Muziki wa klasiki
Muziki wa Klasiki upo katika aina za orchestra (muziki unaopigwa na jopo la watu au kwa jina lingine waweza kuitwa bendi). Asili ya muziki huu ni hasa kwenye utamaduni wa Kimagharibi na hasa kwenye muziki wa liturujia.
Kwa kawaida hulenga ala za nyuzi, yaani Violin, viola, cello, na besi-mbili ambavyo vyote ni vyombo vya nyuzi; kwa pamoja, vinategemeana kufanya orchestra.
Wanaorchestra wana mwelekezaji wao (kondakta) ambaye anaweka sawa tempo (kasi au mdundo), na anawaelekeza wanaorchestra kwa kutumia fimbo maalum wakati wanapiga moja kati ya nyimbo ambazo huzipiga kwa maonyesho maalum.
Kuna watunzi kedekede wa muziki wa klasiki. Lakini hapa pana orodha ndogo ya watunzi hao kwa mwenendo wa nyakati:
Zama za Kati
haririMtindo wa Zama za Kati ulienea sana kunako karne ya 5 hadi kwenye karne ya 15 na waliotingisha walikuwa kina:
Zama za Mwamko
haririMtindo wa Renaissance ulibamba sana kuanzia karne ya 15 hadi karne ya 17 na waliotingisha walikuwa kina:
Kipindi cha Baroko
haririBaroko ilikuwa kipindi kuanzia takriban mwaka 1600 hadi 1750. Wakati huo walitinga hasa:
Kipindi cha Klasiki
haririKatikati ya karne ya 18 hadi kunako miaka ya 1820 ilikuwa ikijulikana kama Kipindi cha Classical yenye watunzi maarufu kama:
Kipindi cha Romantiki
haririKipindi hiki kilianza kunako 1820 na kudumu hadi 1910; kilijukana kama Kipindi cha Romantiki na kutoa watu kama:
Karne ya 20
haririKile kinachojulikana kama Muziki wa klasiki wa karne ya 20 umekuja kuanzia 1910 na kuendelea na watunzi wafuatao na wengineo:
- Claude Debussy
- Maurice Ravel
- Arnold Schoenberg
- Igor Stravinsky
- Bela Bartok
- Benjamin Britten
- Dmitri Shostakovich
- Phillip Glass
- Dmitri Kabalevsky
Kwenye karne ya 20, muziki wa klasiki umebadilika sana. Kuanzia mwaka 1950, ala za umeme zilianza kutumika kwa kutengeneza sauti mpya, na vifaa vya muziki vya umeme vikaanza kutumiwa katika kufanyia muziki huu vilevile.
Tangu mwaka 1970, watunzi wengi wa muziki huo wakaanza kutofautisha baina ya muziki wa rock, pop, classical, asili, jazz na muziki wa dunia, kwa kutoa aina mpya za mitindo ili kuendeleza fani nzima ya muziki.
Viungo vya nje
haririEuropean classical music travel guide kutoka Wikisafiri
- Historia ya Muziki wa Klasiki
- Video ya wanamuziki mashuhuri wa Muziki wa Klasiki
- Video ya nyimbo 50 maarufu za Muziki wa Klasiki
- Ala za Muziki wa Klasiki
- Zana bora za kusikiliza Muziki wa Klasiki Ilihifadhiwa 14 Julai 2018 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muziki wa klasiki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |