Ufunda
(Elekezwa kutoka Nectamia)
Ufunda | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kundi la ufunda tumbo-njano (Ostorhinchus apogonoides)
| ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 37 na spishi 362, 50 katika Afrika ya Mashariki:
|
Funda, dagaa-donzi au dagaa ya gege ni samaki wadogo kiasi wa baharini wa familia Apogonidae katika oda Perciformes lakini spishi kadhaa zinaishi katika maji baridi, zile za jenasi Glossamia hasa.
Maelezo
haririKwa kawaida funda ni samaki wadogo. Spishi nyingi huwa chini ya sm 10 na mara nyingi huwa rangi kali. Wanajulikana kwa mdomo wao mkubwa na kwa mgawanyiko wa pezimgongo katika mapezi mawili tofauti. Spishi nyingi huishi katika maji ya tropiki au nusutropiki, ambapo hukaa katika miamba ya matumbawe na nyangwa. Hawa ni samaki wa usiku na wanashinda mchana katika mianya ya giza ndani ya mwamba. Angalau baadhi ya spishi huatamia mayai yao ndani ya mdomo wa madume.
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri- Apogon campbelli, Ufunda wa Campbell (Campbell's cardinal)
- Apogon coccineus, Ufunda Mwekundu (Ruby cardinalfish)
- Apogon nitidus, Ufunda Madoa-buluu (Bluespot cardinalfish)
- Apogon semiornatus, Ufunda Milia-hanamu (Oblique-banded cardinalfish)
- Apogonichthyoides nigiripinnis, Ufunda Mapezi-meusi (Bullseye)
- Apogonichthyoides taeniatus, Ufunda Milia-miwili (Twobelt cardinal)
- Apogonichthyoides timorensis, Ufunda wa Timor (Timor cardinalfish)
- Apogonichthys ocellatus, Ufunda Madoa-macho (Ocellated cardinalfish)
- Apogonichthys perdix, Ufunda Sikipi (Perdix cardinalfish)
- Archamia bleekeri, Ufunda wa Gon (Gon's cardinalfish)
- Cheilodipterus arabicus, Ufunda Chui (Tiger cardinalfish)
- Cheilodipterus artus, Ufunda Mbweha (Wolf cardinalfish)
- Cheilodipterus macrodon, Ufunda Meno-makubwa (Large-toothed cardinalfish)
- Cheilodipterus quinquelineatus, Ufunda Milia-mitano (Five-lined cardinalfish)
- Fibramia amboinensis, Ufunda wa Amboina (Amboina cardinalfish)
- Fibramia lateralis, Ufunda Kibyongo (Humpback cardinalfish)
- Fibramia thermalis, Ufunda Milia-nusu (Half-barred cardinalfish)
- Foa fo, Ufunda Foa (Weedy cardinalfish)
- Fowleria aurita, Ufunda Macho-baka (Cross-eyed cardinalfish)
- Fowleria variegata, Ufunda Rangirangi (Variegated cardinalfish)
- Gymnapogon africanus, Ufunda Fuwele (Crystal cardinalfish)
- Lepidamia natalensis, Ufunda wa Natal (Natal cardinalfish)
- Neamia octospina, Ufunda Miiba-minane (Eightspine cardinalfish)
- Nectamia fusca, Ufunda Moshi (Ghost cardinalfish)
- Ostorhinchus angustatus, Ufunda Milia-mipana (Broad-striped cardinalfish)
- Ostorhinchus apogonoides, Ufunda Tumbo-njano (Short-tooth cardinalfish)
- Ostorhinchus aureus, Ufunda Dhahabu (Ring-tailed cardinalfish)
- Ostorhinchus bryx, Ufunda Mlia-mmoja (Offshore cardinalfish)
- Ostorhinchus cookii, Ufunda wa Cook (Cook's cardinalfish)
- Ostorhinchus cyanosoma, Ufunda Milia-machungwa (Yellow-striped cardinalfish)
- Ostorhinchus fasciatus, Ufunda Milia-miwili (Broad-banded cardinalfish)
- Ostorhinchus flagelliferus, Ufunda Mjeledi (Coachwhip cardinalfish)
- Ostorhinchus fleurieu, Ufunda Ua (Flower cardinalfish)
- Ostorhinchus gularis, Ufunda Mchanga (Gular cardinalfish)
- Ostorhinchus nigripes, Ufunda Miguu-myeusi (Blackfoot cardinalfish)
- Ostorhinchus spilurus, Ufunda Somali (Somali cardinalfish)
- Pristiapogon fraenatus, Ufunda Hatamu (Bridled cardinalfish)
- Pristiapogon kallopterus, Ufunda Kimeto (Iridescent cardinalfish)
- Pseudamia gelatinosa, Ufunda Bokoboko (Gelatinous cardinalfish)
- Pseudamiops pellucidus, Ufunda Mwangavu (Limpid cardinalfish)
- Rhabdamia gracilis, Ufunda Mwembamba (Luminous cardinalfish)
- Siphamia mossambica, Ufunda Chani (Sea urchin cardinalfish)
- Siphamia tubifer, Ufunda Mirija (Tubifer cardinalfish)
- Sphaeramia orbicularis, Ufunda Mviringo (Orbiculate cardinalfish)
- Taeniamia flavofasciata, Ufunda Milia-njano (Yellow-lined cardinalfish)
- Taeniamia fucata, Ufunda Milia-myekundu (Orange-lined cardinalfish)
- Taeniamia mozambiquensis, Ufunda wa Msumbiji (Mozambique cardinalfish)
- Verulux cypselurus, Ufunda Mkia-mbayuwayu (Swallowtail cardinalfish)
- Zoramia fragilis, Ufunda Dhaifu (Fragile cardinalfish)
Picha
hariri-
Ufunda mwekundu
-
Ufunda milia-hanamu
-
Ufunda wa Timor
-
Ufunda madoa-macho
-
Ufunda wa Gon
-
Ufunda mbweha
-
Ufunda meno-makubwa
-
Ufunda milia-mitano
-
Ufunda macho-baka
-
Ufunda rangirangi
-
Ufunda moshi
-
Ufunda milia-mipana
-
Ufunda dhahabu
-
Ufunda wa Cook
-
Ufunda milia-machungwa
-
Ufunda milia-miwili
-
Ufunda ua
-
Ufunda hamatu
-
Ufunda kimeto
-
Ufunda mwembamba
-
Ufunda mviringo
-
Ufunda milia-njano
-
Ufunda milia-myekundu
-
Ufunda dhaifu
Marejeo
hariri- Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
- Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Viungo vya nje
hariri- Ufunda kwenye hifadhidata ya samaki Ilihifadhiwa 28 Juni 2020 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ufunda kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |