajerumani, Wafaransa, Wasweden,Waserbia, Wafinland, Wakroatia, Wahispania wote wameunda kitu kisichonakili utamaduni huu wa Marekani. --Kipala 15:46, 18 Novemba 2007 (UTC)
- Muddy, umeshakuwa m,tu mzima hapa wiki. Amua mwenyewe. Tafakari 1) unataka aina gani yaani unataka kupongeza aina gani ya kazi? (tuzo moja kwa yote, au kufuatana na idara au vichwa?). Halafu nembo gani? Ile barnstar ni Marekani - wengine walitunga kwa kuunganisha kusifu na kutania kidogo; landa kucheza kidogo na nembo zinazojulikana kama mwenge, jogoo, pinde/mshale, mkuki, ndizi na chungwa, n.k. --Kipala 11:49, 19 Novemba 2007 (UTC)
Thank you very much for your support on my article. --BBKurt 00:01, 1 Desemba 2007 (UTC)
aftermath
Salaam Muddy naomba angalia maendeleo ya swali lako huko kwa Oliver. --Kipala 12:49, 1 Desemba 2007 (UTC)
Lugha: bamba nk
Muddy unaongelea mambo muhimu sana. Ni kweli ya kwamba katika makala za kisayansi natumia hasa Kiswahili cha Kamusi (kwa mfano KAST. Nimeshahisi ya kwamba sehemu ya maneno haya hayaeleweki kwa msemaji mwenye elimu ya wastani. Ni kwa njia ya majadiliano tu kuona kiasi gani hakieleweki rahisi.
Njia mbele kwa wazo langu ni koboresha maelezo si kuongeza Kiingereza. Sababu mbili:
A) si wasemaji wote wa Kiswahili wanaojua Kiingereza (hata kama ni wengi kati ya wasomi) lakini Kiswahili huongelewa pia Kongo ambako lugha kuu ni Kifaransa.
B)itasaidia nini kama msomaji hajui maneno yale ya Kiingereza kwa sababu hajawahi kusikia habari zinazoongelewa. Samahani nikiuliza lakini "tectonic plates" itasaidia nini? Kama mtu hana habari bado kuhusu muundo wa kijiolojia wa dunia yetu si rahisi kuelewa "plate" yamaanisha hapa kitu gani. Hapa anapaswa kusoma na kufuata maelezo ya viungo.
Kwa hiyo njia mbele ni maelezo bora na rahisi zaidi kwa Kiswahili. Unaonaje, kama badala ya
"Mfereji huu uko kando ya Visiwa vya Mariana karibu na Guam. Ni mahali ambako bamba la Pasifiki hujisukuma chini ya Bamba la Ufilipino" iwe sasa
"Mfereji huu uko kando ya Visiwa vya Mariana karibu na Guam. Ni mahali ambako vipande viwili vya ganda la dunia vyagusana na hasa bamba la Pasifiki hujisukuma chini ya Bamba la Ufilipino". Halafu katika makala bamba la Pasifiki kuongeza elezo ya kwamba "bamba" hapa ni kipande cha ganda la dunia kinachoelea juu ya kiini cha kiowevu ndani ya dunia.
Unaonaje? --Kipala 11:29, 3 Desemba 2007 (UTC)
Muddy namoba uangalie makala mawili yanayotajwa hapo juu kama zinaeleweka. Kila kasoro au swali unayoona bado naomba uandika kwenye ukurasa wa majadiliano. --Kipala 14:23, 4 Desemba 2007 (UTC)
Kiesperanto
Salaam, Muddy! Kiesperanto ni lugha ya kimataifa, na siyo lugha ya nchi moja au nchi chache tu. Kama unavyoweza kusoma katika makala Kiesperanto, lugha hiyo imepangwa na L.L.Zamenhof ambaye alikuwa na nia ya kutengeneza lugha rahisi ili iwe lugha saidizi ya kimataifa. Ingawa siku hizi Kiingereza inatumika zaidi kimataifa, Kiesperanto bado inatumika na watu mbalimbali katika karibu nchi zote duniani. Mimi nilipokuwa Tanzania, nilikutana na Waesperanto wanne (wawili jijini Dar es Salaam, moja jijini Arusha na moja mjini Bunda). Kila siku ninawasiliana kwa mtandao na waesperanto wanaotoka mataifa mengi mbalimbali. Maelezo mengine kuhusu Kiesperanto yanapatikana hapa. Ukiwa bado na maswali kuhusu Kiesperanto, naweza kukujibia. Marcos 21:45, 11 Desemba 2007 (UTC)
- Salaam nyingi, Ndugu Muddyb! Nipo tayari kukusaidia ukijifunza Kiesperanto. Nitumie maandishi yako, na mimi nitayasahihisha. Marcos 00:55, 13 Desemba 2007 (UTC)
Wiki za Afrika
Muddy huko awali sikujibu kuhusu kichwa hiki. Lakini nakubali unavyosema. Bado naona tunahitaji kupanusha msingi wetu yaani idadi ya wachangiaji. Nikiangalia historia yetu tulikuwa wachache mno. Sehemu kubwa ya makala imechangiwa na Oliver na mimi; tangu wewe kuingia tumekuwa watatu. Halafu yupo ChriKo na ndege zake. Zamani walikuwepo watu kadhaa lakini (Ndesanjo, Marcos, SJ, MattCrypto, Joseph, huyu kijana wa Tanga) kwa jumla waliacha ama wamepotea kabisa au wanaonekana mara chache tu. Sijui namna ya kupata wenyeji zaidi. Nasadiki ya kuwa jinsi tunavyoonekana zaidi tukipatikana kwa njia ya google watu wanatufikia bila kutegemea. Hii inaonekana polepole.
Humjuimwalimu anayependa kujaribu kitu pamoja na wanafunzi wake? Hiyo ndiyo nafasi ninayosubiri... --Kipala 12:33, 12 Desemba 2007 (UTC)
- Ninachomaanisha ni hivyo: njia nzuri ya kujenga wikipedia ni ushirikiano na shule au chuo. Sharti ni shule au chuo penye nafasi ya kompyuta. Pia mwalimu aliye tayari kufundisha kwa njia ya mradi. Najua si kawaida sana TZ ingawa ni njia nzuri sana ya kufundisha. Menginevyo shule penye mfadhili atakayesaidia matumizi ya kompyuta?
- Mfano kwa wanafunzi wa sekondari: kila mwanafunzi anaandika makala fupi kuhusu kijiji anapotoka yeye au wazazi wake. Waelezwe awali masharti ya muundo wa makala. Halafu watunge na waelezane katika vikundi walichotunga. Kundini wafanye masahihisho, kama vile kumpa mwandishi kazi ya kufupisha, kuongeza, kutafuta habari za nyongeza, kuandika sehemu upya, kunyosha lugha... Kama ni sawa ama yoze itambulishwe mbele ya darasa au mwalimu anaona imetosha katika vikundi halafu inapelekwa wikipedia.
- Kwenye ngazi ya chuo inawezekana kushughulika maada kiasi nzito zaidi. Labda kueleza maisha ya watu wa siasa au historia; au wataalamu n.k. Hii inategemea na aina ya chuo.
- Faida ya e kwa mwalimu ni: anapata mradi (yaani "teaching project") wa kuvutia na wanafunzi wake wataipenda. Itaonekana baadaye haitabaki kama daftarini tu. Anafundisha namna ya kupanga ujuzi na kutafuta habari.
- Kwetu hapa ni njia isiyo ya kigeni. si jambo la kompyuta tu hata zamani kazi ilifanywa kwa kijitabu cha darasa tu katika somo fulani. Siku hizi ni mara nyingi ya kwamba wanafunzi wanatunga kitu ama kwa tovuti ya shule au kwa kamusi fulani mtandaoni. --Kipala 13:43, 12 Desemba 2007 (UTC)
- Muddy hapa nakubali kiasi mengine hapana. Ni kweli ya kwamba maisha ni magumu na utamaduni ni kujipatia kitu. Lakini si watu wote. Makanisa na misikiti hutegemea watu wa kujitolea. Wengine wanafanya wakiamini ya kwamba watapata kitu katika ahera lakini kwa wengine imeshakuwa mwelekeo wa maisha. Hata nje ya maisha ya kidini wako.
- Nikiongelea nafasi ya shule najua ya kwamba wako walimu (labda wasio wa kawaida) wanaojaribu kutumia mbinu nyingi wa kuwalea wanafunzi wao. Tatizo ni kumpata akiwa katika shule penye nafasi ya mitambo. Hii jambo gumu Tanzania. Naendlea kuota ndoto. --Kipala 14:42, 12 Desemba 2007 (UTC)
Wiki ktk google
Muddy, sijui kwanini ni hivyo. Binafsi sijali sana. Naona zaidi faida kama makala zetu zaonekana tofauti na zile za Kiingereza kwa sababu ni rahisi zaidi kuzitafuta katika orodha. Kama tungepata mstari kwa Kiswahili - vizuri zaidi. Lakini sina picha hata kidogo namna gani kuibadilisha. Kwa sasa nasubiri kama Matt a) anasoma yale niliyoandikakwake na b) kama yeye anajua njia ya kuondoa kosa lile katika dirisha letu "Viungo viungacho..." --91.62.19.185 12:59, 13 Desemba 2007 (UTC)
Asante
Muddy asante kwa sakamu zako. Na mimi nakutakia baraka kwa kipindi hiki pamoja na mwaka mpya. Nakutakia starehe wakati wa sikukuu hizi na mwanga moyoni kutoka kwa Mungu. Amani hii ya Krismasi ni tamko kwa watu wote "aliopendezwa nao". Basi ubarikiwe na tuendelee kushikamana. --Kipala 10:08, 24 Desemba 2007 (UTC)
Idd
Muddy, nisamehe nilisoma haraka salamu zako ni kweli sijakupa hongera ya Idd!! Basi nafuata sasa njia ya kikatoliki ingawa mimi si mkatoliki nakutolea malipizi ya kitubio kwa kuandika makala ya Idd-al-Hajj. Naomba ukubali! --Kipala 21:22, 26 Desemba 2007 (UTC)
airport
Muddy naomba nisaidie lugha. Airport - je mnasema uwanja au kiwanja cha ndege? Kamusi za TUKI zatumia zote mbili na mimi sikumbuki vizuri. Ile ya Dar inaitwaje? --Kipala 08:48, 29 Desemba 2007 (UTC)
Glorious Seven
Muddy makala ni nzuri lakini naona matata kadhaa upande wa kueleweka sawasawa. Lakini hapa mimi niko mbali sina uhakika kama ni tatizo langu tu. Labda umpatie mtu huko uone anachosema. Tatizo ni kama tunatafsiri tunapokea amri za lugha nyingine. Sasa ni swali tufanye nini kama lugha yetu haina dhana mbalimbali kwa mfano "gunslinger", "gunman"? Ni lazima kufuata muundo wa dhana za hadithi ya Kiingereza au heri tuweke haya kando na kusimulia upya? Nimeanza kuandika masahihisho kadhaa lakini inaonekana ingekuwa badiliko kubwa. Kama wenyeji wa huko wanaelewa verma ibaki ilivyo. Menginevyo niambie nitatuma yangu. --Kipala 11:49, 29 Desemba 2007 (UTC)
Sema --Kipala 13:44, 29 Desemba 2007 (UTC)
Asante kwa sahihisho la Schiphol. Nimeweka yangu kwa Magnificent Seven. Ila tu sina muda wa kuchungulia zaidi. Pia hata yangu imekuwa kirefu mno. Nimeona pia kwangu mwenyewe nikianza kutafsiri makala marefu kunatokea ugumu wa lugha kuliko nikifupisha. Nikifupisha napaswa kuwa na lugha yangu. Nikitafsiri mengi nasukumwa na dhana za Kiingereza au Kijerumani au nini na tokeo lake ni lugha nygumu. Naona imetokea kwako pia katika makala hii. --Kipala 14:29, 29 Desemba 2007 (UTC)
Re:Muda umefika
Muddy, asante kwa kuniarifu kuhusu mipango yako. Kwanza nakupa hongera kwa azimio la kuingia masomoni tena. Je ni kozi gani unayosoma? Labda niandikie kwenye email.
Halafu: naona huzuni utakapoonekana mara chache tu lakini naomba sana usiache wikipedia kabisa. Kama huwezi kuchangia kila siku basi angalau naomba tenga siku moja mmbili kwa juma. Oliver kwa mfano ana mtindo anapoandika makala akiwa safarini na kupakia faili akipata nafasi kwenye kompyuta tena. (Je una kastiki ya USB? Sijui huko TZ lakini kwetu bei imekuwa nafuu sana inasaidia kubeba data mfukoni.) Basi nakutakia heri za mwaka mpya na baraka zote! --Kipala 13:36, 1 Januari 2008 (UTC)
Swali la kutia sahihi
Nikikuelewa vema nafasi iko hata hapa kwetu. Ukitazama dirisha hili la "Kuhariri" unaona hizi oicha ndogo juu yake. Ukibonyeza picha ya tatu kutoka upande wa kulia unapata alama za --~~~~. Alama hizi zinatafsiriwa na programu kuwa sahihi na tarehe mara ukihifadho maandiko yako. --62.154.201.129 09:28, 5 Januari 2008 (UTC)
- Utazame ukurasa wangu wa majadiliano. Nimebadilisha "nickname" yangu kuwa "user talk:Kipala". Mengine sijui. --User_talk:Kipala 11:37, 5 Januari 2008 (UTC)
Jamii ya "Watu na Maisha"
Bwana Muddyb, salaam! Naomba usiendelee kutumia jamii ya "Watu na Maisha" wakati ukimaanisha 'category' ya Kiingereza "Living People". Jamii hii itafsiriwe kama "Watu Walio Hai". Nimeshaanza kubadilisha jina la jamii katika kila makala. Ukiingiza makala mpya zenye jamii hiyohiyo utaongeza kazi ya kubadilisha baadaye bure. Asante kwa kuelewa kwako. Nakutakia kazi njema (pamoja na masomo mema ulivyoandika siku kadhaa zilizopita)! Wasalaam, --Oliver Stegen 19:07, 17 Januari 2008 (UTC)
TV
Wauliza habari ya picha. Unamaanisha picha namna gani? Upande gani - uüande wa kamera au ya skrini? --User_talk:Kipala 14:34, 23 Januari 2008 (UTC)
- Kuhusu picha: kimsingi kamera inagawa eneo la picha katika nukta au miraba mingi midogo ("pixel"). Picha nzuri imegawiwa kwa pixel maelfu, picha ileile kama imegawiwa kwa pixel chache inatokea vibaya zaidi. Kwa kila nukta/pixel Kamera inashika habari juu ya rangi na pia juu ya mwangaza (kiwango cha mwanga au giza).
- Tazama picha hii niliyokata kutoka picha katika makala yako ya "Harusi ya Candy" ni sehemu ya macho tu (fungua picha pekee yake utaona miraba mitupu). Nilivyoongeza ukuwa pixel zaonekana vizuri. Habari hizi za rangi na mwangaza pamoja na habari juu ya mahali pa pixel zinabadilishwa kuwa ishara elektronikia. Kwa upande mwingine seti ya TV inapokea habari hizi na kufanya kinyume: inaonyesha kwa kila nukta katika nafasi ya skrini mwangaza na rangi jinsi inavyoambiwa. Nukta au pixel zote pamoja ni picha kamili machoni petu. Kazi ya TV ni kupeleka ishara elektronikia hewani kati ya antena na antena. Kuna maelezo mafupi katika makala ya au --User_talk:Kipala 22:07, 23 Januari 2008 (UTC)
Kufutwa kwa user:Muddy
Nisamehe kweli nimekuelewa vibaya. Basi naona umejenga upya. Kwa hiyo nirudishe ukurasa wa awali au nisirudishe? Naona ukurasa wa majadiliano umesharudi. Kwa hiyo bado unataka nifute makala http://sw.wikipedia.org/wiki/Muddyb_Blast_Producer ? Heri niulize tena! --User_talk:Kipala 15:32, 24 Januari 2008 (UTC)
- Basi imerudi. --User_talk:Kipala 07:25, 25 Januari 2008 (UTC)