Nansimo
Nansimo ni kata ya Wilaya ya Bunda katika Mkoa wa Mara, Tanzania, yenye postikodi namba 31521.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 14,599 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,714 waishio humo.[2]
Wakazi wake hujishughulisha zaidi na kilimo, ufugaji na uvuvi wa samaki katika ziwa Victoria.
Ni kata ambayo imebarikiwa kuwa na vivutio mbalimbali kama vile: safu ya milima, mito na kisiwa kizuri cha Nafuba.
Pia utamaduni wa aina mbalimbali kutoka kwa makabila ya Wajita na Wakerewe umekuwa kivutio kikubwa ndani na nje ya kata hii.
Marejeo
haririKata za Wilaya ya Bunda Vijijini - Mkoa wa Mara - Tanzania | ||
---|---|---|
Butimba | Chitengule | Hunyari | Igundu | Iramba | Kasuguti | Ketare | Kibara | Kisorya | Mihingo | Mugeta | Namhula | Nampindi | Nyamihyoro| Nansimo | Neruma | Nyamang'uta | Nyamuswa | Salama |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nansimo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |