Mzamaji (ndege)

Jenasi ya ndege wa maji wanaozama
Mzamaji
Mzamaji koo-jeusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Gaviiformes (Ndege kama wazamaji)
Familia: Gaviidae (Wazamaji)
Jenasi: Gavia
Forster, 1788
Spishi: G. adamsii (Gray, 1859)

G. arctica Linnaeus, 1758
G. immer (Brünnich, 1764)
G. pacifica (Lawrence, 1858)
G. stellata (Pontoppidan, 1763)

Wazamaji (tafsiri kutoka Kiing.: diver) ni ndege wa maji wa jenasi Gavia, jenasi pekee ya familia Gaviidae. Wanafanana na vibisi na minandi lakini ni tofauti na wamepewa oda yao Gaviiformes. Wana ngozi kati ya vidole kama minandi lakini domo lao lina ncha kali bila kulabu kama vibisi. Kama zile spishi nyingine huzamia kabisa ili kukamata samaki, gegereka, amfibia, koa na luba. Hulijenga tago lao kwa matope, mimea ya maji na manyasi ardhini karibu na maji ya ziwa katika kande za kaskazini za Amerika, Ulaya na Asia. Jike huyataga mayai 1-3. Nje ya majira ya kuzaa hupatikana baharini na spishi kadhaa huhama mpaka pwani za Afrika ya Kaskazini-magharibi.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri
  Makala hii kuhusu "Mzamaji (ndege)" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili diver kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni mzamaji.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.