Mayotte

département ya Ufaransa
Mayotte
Kisiwa cha Mahore
Flag of France Coat of Arms of Mayotte
(Bendera ya Mayotte) (Coat of Arms of Mayotte)
La Marseillaise | ni wimbo wa taifa wa Ufaransa
Mahali pa Mayotte
Lugha za Taifa Kiswahili (shimaore)
Kifaransa
Mji Mkuu Mamoudzou
Rais
Rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron
Eneo
 - Jumla
 - 0.4% Maji
Kadiriwa 185 duniani
374 km²
Umma
 - Kadirio 2019 (270,372)
 - Sensa, julai 2002 (160,265)
 - Umma kugawa na Eneo (kilomita) 720
Kadiriwa 187 duniani
; (11 duni)
Chumo cha uchumi
 - Jumla
 - kwa kipimo cha umma
$466.8 billion (208 kadir)
$2,600 (165)
Uhuru
 - Kadirifu
 - Barabara
Eneo la Ufaransa
Kura ya maoni kubaki eneo la Ufaransa
Fedha Euro
Saa za Eneo UTC +3
Wimbo wa Taifa La Marseillaise
Intaneti TLD .yt
kodi za simu 269

Mayotte ni eneo la ng’ambo la Ufaransa (kwa Kifaransa: Départment de Mayotte). Linaundwa na visiwa vya Mahore na Pamanzi pamoja na vingine vidogo. Eneo hili kijiografia ni hasa muungo wa funguvisiwa la Komoro lakini si kisiasa.

Ramani ya Komoro na Mayotte.

Mayotte iko katika kaskazini ya Mfereji wa Msumbiji kwenye Bahari Hindi, kati ya Madagaska upande wa mashariki-kusini na Msumbiji bara upande wa magharibi. Iko kilometa 295 magharibi kwa Madagaska na km 67 kusini mashariki mwa Anjouan.

Ardhi ya Mayotte ina eneo la takriban km² 374. Ni mwamba wa matumbawe.

Mji mkuu ni Mamoudzou tangu mwaka 1977. Mji mkuu wa zamani ni Dzaoudzi kwenye kisiwa cha Pamanzi.


Historia hariri

 
Andriantsoly, Sultani wa mwisho wa Mayotte, 1832-1843.

Mayotte inaonekana kuwa imekaliwa na watu kutoka karne ya 7, wakitokea Madagaska, wengine wenye asili ya Asia na wengine wenye asili ya Afrika.

Kati ya karne ya 8 na karne ya 11 wakazi walisilimu, na kuna msikiti mkongwe (katika Tsingoni) wa karne ya 14, pamoja na mirhab ya matumbawe (1532). Visiwa vyote vya Komoro vinafuata utamaduni wa Kiswahili vikiwa pamoja na Mayotte.

Mwaka wa 1841, wakati idadi ya watu ilipungua kwa wakazi chini ya 3000, sultani wa mwisho Andriansoly (kutoka Madagaska) aliuza kisiwa kwa Ufaransa kwa kubadilishana ya ulinzi wa nchi hiyo, hivyo Mayotte ikawa koloni la Kifaransa.

Mwaka 1974, wakati visiwa vingine vitatu vya Komoro walidai uhuru na kuunda Umoja wa Comoro, Mayotte iliomba kubaki na Ufaransa, na mwaka 2011 ilipewa hali ya eneo la ng'ambo la Ufaransa kwa kura ya maoni.

Lugha na dini hariri

Kuna lugha tatu ambazo huzungumzwa kisiwani Mayotte, yaani Kifaransa (lugha rasmi), Kimaore ya Komori (55.1%), na Kibushi ya Madagaska.

Upande wa dini, asilimia 97 ni Waislamu na 3% ni Wakristo.

Utalii hariri

Kisiwa cha Mayotte kina mchanga wa pwani ya rangi tofauti (nyeusi, kahawia, kijivu, nyekundu, beige, nyeupe). Rasi yake ni kubwa (km² 1500).

Usafiri hariri

 
Bahari karibu na Mamoudzou.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri


Nchi za Afrika  
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira