Nape Moses Nnauye ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM. Alihudumia kama katibu wa itikadi wa CCM. Amechaguliwa kuwa mbunge wa Mtama kwa miaka 2015 hadi sasa. [1]

Aliteuliwa na rais Magufuli kuwa waziri wa habari, utamaduni na michezo. Mwaka 2017 aliondolewa uwaziri baada ya kuagiza uchunguzi wa tendo la Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliyewahi kuvamia ofisi za kituo cha habari cha binafsi cha Clouds[2][3]. Alipojaribu kujieleza mbele ya wanahabari alizuiwa na maafisa wa usalama waliotoa bastola na kumwamuru asiseme kitu.[4][5]

Baada ya kutokea kwa taarifa kuwa alishiriki katika majidiliano ya kumkosoa rais, kwenye mwaka 2019 alikutana na rais Magufuli akaomba kusamehewa akapata kibali cha rais[6].

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 alirudi bungeni. Kwenye Januari 2022 ameteuliwa na rais mpya Samia Suluhu Hassan kuwa waziri wa Wizara ya Habari na Teknolojia ya Habari.[7]

Marejeo

hariri
  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017
  2. https://theinsider.ug/index.php/2017/03/20/tanzania-government-officials-raid-a-tv-station/ Ilihifadhiwa 15 Januari 2022 kwenye Wayback Machine. Tanzania government officials raid a TV-station, tovuti ya theinsider.ug, 20.03.2017
  3. https://www.bbc.com/swahili/habari-39416652 Nnauye: Waziri aliyefutwa asema bado anaunga mkono juhudi za Magufuli ; Tovuti ya BBC 28 Machi 2017
  4. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/nape-s-parting-shot-reveals-deep-divisions-within-govt-2584142 Ilihifadhiwa 15 Januari 2022 kwenye Wayback Machine. Nape’s parting shot reveals deep divisions within govt; Citizen 24.03.2017
  5. https://www.rfi.fr/en/africa/20170324-tanzania-sacked-information-minister-held-gunpoint-has-no-regrets-about-being-fired Tanzania: Sacked information minister, held at gunpoint has 'no regrets' about being fired, Tovuti ya rfi.fr 24/03/2017;
  6. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/news/president-magufuli-s-hand-of-forgiveness-sets-social-media-abuzz-2691590 Ilihifadhiwa 15 Januari 2022 kwenye Wayback Machine. President Magufuli’s hand of forgiveness sets social media abuzz; Citizen 11.09.2019
  7. https://www.bbc.com/swahili/habari-59920241 Rais Samia afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kubuni wizara mpya, Tovuti ya BBC 8 Januari 2022