Neema Mduma (alizaliwa mkoani Morogoro, 21 Oktoba 1989 (1989-10-21) (umri 35) ni mwanazuoni, daktari aliyebobea kwenye taaluma ya sayansi na teknolojia. Ni mmoja kati ya Watanzania waliowahi pata Udaktari wa Filosofia (PhD) katika umri mdogo na kati ya watu wenye kuwatia ari mabinti wengine katika masuala ya elimu, hususani masomo yenye kuhusisha sayansi na hesabu.

Neema Mduma
Amezaliwa 21 Oktoba 1989 (1989-10-21) (umri 35)
Morogoro
Nchi Tanzania
Kazi yake Mhadhiri Mwandamizi
Mwajiri Nelson Mandela African Institution of Science and Technology
Elimu Shahada ya Uzamivu (PhD)
Dini Mkristo
Dhehebu Mlutheri
Ndoa Ameolewa
Mwenza Hudson Laizer
Wazazi Baba: Mathias Mduma

Mama: Judith Tesha

Tovuti https://nm-aist.ac.tz

Neema, ambaye kwa kabila ni Mpare, baba yake ni mchungaji wa kanisa anayefahamika kwa jina la Mathias Mduma na mama yake ni mwalimu anayefahamika kwa jina la Judith Tesha.

Alisoma awali katika shule ya msingi Bungo iliyopo mjini Morogoro kuanzia mwaka 1996 mpaka mwaka 2002. Kuhitimu kwake darasa la saba kukampa nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari Kilakala Sekondari ambayo ni shule ya vipaji maalumu kwa wasichana. Hivyo alianza kidato cha kwanza mwaka 2003 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2006 na kuendelea na kidato cha tano mwaka 2007 na kuhitimu kidato cha sita mwaka 2009 hapo hapo Kilakala.

Mwaka 2009 alipata nafasi ya kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini) na kuanza masomo ya shahada ya kwanza na alisomea shahada ya Sayansi ya Habari na Mawasiliano. Mara baada ya kumaliza shahada hiyo alijiunga na taasisi ya NM-AIST na kuendelea na shahada ya sayansi ya uzamili (MSc) na baadae shahada ya uzamivu (PhD) kwenye mambo ya sayansi na teknolojia ya mawasiliano akibobea katika masuala ya Akili Mnembe (Artificial Intelligence).

Neema zaidi ya kuwa na mapenzi na elimu, ni mtafiti mzuri na amekuwa akishirikiana na watafiti wenzake katika kutafuta namna mbali mbali za kuweza tatua changamoto za kijamii. Mfano wakati wa mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19, Neema alishirikiana na wenzake kutoka Kenya na Uganda na kuweza fanikiwa pata fedha ya kuwawezesha kufanya utafiti katika kada za kilimo, elimu na afya.[1]

Mara baada ya kumaliza masomo, Neema aliajiriwa kama Mkufunzi msaidizi katika Chuo Kikuu cha Iringa kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2017 kisha akajiunga na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela ambapo alifanikiwa kuajiriwa na kuwa Mhadhiri msaidizi na baadae kama Mhadhiri, na tarehe 23 mwezi wa pili mwaka 2024 Neema alipandishwa daraja kutoka Mhadhiri na kuwa Mhadhiri mwandamizi baada ya kukidhi vigezo vya kufundisha, kufanya tafiti na kutoa machapisho ya kisayansi.

Shughuli za kijamii

hariri

Neema akiwa anamalizia masomo yake ya uzamivu (PhD), aliamua kufanya utafiti na kujikita katika kutafuta suluhisho la kudumu ili kuweza tatua tatizo la utoro mashuleni wenye kupelekea wanafunzi kufeli katika masomo yao au kuacha shule kabisa. Hivyo alitengeneza mfumo ulio itwa Baki shule. Mfumo huu unatumia akili mnembe katika kutambua viashiria vya utoro ulio kithiri ama dalili za utoro kwa mwanafunzi au wanafunzi na kuweza wasaidia wazazi na walimu kutambua mapema kabla tatizo halija kithiri na kuathiri ufaulu wa mtoto darasani.[1]

Ili kuweza saidia jamii ya Kitanzania, Neema hutumia muda wake wa ziada kukutana na mabinti mashuleni na kuweza zungumza nao kuhusu masomo ya Sayansi na Hesabu huku akitoa mafunzo ya kuandika mistari ya Codes zenye kufanya Kompyuta kutenda jambo fulani. Elimu hii huwasaidia mabinti kuweza penda masomo ya Sayansi na Hesabu hivyo kuweza timiza ndoto zao za kuwa Wanasayansi kama Neema au kwenda mbali zaidi. [2]

Miradi endelevu

hariri
  1. Mradi wa kutumia takwimu katika kupambanua changamoto za magonjwa kwenye mazao. Mradi unao dhaminiwa na IDRC na SIDA kupitia LACUNA Fund in Agriculture (2023)[3]
  2. Mradi wa kujifunza kwa kina mbinu za kugundua mapema magonjwa katika mazao. Mradi huu unafadhiriwa na IDRC na SIDA kupitia Kituo cha mafunzo ya Teknolojia cha Africa (ACTS)[4]

Mijadala na Mihadhara

hariri

Matumizi ya "Machines Learning" kwenye Elimu, Kilimo na Afya [5]

Tuzo na Teuzi Mbalimbali

hariri
  1. 100 Tanzanian Changemakers Iliyo tolewa na Serengeti Bytes, 2023
  2. Appointed Member of the Committee for Preparing Tanzania Development Vision 2050, 2023
  3. Appointed Member of the Committee for Preparing the Concept on Supporting the Establishment of the Africa Centres of Excellence (ACEs) in Tanzania, 2023
  4. Distinguished Staff awarded by the school of CoCSE at the Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, 2023
  5. Best Worker for Academic Staff at the Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, 2022
  6. WIMA STEM iliyo tolewa na Women in Management Africa (WIMA), 2021
  7. Excellence in Science and Technology Leadership iliyo tolewa na Coca-Cola Kwanza Ltd, 2021
  8. International Women’s Day Recognition iliyo tolewa na Puma Energy Tanzania, 2021
  9. L’Oréal-UNESCO for Women in Science, 20 Young Talents in Sub-Saharan Africa, 2020
  10. Women in Science iliyo tolewa na Next Einstein Forum, 2019
  11. Tanzania Sheroes Iliyo tolewa na taasisi ya The Launchpad na Ubalozi wa Sweden, 2019
  12. Queen Elizabeth Scholar Iliyo tolewa na the Carleton University Mjini Ottawa Nchini Canada, 2019
  13. Deep Learning Indaba conference, MIT Press Book award iliyo tolewa Nairobi, Kenya, 2019
  14. The 4th Business Plan Competition, First winning team in Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, 2016
  15. Nelson Mandela Week Exhibitions, Third winner award in Nelson Mandela African Institution of Science and Technology, 2015

Viungo vya Nje

hariri
  1. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/woman/neema-academic-who-inspires-girls-to-break-the-glass-ceiling-3709182
  2. https://african.business/2021/02/technology-information/young-african-women-in-stem-neema-mduma-machine-learning
  3. https://africa.businessinsider.com/local/lifestyle/dollar63000-granted-to-the-amazing-tanzanian-woman-using-machine-learning-for/z56lkxd
  4. https://www.youtube.com/watch?v=k9fKzhIf3Fk
  5. https://mzalendo.co.tz/2023/03/30/tumieni-tehama-kutatua-changamoto/
  6. https://fullshangweblog.co.tz/2023/03/30/tumieni-tehama-kutatua-changamoto/
  7. https://www.sayarinews.co.tz/2023/03/tumieni-tehama-kutatua-changamoto.html
  8. https://www.dulenews.com/2023/03/tumieni-tehama-kutatua-changamoto.html?m=1
  9. https://www.youtube.com/watch?v=kVOPgxT-dD4
  10. https://www.growfurther.org/teaching-smartphones-how-to-predict-plant-disease/?utm_source=Grow+Further&utm_campaign=1323c48795-EMAIL_CAMPAIGN_2023_02_21_10_15&utm_medium=email&utm_term=0_-1323c48795-%5BLIST_EMAIL_ID%5D
  11. https://www.growfurther.org/now-comes-the-hard-part/
  12. https://owsd.net/news/news-events/owsd-early-career-fellows-announced
  13. https://www.youtube.com/watch?v=DljSd-mbSGY
  14. https://en.unesco.org/news/unesco-and-foundation-loreal-recognize-20-young-women-scientists-sub-saharan-africa
  15. https://www.france24.com/fr/vidéo/20211208-tanzanie-une-application-pour-prévenir-le-décrochage-scolaire
  16. https://www.africanews.com/2020/11/26/empowering-african-women-in-science-business-africa/
  17. https://theexchange.africa/countries/tanzania/meet-tanzanias-youngest-phd-holder-winner-of-youngest-women-scientist-awards/?amp=1
  18. https://newafricanmagazine.com/25116/
  19. https://african.business/2021/02/technology-information/young-african-women-in-stem-neema-mduma-machine-learning/
  20. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/woman/women-in-leadership-and-the-next-level-of-success-4107130
  1. 1.0 1.1 https://newafricanmagazine.com/25116/
  2. https://www.thecitizen.co.tz/tanzania/magazines/woman/neema-academic-who-inspires-girls-to-break-the-glass-ceiling-3709182#google_vignette
  3. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC10121386/
  4. Super User. "Detecting Crop Diseases Using Mobile Application". www.acts-net.org (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-03-09. {{cite web}}: |author= has generic name (help)
  5. https://globalyoungacademy.net/nmduma/