Iramba ni kata ya Wilaya ya Bunda katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31519[1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,715 waishio humo.[2]

Kata ya Iramba ina vijiji vitano ambavyo ni Isanju, Mugara, Nyarugoma, Sikiro na Mwiruruma. Makao makuu ya kata yapo Isanju.

Jamii ya watu wa Iramba ni hasa ya makabila ya Wajita, Wasukuma, Wakerewe na Wajaluo. Wakazi wa kata wanajishugulisha hasa na kilimo, uvuvi, na ufugaji.

Pia kata hii inazungukwa na maji pande kuu tatu ikiwa kama rasi iliyoingia ziwani. Kwa upande wa majini imezungukwa na visiwa kama Ilela, Nyamigongo, Nyambugu, Igali, Burwa, Bugurani na Nyamasanje.

Upande wa nchi kavu vijiji vyote vitano vinavyounda kata hiI vinaunganishwa na safu ya milima ya Iramba (iramba hill).

Kilimo: maeneo ya kilimo ndani ya kata yanafanyika katika mwambao wa ziwa Victoria na maeneo ya milimani (safu za milima ya Iramba). Wakulima wa maeneo haya hushughulika na mazao ya muhogo, viazi vitamu, uwele na mtama kama mazao ya chakula; pia pamba, mahindi na mpunga kama mazao ya biashara.

Uvuvi: vijana wengi wa Iramba wanajishughulisha na uvuvi; samaki wanaovuliwa ni sato, sangara na dagaa. Maeneo yaliyoshamiri kwa uvuvi ni Mugara, Sikiro, Isanju na Nyarugoma, pamoja na maeneo ya visiwani kama Ilela, Nyamigongo na Igari ambavyo ni vivutio vya wavuvi katika kata ya Iramba.

Ufugaji: jamii ya Iramba wanajihusisha na ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku.

Biashara: kuna wajasiriamali na vikundi mbalimbali vya wakina mama wanaojihusisha na ujasiriamali, pia wafanyabiashara wa samaki, mazao ya chakula, bidhaa mabalimbali na wafanyabiahara kutoka nje wanaoingia ndani ya kata.

Vivutio vya Iramba:

  • safu za milima ya Iramba ambayo inaunganisha vijiji vyote vya kata hii.
  • ziwa Victoria ambalo limezunguka vijiji vinne vya kata hii na kufanya Iramba kuwa kama rasi iliyoingia majini.
  • visiwa vinne vinavyozunguka kata hii ambavyo ni Igari, Ilela, Nyambugu na Nyamigongo.
  • kivuko cha MV MARA ambacho huunganisha Iramba na Majita (wilaya ya Bunda na wilaya ya Musoma Vijijini)
  • daraja kubwa ambalo halikujengwa na binadamu: hili hujulikana kama daraja la Mungu ambalo hutenganisha Mugara na Sikiro (Nyabhikombwe)

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Bunda Vijijini - Mkoa wa Mara - Tanzania  

Butimba | Chitengule | Hunyari | Igundu | Iramba | Kasuguti | Ketare | Kibara | Kisorya | Mihingo | Mugeta | Namhula | Nampindi | Nyamihyoro| Nansimo | Neruma | Nyamang'uta | Nyamuswa Salama


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iramba (Bunda) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.