Nchi za Kibalti (pia: nchi za Baltiki) ni jina la kujumlisha nchi tatu upande wa mashariki wa Bahari Baltiki ambazo ni

  1. Estonia
  2. Latvia
  3. Lituanya.
Nchi za Kibalti
Ramani ya Bahari ya Baltiki

Zote tatu zilikuwa na historia ambako utawala juu yao ulipiganiwa kati ya Ujerumani, Poland, Uswidi na Urusi.

Tangu karne ya 18 zote tatu zilikuwa sehemu ya milki ya Urusi. Baada ya mapinduzi ya Urusi ya 1917 na mkataba wa Versailles zote tatu zilipata uhuru wao lakini zilivamiwa tena na Urusi wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia na kuwa jamhuri ndani ya Umoja wa Kisovyeti.

Baada ya kuporomoka kwa Umoja wa Kisoveti mwaka 1990 / 1991 zikapata uhuru wao.

Tangu 2004 zote tatu ni ni wanachama wa Umoja wa Ulaya.

Siku hizi pia Mkoa wa Kaliningrad wa Urusi (hadi 1945 Prussia ya Mashariki) huhesabiwa kuwa sehemu ya nchi za Kibalti.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nchi za Kibalti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.