Nchi ya kimabara
Nchi ya kimabara ni nchi yenye eneo kwenye bara mbili au zaidi.
Mifano yake ni:
- Uturuki (Ulaya na Asia)
- Urusi (Ulaya na Asia)
- Misri (Afrika na Asia)
- Yemeni (Asia na visiwa upande wa Afrika)
Nchi kadhaa yana maeneo ya ng'ambo kama urithi wa uenezi wa kikoloni, hasa kama wakazi wa maeneo yasiyopewa uhuru wamezoea au kukubali kabisa kuendelea kama raia wa nchi iliyokuwa mkoloni zamani.
Mifano yake ni:
- Ufaransa (Ulaya) yenye maeneo katika Amerika ya Kaskazini (Saint Pierre na Miquelon), Amerika ya Kusini (Guyana ya Kifaransa), Afrika (visiwa vya Mayotte na Réunion) na Pasifiki (Polynesia ya Kifaransa ).
- Uingereza (maeneo kwenye mabara yote kwa mfano Gibraltar katika Ulaya, Saint Helena katika Afrika, Visiwa vya Virgin vya Uingereza katika Amerika, Diego Garcia katika Asia)
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|