Puju
(Elekezwa kutoka Naso)
Puju | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Puju madoadoa (Naso brevirostris)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Puju au puju pembe ni samaki wa baharini wa jenasi Naso katika familia Acanthuridae wa oda Perciformes. Kama ndugu wao kangaja wana jozi za miiba kwa umbo la vijembe kwenye kila upande wa msingi wa mkia. Lakini rangi zao si kali kama zile za kangaja. Spishi fulani huitwa karanzaga au sange pia.
Maelezo
haririSpishi kadhaa za puju zina kivimbe kirefu kwenye paji. Kwa wengine hufanana na kangaja lakini huwa ni wakubwa zaidi. Puju mkia-ncha-nyeupe anaweza kufika urefu wa m moja. Wana jozi moja, mbili au tatu za vijembe. Hula miani kwenye miamba ya matumbawe.
Uvuvi
haririPuju hupendwa na wavuvi kwa mkuki na kwa kawaida hubanikwa wazima.
Spishi za Afrika
hariri- Naso annulatus, Puju Mkia-ncha-nyeupe (Whitemargin unicornfish)
- Naso brachycentron, Puju Kibyongo (Humpback unicornfish)
- Naso brevirostris, Puju Madoadoa (Spotted unicornfish)
- Naso elegans, Puju Maridadi (Elegant unicornfish)
- Naso fageni, Puju Uso-farasi (Horseface unicornfish)
- Naso hexacanthus, Puju Ulimi-mweusi au Karanzaga (Sleek unicornfish)
- Naso mcdadei, Puju Pua-mraba (Squarenose unicornfish)
- Naso minor, Puju Mdogo (Blackspine unicornfish)
- Naso thynnoides, Puju Vijembe-viwili (Oneknife unicornfish)
- Naso tonganus, Puju Pua-tunguu (Bulbnose unicornfish)
- Naso unicornis, Puju Mgongo-buluu au Sange (Bluespine unicornfish)
- Naso vlamingii, Puju Pua-kubwa (Bignose unicornfish)
Spishi za mabara mengine
hariri- Naso caeruleacauda (Bluetail unicornfish)
- Naso caesius (Grey unicornfish)
- Naso lituratus (Orangespine unicornfish)
- Naso lopezi (Elongated unicornfish)
- Naso maculatus (Spotted unicornfish)
- Naso reticulatus (Reticulated unicornfish)
- Naso tergus (Taiwan unicornfish)
- Naso tuberosus (Humpnose unicornfish)
Picha
hariri-
Puju mkia-ncha-nyeupe
-
Puju kibyongo
-
Puju maridadi
-
Puju ulimi-mweusi
-
Puju vijembe-viwili
-
Puju pua-tunguu
-
Puju mgongo-buluu
-
Puju pua-kubwa
-
Grey unicornfish
-
Orangespine unicornfish
-
Elongated unicornfish
-
Reticulated unicornfish
-
Humpnose unicornfish
Marejeo
hariri- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Puju kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |