Wilaya ya Mtwara Vijijini

(Elekezwa kutoka Mtwara Vijijini)

Wilaya ya Mtwara Vijijini ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Mtwara.

Mahali pa Mtwara Vijijini (kijani) katika mkoa wa Mtwara.

Wilaya hii imepakana na Msumbiji upande wa kusini, Wilaya ya Tandahimba upande wa magharibi, Mkoa wa Lindi upande wa kaskazini na Mtwara Mjini pamoja na Bahari Hindi upande wa Mashariki.

Eneo la wilaya ni kilomita za mraba 3,597 km². Mto mkubwa ni Ruvuma ambao ni pia mpaka wa Msumbiji.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 158,504 [1]. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 228,003 [2] waishio humo.

Wakazi walio wengi ni Wamakonde na Wamakua.

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Sensa ya 2012, Mtwara DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-17.
  Kata za Wilaya ya Mtwara Vijijini - Mkoa wa Mtwara - Tanzania  

Dihimba | Kitere | Libobe | Lipwidi | Madimba | Mahurunga | Mangopachanne | Mayanga | Mbawala | Mkunwa | Moma | Mpapura | Msanga Mkuu | Msimbati | Muungano | Nalingu | Nanguruwe | Naumbu | Ndumbwe | Tangazo | Ziwani


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mtwara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mtwara Vijijini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.