Muigizaji Elizabeth Micheal

Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ni mwigizaji wa kike wa Tanzania aliyezaliwa Aprili 16, 1999.mwaka 2013 alishinda tuzo ya kitaifa katika tamasaha la filamu la Zanzibar kama mwigizaji bora wa kike kwenye kategoria ya ''Mwanmke wa kanuni''. pia mwaka 2016 alishinda tuzo ya ''Africa Magic Viewer's Choice Awards'' kama muigizaji bora wa kike afrika mashariki[1]. Mwaka 2017 muigizaji huyu alitajwa kama washiriki wnaowania tuzo ya mwanamke chipukizi mwenye mvuto katika jamii[2][3] .Mwaka 2017 muigizaji huyu alishtakiwa na kesi ya mauaji ya muigizaji maarufu Steven kanumba na kupewa kifungo cha miaka miwili jela ila mwaka 2018 alikuwa miongoni wa wafungwa waliopewa msamaha wa mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli amabapo kifungo chake kilipungua na baadae aliachiwa huru Mei,9,2018 baada ya kutumikia kifungo cha miezi sita jela na kufuanya huduma za kijamii kwa muda uliobaki baada ya kuonekana kuwa na tabia njema alivyokuwa jela[4] . Mwaka 2018, Novemba 12 muigizaji huyu alimaliza rasmi kifungo chake alichokuwa akikitumikia [5]

Maisha ya awali na Elimu

hariri

Elizabeth micheal alizaliwa na kukulia mkoani Dar es Salaam, Tanzania. baba yake Elizabeth alikuwa anaitwa Micheal Kimemeta na mama yake alikuwa anaitwa Lucrecia Kalugiira. Elizabeth alisoma katika shule ya msingi ya Remnant Academy pia alisoma shule ya sekondari perfect vision na shule ya sekondari St Marys ambapo alichukua elimu yake ya kidato cha tano na cha sita. pia elizabeth alisoma chuo cha Utumishi wa umma ampabo alisomea diploma ya usimamizi wa rasimali watu.

kazi ya uigizaji

hariri

Elizabeth micheal alianza kuigiza alivyokuwa mtoto akiwa na miaka mitano ambapo alianza kuigiza na muigizaji nguli ambaye ni Mahsein Abdallah almaarufu kama Dr cheni. muigizaji huyu ndiye aliyegundua kipaji cha lulu au elizabeth micheal na kumpeleka katika kikundi cha kuigiza cha kaole. hapo ndo safari ya lulu ilipoznaza rasmi na kuanza kuonekana kwenye televisheni na kuigiza kwenye maigizo mbali mbali kama Dira ambalo ndo lillkuwa igizo lake la kwanza kabisa na mengineyo kufuata kama Zizimo,Bragumu,Gharika ,Taswira na Demokrasia. Filamu hizi zote ziliigizwa miaka ya 2000 [6] . elizabeth alianza kutumia jina la Lulu kama muhusika katika filamu ya Misukosuko ambapo filamu hii ilijizolea umaarufu mwaka 2005.


elizabeth micheal alianza kushiriki kwanye dili kubwa kama kuwa miongoni ya wahusika kwenye tamthilia ya redio ya Wahapahapa mwaka 2009 amababo ilikuwa ikisambazwa na kampuni ya kitaifa ya midia ya Tanzania akichukua uhusika wa Mainda huku akieleza umuhimu wa mazungumzo ya mzazi na mtoto kwa kulinda ujana pale wanapopitia changamoto za kubalehe. kazi hii ilikuwa chini ya usimamizi wa Jordan Rider. Baada ya hapo muvi alizoigiza ni kama zifuatavyo Machozi ya Fmilia, Kiwimbi cha machozi, Oksijeni, Mfanyakazi wa ndani wa kiume na Mwanamke wa kanuni hizo ni baadhi za filamu ila aliigiza na pia kuonekana kwenye filamu zaidi ya 20


Agosti mwaka 2013 aliiachia filamu yake iitwayo Foolish Age[7] (balehe) ambapo filamu hii alitumia nguvu kubwa kama mtayarishaji na kuizindua katika kumbi za Mlimani City, Dar es salaam na kuoneshwa kwenye tamasha la kitaifa la filamu Zanzibar mwaka 2014. na filamu hii ilimpelekea kushinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike kwenye tuzo za watu pia ilitajwa kuania ilamu bora kwenye hizo Tuzo za Watu.


mwaka 2015 aliachia filamu yake ya pili iitwayo Mapenzi ya Mungu(Gods Love) ambayo alicheza kama muhusika mkuu na filamu hii ilioneshwa kwenye tamasha la kitaifa la filamu Zanzibar pia filamu hii ilishinda katika tuzo za chaguo la watu Afrika mwaka 2016 kama filamu bora ya afrika mashariki. julai mwaka 2016 aliachia muvi yake ya tatu aliyotyarisha na kuiongoza inayoitwa Ni Noma.filamu hii ilikuwa inauzwa kwenye app za simu janja.

Maisha Binafsi

hariri

Oktoba Mwaka 2018 Elizabeth Micheal alichumbiwa na Francis Ciza almaarufu kama Majizzo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya redio iitwayo Efm na Television Iitwayo TVE [8] na baada uchumba elizabeth akaolewa mwaka 2021 tarehe 17 mwezi wa 7 na kufanikiwa kupata mtoto wa kwanza wa kiume kwa jina la Genesis na mwaka 2022 Desemba alipata mtoto wa pili wa kike kwa jina la Gracious.

Orodha ya kazi za kibalozi, kazi za kuidhinishwa pamoja na kazi za kivyama

hariri
  • mwaka 2013, elizabeth micheal alichaguliwa kuwa balozi wa tamasaha la filamu la Tanzania katika filamu yake ya Folish Age (Balehe)
  • Februari mwaka 2014 alisaini mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya simu ya Airtel kama muongozaji wa kipindi cha Airtel Yatosha.
  • Mwaka 2015 alisaini mkataba wa kibalozi katika kampuni ya Pisha Tanzania na kuwa Balozi wa app ya simu janja ya Paisha Tanzania.
  • mwaka 2016 alisaini mkataba wa kuwa balozi wa bidhaa za watoto na pedi za kike katika kampuni ya Hengan na Freestlye.
  • Oktoba 2017 alitajwa kuwa balozi wa tuzo za filamu za Sinema Zetu (SZIFF)
  • Machi 2019 alikuwa muongozaji wa Tuzo za kitaifa za filamu Sinema Zetu.
  • Februari mwaka 2020 alisaini mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya kisimbuzi cha DSTV
  • Alisaini mkataba na kampuni ya Azania kama balozi wa Unga ya Ngano ya Azania
  • Kwanzia mwaka 2020 mpaka 2021 alikuwa balozi wa simu ya Tecno nchini Tanzania.

Orodha ya sinema alizoigiza

hariri
Mwaka Jina la Tamthilia Jina la Uhusika Watayarishaji wa hizi Filamu
2000 Dira Nemu Televisheni ya ITV
2001-2006 Zizimo Lulu
Taswira
Baragumu
Gharika
Sayari
Tufani
Tetemo
Jahazi
Demokrasia pia tamthilia hii ilikuwa inarushwa kwenye Televisheni ya Taifa
2006–2010 Watoto Wetu *Muongoza Kipindi kipindi cha Watoto katika Televisheni ya ITV
2014–2015 Tanzania Movie Talents (TMT) *Muongoza kipindi Televisheni ya ITV katika kipindi cha mashindano ya kuigiza
Jan 2018-2020 Sarafu Jackline Sanga "Jacky" Aired on Maisha Magic Bongo (Dstv Channel).
2021 Mimi Naomi Yeye alikuwa mtayarishaji pamoja na muongozaji msaidizi

Tamthilia za Redio

hariri
Mwaka Filamu uhusika Redio
2009 Wahapahapa Mainda ilirushwa kwenda Radio One Tanzania and Radio Free Africa

Filamu

hariri
Mwaka Filamu Jina la uhusika waigizaji alioigiza nao
2005 Misukosuko Part 2 Catherine Jimmy Mponda, Seba and Salama Salmin (Sandrah)
2006 Wema Betty Senga
2007 Silent Killer (Muuaji Mkimya) Mohamed Nurdin (Chekibudi) pamoja na Shumileta
2008 Family Tears Lindah Steven Kanumba, Wema Sepetu, Jacqueline Wolper and Richard Bezendhout
Mtoto wa Nyoka
Lost Twins Anita (young) Steven Kanumba, Hashimu Kambi, Suzan Lewis.
2009 Taste of Love Martha Aunty Ezekiel, Blandina Chagula, Mahsein Awadh.
Ripple of Tears Lizy/Smiles Steven Kanumba
Passion Jacqueline Wolper, Irene Uwoya, Yusuph Mlela, Hashim Kambi
Unfortunate Love Steven Kanumba, Lisa Jensen, Zamda
Too Late ( Umeshachelewa) Mahsein Awadh (Dr Cheni), Tumaini Bigirimana (Fifi), Issa Mussa
Reason To Die Nyina Mahsein Awadh (Dr Cheni)
2010 Family Disaster Julieth Vincent Kigosi na Diana Kimaro
Crazy Love (Mapenzi ni ukichaa) Student Steven Kanumba, Shamsa Ford na Hemed Suleiman
Magic House (Jumba la Dhahabu) Dorah Steven Kanumba ,Nargis Mohamed
My dreams ( Ndoto Zangu) Jane Vincent Kigosi, Irene Uwoya, Shamsa Ford, Mahsein Awadh
2011 Birthday Party Salma Jabu (Nisha)
Ritazo Ritazo Riyama Ally
Tattoo Bridget Steven Knumba na Vicent Kigosi
Confusion Besta Diana Kimario, Hemedi Suleiman
2012 House Boy Lulu Wema Sepetu, Kajala Masanja and Mr Blue
Woman Of Principles Linah Vincent Kigosi and Nargis Mohamed
Dangerous Girl Hidaya
Mtoto wa Mbwa Nice Simon Mwakapagata (Rado)
Yatima Asiyestahili Njwele Nice Mohamed and Jeniffer Kyaka
Oxygen Sydney, Hashim Kambi, Grace Mapunda
2013 Foolish Age Loveness Alikuwa mtayarishaji mkuu huku akiigiiza na Diana Kimaro pamoja Hashimu Kambi
2014 Family Curse Hashimu Kambi, Yusuph Mlela, Cathy Rupia
2015 Mapenzi Ya Mungu Shikana Also Producer

With Flora Mtegoa, Linah Sanga

2016 Ni Noma Angela alikuwa mtayarishaji na aliigiza na Kulwa Kikumba pamoja isarito Mwakalikamo

Marejeo

hariri
  1. https://www.bing.com/ck/a?!&&p=c43565d92d538254JmltdHM9MTY4NDQ1NDQwMCZpZ3VpZD0wNjJmMzRlYi03NWU0LTYxMDMtMGQzMC0yNjQxNzQ1NjYwYTgmaW5zaWQ9NTQ4NA&ptn=3&hsh=3&fclid=062f34eb-75e4-6103-0d30-2641745660a8&u=a1L2ltYWdlcy9zZWFyY2g_cT1hZnJpY2ErbWFnaWMrdmlld2VycytjaG9pY2UrYXdhcmRzK2x1bHUmaWQ9NEM1QjQ5QURGNDg5OUY0QkQxMzE4OTYxQTM1Q0FEREQxODM3NjBBMiZGT1JNPUlRRlJCQQ&ntb=1
  2. https://en.wikipedia.org/wiki/Elizabeth_Michael#cite_ref-5
  3. https://en.wikipedia.org/wiki/Elizabeth_Michael#cite_ref-6
  4. http://nairobiwire.com/2018/05/why-tanzanian-actress-elizabeth-michael-has-been-released-from-prison.html
  5. https://www.thecitizen.co.tz/magazine/thebeat/Freedom-for-Lulu-at-last-after-six-long-years/1843792-4855022-2h7tf3z/index.html
  6. http://swahiliworldplanet.blogspot.com/2014/04/birthday-girl-lulu-elizabrth-michael.html
  7. https://web.archive.org/web/20160827222612/http://www.8020fashionsblog.com/foolish-age-premier/
  8. https://www.pulselive.co.ke/entertainment/elizabeth-lulu-holds-traditional-wedding-days-after-completing-jail-term/807wq2w