Mzumai
Mzumai | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mizumai ikitoa mbegu (Chrysopogon zizanioides)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Mzumai (Chrysopogon zizanioides) au mkasikasi ni spishi ya nyasi katika nusufamilia Andropogoneae. Kwa asili spishi hii inatoka Uhindi lakini siku hizi hupandwa sana katika ukanda wa tropiki. Nchi kuu za uzalishaji ni Haiti, Uhindi, Java na Reunion.
Mzumai hupandwa sana kwa kuzuia mmomonyoko kwa sababu mizizi yake inapenya ardhi hadi m 3-4. Majani yanaweza kutumika kwa kulisha wanyama na kwa kutengeneza kamba, mikeka, vikapu n.k.. Mafuta yanasindikwa kutoka mizizi ambayo hutumika katika utamaradi, sabuni ya kiayurveda, dawa za ngozi na tendwa ya harufu.
Picha
hariri-
Mizizi ya mzumai sokoni kwa Reunion
-
Mafuta ya mzumai
-
Kipepeo kilichotengenezwa kwa vitembwe vya mzumai