My Love
"My Love" ni moja wa wimbo wa Westlife, ulitolewa kama singo kutoka katika albamu yao ya Coast to Coast.
“My Love” | ||
---|---|---|
Single ya Westlife | ||
Muundo | CD Single | |
Aina | Pop | |
Mtunzi | Jörgen Elofsson, Per Magnusson, David Kreuger |
Wimbo wa 'My love' ndio ulikuwa wimbo wa saba kufika katika nafasi ya kwanza katika chati ya Muziki ya uingereza. Wimbo huo ulishika nafasi ya thelathini na tano katika nyimbo zilizoongoza kwa mauzo kwa mwaka 2000, nchini Uingereza.
Mpangilio wa Nyimbo
haririCD Ya Kwanza
hariri- My Love (Radio Edit) - 3:52
- If I Let You Go (USA Mix) - 3:40
- Enhanced Section
CDm Ya Pili
hariri- My Love (Radio Edit) - 3:52
- My Love (Instrumental) - 3:52
- Enhanced Section (Including "My Love" Video)
Nyimbo za Video
haririkwa upande wa video ya wimbo huu. Wimbo unaanza wakiwa katika Stesheni ya reli, ambapo, Nicky Byrne anawataarifu wenzake kuwa, ndege yao iliyokuwa inafuatia imeahirishwa. Wenzake wanakasirika kutokana na habari hiyo, ambapo Bryan anasema kuwa, yeye anaenda nyumbani. Wengine wanamfuata na ndipo wimbo unaanza.
Shairi la kwanza linafanyika ndani ya uwanja wa ndege, na wakati wa kiitikio, mandhari inabadilika na kuwa eneo la mjini. Baada ya kiitikio cha kwanza kumailizika, mandhari inabadilika tena na kuwa katika eneo la barabara kubwa. Halafu tena katika Kiitikio cha pili, mandhari inabadilika na kuwa katika eneo la pwani. Halikadhalika katika kiitikio cha mwisho kundi hilo la Westlife, wanaimba wakiwa katika kilele wakionesha bahari pembeni mwa barabara kubwa.
Mtiririko wa Nyimbo
haririChati | Ulipata Nafasi |
---|---|
Argentine Nafasi ya singo | 1 |
Australian Singles Chart | 36 |
Belgian Singles Chart | 6 |
Irish Singles Chart | 1 |
Netherlands Singles Chart | 9 |
New Zealand Singles Chart | 3 |
Norwegian Singles Chart | 3 |
Swedish Singles Chart | 1 |
Swiss Singles Chart | 38 |
UK Singles Chart | 1 |
Viunga vya Nje
haririAlitanguliwa na "Holler" by Spice Girls |
UK number-one single 5 Novemba 2000 - 12 Novemba 2000 |
Akafuatiwa na "Same Old Brand New You" by a1 |
Makala 2000s pop single-related bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |