Ukukwi
(Elekezwa kutoka Naranyasi)
Ukukwi | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Naranyasi au ukukwi mabaka (Philothamnus semivariegatus)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 20:
|
Kukwi ni spishi za nyoka kijani wa jenasi Philothamnus katika familia Colubridae wasio na sumu. Spishi nyingine huitwa isale, namalanga, naranyasi, ngowe au nyokameni.
Kwa kawaida urefu wa nyoka hawa ni chini ya m 1, mara nyingi sm 50-100 na hadi 130 kwa kipeo. Rangi yao ni kijani pengine pamoja na rangi nyingine kame kijivu, buluu, nyekundu na njano. Spishi kadhaa zina madoa. Nyokameni ni mwekundu au kahawianyekundu.
Nyoka hawa wanatokea karibu na maji mara nyingi kwa sababu takriban spishi zote hula vyura na ndubwi zao. Lakini hupita masaa mengi mitini ambapo huwinda mijusi na vyura-miti.
Kukwi hawana sumu lakini wanaweza kung'ata na wakifanya hii husogea kichwa huku na huku ili kusababisha mikwaruzo mibaya.
Spishi
hariri- Philothamnus angolensis Ukukwi wa Angola (Angolan green snake)
- Philothamnus battersbyi Isale, Sale au Ukukwi wa Battersby (Battersby's green snake)
- Philothamnus bequaerti Ukukwi wa Uganda (Uganda green snake)
- Philothamnus carinatus Ukukwi Magamba-kuminatatu (Thirteen-scaled green snake)
- Philothamnus dorsalis Ukukwi Milia (Striped green snake)
- Philothamnus girardi Ukukwi wa Annobon (Annobon wood snake)
- Philothamnus heterodermus Ukukwi-misitu (Forest green snake)
- Philothamnus heterolepidotus Ukukwi Mwembamba (Slender green snake)
- Philothamnus hoplogaster Namalanga au Ukukwi Kusi (Southeastern green snake)
- Philothamnus hughesi Ukukwi wa Hughes (Hughes's green snake)
- Philothamnus irregularis Ukukwi Kaskazi (Northern green bush snake)
- Philothamnus macrops Nyokameni au Ukukwi wa Usambara (Usambara green snake)
- Philothamnus natalensis Ukukwi wa Natal (Natal green snake)
- Philothamnus nitidus Ukukwi wa Loveridge (Loveridge's green snake)
- Philothamnus ornatus Ukukwi Mgongo-mlia (Stripe-backed green snake)
- Philothamnus pobeguini Ukukwi wa Gini (Guinean green snake)
- Philothamnus punctatus Ngowe au Ukukwi Madoadoa (Speckled green snake)
- Philothamnus ruandae Ukukwi wa Rwanda (Rwanda forest green snake)
- Philothamnus semivariegatus Naranyasi au Ukukwi Mabaka (Spotted bush snake)
- Philothamnus thomensis Ukukwi wa Sao Tome (São Tomé wood snake)
Picha
hariri-
Isale
-
Ukukwi wa Natal
-
Ukukwi wa Sao Tome
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ukukwi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |