Guyana ya Kifaransa

département ya Ufaransa
Région Guyane
Flag of France.svg Nembo
Jina la Kifaransa Région Guyane
Jina la kawaida Guyana ya Kifaransa
Mji Mkuu Cayenne
Eneo 83,534 km²
Mkuu wa Mkoa Rodolphe Alexandre
Idadi ya wakazi 250,109
Sensa ya mwaka 2013
Wakazi kwa km² 3
Wilaya (arrondissements) 2
Ramani Reunion na Ufaransa bara French Guiana in its region.svg
-- Kwa nchi jirani ya Guyana angalia makala Guyana--

Guyana ya Kifaransa (kwa Kifaransa: Guyane française au Guyane pekee) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa ("département d'outre-mer" au DOM) katika Amerika Kusini.

Imepakana na Brazil na Surinam.

Pwani ya Bahari ya Karibi (Atlantiki) iko upande wa kaskazini.

Ilikuwa koloni la Ufaransa; sasa imekuwa sehemu kamili ya Ufaransa kisiasa na kisheria. Wakazi ni raia wa Ufaransa. Eneo lina hali ya mkoa (departement) na pia kanda (region) katika Ufaransa. Hivyo Guyane ni sehemu ya Umoja wa Ulaya. Pesa yake ni Euro.

Makao makuu ya Guyane ni mji wa Cayenne.

WatuEdit

Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa 250,109 katika mwaka 2013.

Wakazi walio wengi ni wa asili ya Afrika au wa mchanganyiko wa Kiafrika-Kizungu (60-70%). Asilimia 14 ni Wazungu; wengine ni Waindio asilia (3-4%), Wachina (3-4%), Wahindi na wahamiaji wa hivi karibuni kutoka Laos (1-2%).

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kifaransa.

Upande wa dini, wakazi walio wengi ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyana ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

  Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guyana ya Kifaransa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.