Wapare
Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa nchi ya Tanzania.
Wanakadiriwa kuwa 1,000,000 hivi.
Makao
Wapare wanatokea katika wilaya za Same na Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, lakini pia wapo katika wilaya ya Moshi sehemu za Chekereni, Himo, Mabungo, Uchira, Moshi mjini, na pia katika wilaya ya Hai sehemu za Rundugai na mto Weruweru. Wapare pia wanaishi katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, sehemu za Bumbuli na Mavumo.
Lakini kutokana na mahusiano yaliyopanuka nchini Tanzania, Afrika na dunia kwa jumla, kutokana na suala la utandawazi Wapare wametapakaa kote Tanzania kwa shughuli mbalimbali, kwa mfano jamii kubwa ya Wapare waliohamia mkoa wa Morogoro na kujenga makazi, na hali imekuwa hivyo katika mikoa yote nchini na kwingineko.
Maeneo ya Wapare yamekuwa na mvuto wake mfano katika milima ya Upareni kwenye maeneo kama Chome na Kwizu kuna mandhari ya kijani kibichi ambayo inavutia japo shughuli za binadamu za kila siku zimekuwa zikiharibu mazingira ya Upareni kadhalika. Kuna maeneo yanayovutia kama milimani (Usangi, Ugweno, misitu ya Shengena n.k.) Pia skimu ya umwagiliaji iliyopo Ndungu inasaidia katika shughuli za kilimo kama kilimo cha mpunga. Pia kuna mwamba wa kuvutia Same unaofanana na pua ya binadamu maarufu kama ikamba la fua. mji mkuu katika kabila la upare ni maore ulioko wilaya ya same ma chief wake alikuwa mfumwa boaz mashambo
Mito ya Upare
Kuna mto Yongoma, Hingilili, Mhoke vuta, Nakombo, Rika, Mweta nano hii mito yote iko Pare ya kusini. Katika mto Hingilili kuna maporomoko makubwa na yanayosadikiwa kuwa marefu kuliko yale ya Victoria Falls, haya yanajulikana kama Ndurumo yapo eneo la Gonja Bombo umbali wmfupi kutoka mtaa wa Mang'ang'a katika eneo linaloitwa Mbula.
Maziwa na mabwawa
Kuna ziwa Jipe, bwawa la Nyumba ya Mungu na Kalemawe n.k.
Maeneo mazuri ya kutembelea
- Mbuga ya Mkomazi
- Bwawa la Nyumba ya Mungu
- Msitu wa asili wa Shengena
- Bwawa la Kalimawe
- Maporomoko ya Ndurumo - Gonja Bombo
- Msitu wa Ngagheni Mpinji- Vudee uliokuwa wa matambiko karne ya 17 mpaka 19
- Mlima wa Masheko Ndolwa-Vudee uliokuwa na Matambiko ya Wapare
- Jabali la Mhewe -Vudee lililopasuliwa na wananchi wa Vudee kuwezesha barabara kupita miaka ya 1960 na 1961.
- Msitu wa Wambugu ulioko karibu na Dangaseta- Mwembe uliotumika kwa matambiko ya kabila linaloishi Lushoto Tanga-hadi leo wachache wao bado hufika kutambika pale.
- Msitu na chanzo cha maji ya kwachegho sehemu ambayo ni ya ajabu maana ndio sehem pekee ambayo maji yanaonekana kutiririka kuelekea sehemu ya muinuko
- Mlima Kindoroko
Asili
Wapare wanasemekana wametoka katika nchi ya Kenya sehemu za Taita, Taveta na Ukamba.
Wapare pia wana ukaribu na makabila ya Mkoa wa Tanga hasa Wasambaa, Wazigua na Wanguu. Ukaribu wao uko katika lugha ambapo maneno mengi ya makabila haya yanafanana. Vile vile majina ya baadhi ya maeneo yaliyopo kwa Wapare yapo pia kwenye maeneo wanamoishi makabila hayo. Kwa mfano, kwa Wapare kuna majina ya maeneo kama vile Gonja, Ndeme, Ndolwa n.k. Majina haya yapo pia maeneo ya Wanguu na Wasambaa. Hii inaonesha kwamba makabila haya yana asili moja.
Kuna watu wanadai kwamba Wapare asili yao ni Uchagani. Eti Wapare kwa Kichagga maana yake ni "wapige". Hii si kweli kabisa. Isipokuwa watu wa makabila haya wote walitokea Kenya. Wachagga walitangulia wakawahi kuishi maeneo yenye rutuba hasa kuzunguka mlima Kilimanjaro. Wapare walikuja baadaye na walipotaka kuishi na Wachagga ndipo vita vikatokea kati ya Wapare na Wachagga. Ili kuepusha umwagaji damu zaidi Wapare walisogea kusini zaidi kuelekea mkoa wa Tanga. Wapare wenyewe kwa asili hujiita Vaasu ikiwa na maana ya "vareasa" au "watu wanaotumia pinde na mishale".ikiwemo ya sumu
Tabia
Wapare ni miongoni mwa makabila ambayo watu wake wamesoma sana na wana ushawishi mkubwa katika nyanja za siasa na uchumi wa Tanzania.
Wapare pia ni kabila la watu wanaopenda haki (yaani hawapendi kuonewa wala kumuonea mtu). Ndiyo maana watu wengine wanadhani wanapenda kesi, bali kesi ni njia mojawapo ya kuhakikisha haki inatendeka katika jamii. Utawasikia watu wengine wakidai kuwa Mpare yupo tayari kuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Dhuluma kwa Wapare ni kitu kilichokuwa kimepigwa marufuku hata kwenye matambiko yao, japo siku hizi kuna uwezekano baadhi yao wakawa hawana sifa hii tena.
Uchumi
Wapare walianza kufua chuma kabla ya mwaka 1700 na wafuaji walikuwa wakiitwa Washana, na huo ukoo upo hata leo hii. Wapare walikuwa wakiuza bidhaa zinazotengenezwa na chuma kama majembe, mapanga, visu, silaha kama mikuki kwa makabila ya jirani mfano Wachaga, na wamekuwa na uhusiano tangu siku nyingi. Bidhaa zao hizi ziliuzwa hata kwa Wasambaa.
Jamii za Wapare zimegawanyika katika makundi ya wafugaji na wakulima. Wakati wafugaji wengi walihamia katika tambarare za Upareni, wakulima waliishi milimani na wafuaji wa chuma walikaa maeneo yote yaliyokuwa na uwezekano wa kupata chuma.
Utamaduni
Kwa asili Wapare hupeleka vijana wa kiume jando (mshitu) ambako walipata mafunzo jinsi ya kuishi na familia, japo siku hizi utamaduni wa kupeleka vijana mshitu hufanywa na watu wachache.
Wapare ni wachapakazi sana wakichanganya kilimo, ufugaji na biashara, ndiYo maana hata leo wana uchumi mzuri katika viwango vya Tanzania.
Tamaduni, mila na desturi za wapare zimekuwa zikifanana sana kwa koo karibu zote. Hapo kale Wapare pia waliweza kutengeneza au kuifunga mvua kwa shughuli za jadi, jambo ambalo wapo baadhi ya Wapare ambao mpaka leo wanaweza. Kwa mfano Mtemi wa Same Mohammedi Kibacha Singo, ambaye aliacha uongozi mara baada ya Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga marufuku utawala wa jadi. Kiongozi huyo aliyefariki dunia mwaka 1981 alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuleta mvua.
Pia walikuwepo hata watu maarufu maeneo ya wilaya ya Same ambao waliamini dawa fulani ambazo waliziweka shambani na hapo hakuna hata mdudu wala ndege atakayeweza kutua eneo hilo. Mambo haya na mengine mengi kwa sasa yanapotea kama si kwisha kabisa.
Wapare pia wamekuwa wakihusishwa na imani za uchawi na ushirikina kama ilivyo kwa makabila mengine Tanzania, lakini suala hili ni la mtu binafsi zaidi na si la jamii fulani peke yake kwa sababu ni imani ambazo zipo kote Tanzania na hatuwezi kunyooshea kidole eneo fulani.
Kwa wapare walio wengi, uchawi na wizi vilipigwa marufuku hadi kwenye matambiko. Mchawi na mwizi waliombewa wafe kama ikitokea wapo kwenye jamii. Kuna utamaduni unaoitwa "mma" ambapo matambiko yalifanyika mahali fulani na mwizi akaitwa pale yanapofanyikia kisha mwombaji akaulizwa angependa mwizi apewe adhabu gani.
Kwa kawaida adhabu mbili kuu ndizo zilikuwepo: kumfanya mwizi augue sana kwa muda mrefu kabla ya au kumuuwa mara moja. Mwombaji akimamua mwizi auawe basi kwa vile anaonekana kwenye matambiko, mtaalamu wa matambiko humuuwana akafariki mida hiyohiyo huko aliko. Tatizo la kuu la "mma" ni kwamba lilikuwa linaua watu wote wa ukoo wa mwizi au mchawi (lakini mwizi akiwa wa kwanza). Ni mpaka watakaopjua kuwa ni "mma" ndipo watafanya matambiko ya kutoa mnyama kafara kwa ajili ya kuzima athari za mma. Kwenye kuuzima mma ni lazima aliyedhulumiwa ahusishwe kwenye matambiko ikiwa ni pamoja na kuombwa radhi, vinginevyo mma hautazimika. Athari zingine za "mma" ni kwamba aliyeomba tambiko hilo (yaani aliyeibiwa au aliyedhulumiwa), ni lazima atoe kafara mnyama kama vile kondoo au ng'ombe kabla na baada ya tambiko. Baada ya mwizi kufa ni lazima mwombaji atoe mnyma kafara ili kuzima madhara ya "mma". Vinginevyo vifo vitokanavyo na mma humrudia mwombaji na ukoo wake.
Kuna watu maalum waliokuwa wamebobea kwenye mambo ya "mma". Kwa sababu ya matambiko hayo ndio maana wapare wengi si wezi - japokuwa siku hzi baadhi yao wamejiingiza kwenye wizi. Tambiko lingine linalofanana na hilo liliitwa " kubigha nyungu" (kwa Kiswahili - kupiga chungu). Chungu hicho kilipigwa kama tambiko la kumuuwa mtu aliyedhulumu (au ukoo wao uliohusika na dhuluma) watu wengine. Chungu hicho hupigwa chini mara moja kwa kishindo, ambapo tendo hilo lilambatana na matambiko fulani. Mara chngu hicho kipasukapo kwa mshidno ndipo ukoo wa waliodhulumu huanza kufa mmojammoja. Iliaminika kwamba kitendo cha chungu kusambaratika vipande vipande ndivyo na ukoo uliodhulumu husambaratika. Tambiko hili lilichangia kwa kiasi kikubwa Wapare kuwa kabila la wapenda haki. Nasikia tambiko hili lilikuwepo hata kwa makabila ya jirani kama vile wasambaa, Wameru n.k. Hata hivyo matambiko hayo kwa sasa hivi hayapo. Yamebaki historia kwenye kabila la wapare na hayo makabila mengine.
Ngoma za jadi zilipigwa kwa matukio maalumu kama kwenye jando au unyago, pia nyimbo za Kipare zilitumika katika ngasu kama harusi na sherehe nyingine na kupendezesha tukio husika. Baadhi ya nyimbo huimbwa hadi leo hata kwenye sherehe za ukumbini na baadhi zimerekodiwa.
Wapare walikuwa na utamaduni wa shughuli za sanaa kama methali, hadithi, maigizo n.k. wakati wa mapumziko na matukio fulani. Hali hii imepelekea kuwepo wasanii wengi maarufu wa maigizo na nyimbo kama Halima Madiwa, Jacob Steven (JB), Sinta, Sara Mvungi, Roma Mkatoliki na wengineo wengi
Kabla ya kuingia kwa tiba za magharibi Wapare walikuwa wakiamini tiba za mitishamba kwa kutibu magonjwa mbalimbali kama kirumu, kirutu n.k. Ipo miti maarufu kama mwori ambayo ilitumika. Mchango wa dawa za mitishamba kwa watoto na watu wazima ulionesha mafanikio tangu zamani na hata sasa.
Chakula kikuu kwa wapare kilikuwa ni makande (mchanganyiko wa mahindi na maharage). Aghalabu chakula hiki kiliandaliwa siku ya Ijumaa jioni hadi Jumapili jioni ili watu waweze kupumzika vizuri mwisho wa wiki bila kuwaza masuala ya upishi.
Samaki pia ni kipenzi cha Wapare wengi na ndiyo maana utawasikia watani wao wakuu yaani Wachaga wakiwatania kuwa Wapare wanakula ugali kwa picha ya samaki. Huu ni utani ulioasisiwa na wachagga baada ya kutembelea kaya nyingi za wapare na kukuta wamehifadhi samaki. Hapo ndipo mchagga mmoja alisikika akisema "Yesu yaani wapare wanapenda samaki, kila nyumba unayoingia utakutana na samaki. Yaani siku wakikosa samamki watakula ugali kwa picha ya samaki". Utani huo ulikuzwa na wachagga hadi ukaonekana kama ni kweli, ukizingatia wachagga wametapakaa nchi nzima.
Hata hivyo wapare nao wana utani wao kwa wachagga unaosema "Muagha wedi ni ula efwie". Yaani "mchagga mzuri ni yule aliyekufa" wakimaanisha kwamba wachagga wote ni walaghai na wadhulumishi wakati wote wa maisha yao. Ni mpaka atakapokufa ndipo ulaghai na udhulumishi wake vitaisha.
Miiko
Kuna miiko ya Wapare kama vile kufuatilia maji kwenye mabirika yao yaliyokuwa yakijulikana kama NDIVA; kwa wakinamama ilikuwa ni marufuku kusogelea maeneo hayo hasa wakiwa na vyungu vyao vyenye masizi au hata bila kitu.
Pia kulikuwa marufuku kwa wakinababa kula meza moja na wakinamama: walikula sehemu tofauti wanaume na wanawake bila kujali umri walizingatia jinsia tu.
Dini
Zamani Wapare walikuwa na sala tofauti kwa kila ukoo na eneo lao la tambiko. Katika karne ya 19 hadi 20 wamisionari wa Ukristo waliingia maeneo mengi ya Upare.
Imani za Wapare kwa sasa zinatofautiana kutokana na maeneo: walio kusini mwa wilaya ya Same katika maeneo ya Ndungu, Kihurio, Bendera, Hedaru, Makanya, Suji, Chome, Tae, Gonja, Mamba hadi Vunta kuna waumini wa kanisa la Sabato wengi sana.
Maeneo kama Chome, Mbaga, Gonja, Vudee yana waumini wengi wa Kanisa la Kilutheri.
Katika Wilaya ya Mwanga kuna idadi kubwa ya Walutheri na Waislamu.
Wakatoliki, japo ni wachache, wanapatikana zaidi katika maeneo ya Kisangara Juu, Vumari na Mbaga.
Koo
Wapare wana koo nyingi na majina mengi yakiwa na maana ya maeneo ya asili yao au mazingira ya kuzaliwa kwao, mfano Mbwambo, Mjema, Msangi, Mgweno, Mvungi, Msuya, Mgonja n.k. wana asili ya maeneo yao kama Bwambo, Mjema, Usangi, Vungi, Suya, Gonja n.k.
Mifano ya majina ya watoto wa Kipare
Majina ya kike: (Mazina a vabora va Chasu)
Ingiahedi, Itikija, Kafue, Kapingu, Kapwete, Kodawa, Kokiambo, Komkwavi, Kompeho, Kondisha, Ludao, Mchikirwa, Mshinwa, Mwajuma, Naanjela, Nacharo, Naelijwa, Naetwe, Nafue, Nahuja, Nakadori, Nakiete, Nakijwa, Nakimo, Nakunda, Nakundwa, Namkunda, Nabera, Namangi, Nangasu, Naomba, Nambike, Nampingu, Namshitu, Namsi, Namwai, Namwasi, Nangena, Nanguji, Nanguma, Nankondo, Nanyika, Nanza, Nanzano, Nanzighe, Narindwa, Nasero, Nashumbwe, Natujwa, Navoneiwa, Navuri, Navushiku, Ngalakere, Nghuhia, Niendiwe, Nietiwe, Ntevona, Sangiwa, Shode, Yunesi.
Majina ya kiume:
Bumija, Chali, Chaligha, Charo, Charema, Chedieli, Chuma, Elieseri, Eliesikia, Elinighenja, Elibariki, Elifazi, Elitumaini, Fue, Ghuheni, Gurisha, Ibwe, Igaria, Irema, Irigo, Irira, Kadio, Kadiva, Kajiru, Kakore, Kalage, Kalimbo, Kalinga (jina hili pia lipo Mkoa wa Iringa), Kalutu, Kambaita (jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kaniki, Kanyempwe, Karia (jina hili lipo pia kwa Wachagga), Kateri, Kazeni, Kazoka, Kejo, Kiandiko, Kiandiko, Kiangi, Kiariro, Kideghedo (Same), Kideghesho (Mwanga), Kihara, Kijo, Kilave, Kileghe, Kileng'a, Kinenekejo (wengine hufupisha na kuita Kejo), Kintungwa, Kipesha, Kisamo, Kisenge, Kitojo, Koshuma, Kutua, Letei, Liana, Linga, Lukiko, Lukio, Lukungu, Lusingu, Macha (jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni ukoo), Machwa, Madoffe, Maghembe (jina hili lipo pia kwa Wasukuma likiwa na maana ya majembe), Maliondo, Mapunjo, Mashuve, Mbajo, Mbasha, Mbazi, Mbonea, Mbuji, Mcharo, Mding'i, Mgheni, Mhando (jina hili pia lipo mkoa wa Tanga), Minja (jina hili pia lipo kwa Wachaga ambapo kwao ni ukoo), Mkodo, Mkwavi, Mlavwasi, Mmari (jina hili lipo pia kwa Wachaga lakini maana zikiwa tofauti. Kwa Wapare lina maanisha "mtafuta mali"), Mnaro, Mndima, Mntambo, Mntindi, Mnyindo, Mrekwa, Mrimi, Mrinde, Mrindwa, Mrindoko, Mrio, Mroki, Mshigheni, Mtango, Mtengeti, Mtera, Mteti, Mwanyika (jina hili pia lipo Mkoa wa Njombe), Mweri, Mweta, Mzangaze, Nachai, Ndago, Ngasu, Ngomoi (Same), Ngomuo (Ugweno), Nguve, Ngwijo, Niarira, Nisaghurwe, Nkima, Ntarishwa, Ntekaniwa, Nyange (jina hili lipo zaidi kwa Wachagga lakini linatumika hata kwa Wapare. Kwa Wachagga ni ukoo ambapo kwa Wapare ni jina tu la kawaida), Nzao, Nziajose, Nziamwe, Ojuku, Ombeni, Pekea, Ringo (jina hili lipo pia kwa Wachagga ambapo kwao ni ukoo), Sechome, Sechuma, Sefue, Semboja, Sempeho, Sempombe, Semu, Sengasu, Sengondo (Mwanga), Senguji, Senkondo (Same), Senkoro, Senzia, Senzota, Sevuri, Shaghude, Taseni, Tenga (jina hili pia lipo kwa Wachagga ambapo kwao ni ukoo), Tenshigha, Teri, Twazihirwa, Warema, Zihirwa, Zihirwani.
Ikumbukwe kwamba majina haya si ya koo bali ni majina ambayo Mpare yeyote anaweza akachukua au akamwita mtoto wake. Pia majina haya ni baadhi tu kati ya majina mengi ya Wapare yakiwa na maana tofautitofauti.
Maendeleo
Kama ilivyo kwa makabila mengine Wapare nao wamepiga hatua kubwa kwenye maendeleo ya elimu, siasa na uchumi. Zipo shule nyingi za zamani na mpya katika maeneo ya Wapare. Mazao ya chakula na biashara kama mpunga, katani, mahindi n.k. zimeinua maendeleo ya uchumi.
Pia miundombinu kwa kiasi chake imeboreshwa, kuna mabasi ya Kilenga yafanyayo safari mkoani Kilimanjaro, pia magari yafanyayo safari za mikoani kama Ngorika.
Kwa upande wa siasa wapo pia Wapare ambao wamepiga hatua kubwa katika nyanja za siasa kama Cleopa Msuya aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Asha Rose Mtengeti Migiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kawe, na wengineo wengi kama Anna Kilango Malechela, Profesa Jumanne Maghembe, Michael Kadeghe n.k. Pia Chediel Yohane Mgonja aliyewahi kuwa mwanasiasa maarufu nchini.
Wagweno
Hata hivyo Wapare wa Mwanga wamegawanyika katika jamii mbili: Wasangi na Wagweno. Wakati Wasangi anaongea Kipare kinachoongelewa pia na Wapare wa maeneo mengine, Wagweno wao wana lugha yao iitwayo Kigweno. Kigweno ni mchanganyiko wa Kipare na Kichagga. Hii inaonesha kuwa asili ya Wagweno ni Uchagani, japo zipo nadharia kadha wa kadha zinazoeleza asili ya Wagweno kuwa huenda hata hawana asili ya Uchaga wala Upare lakini mbali na uhusiano wa lugha kinachofanya waonekane kuwa ni sehemu ya Wapare ni namna tamaduni zao nyingine zinavyofanana na Wapare, pia kuchanganyika katika maisha ya kila siku kwenye milima ya Wapare pamoja na Wagweno wengine kuwa na majina ya koo zinazofanana na za Wapare kama Wasuya na Wavungi. Hata hivyo mila na desturi nyingi za Wagweno zinafanana zaidi na zile za Wapare wengine.
Pia ifahamike kuwa Wagweno wana lugha tofauti kabisa na Wapare; maneno yafuatayo ni uthibitisho wa dai hilo:
Embea – chunga-kitendo cha kuchunga wanyama-mfano; anachunga n`gombe. Mndu (nm) (umoja) bvandu (wingi) – mtu-watu Mwana (nm) umoja (wingi) watoto –mtoto-watoto Mfu (nm) – msichana Mthoro – mvulana Mka – mke Mmi – mme Mwali – mwali Ngathu – sherehe/karamu Papa – baba Mama – mama Lumbwio – dada Koko (Mkeku – mlala) – Bibi Kaka – babu Chacha – babu wa baba/mama Chocho – bibi wa mama/baba Mborere – mbaraka/Baraka Ndima (nm) – kazi Kiamba (nm) – hekari/kipande cha shamba Itara (nm) – 1.Chatu 2.namna ya kuhesabu Mfiri/mifiri (nm) –siku Fura – penda Njicha kv – nzuri Mwiri – 1.mwezi 2.mbalamwezi; usiku wa giza Mmbari (nm) – jua Mkwabvi (nm) – mmasai Mfwi (nm) – mshale Bvura – upinde Mnyika – wakuja Mringa (nm) – maji Bvota – ushindi Ifuru – Nyumba za kigweno zinazo ezekwa kwa majani na zinajengwa na miti na matope na juu ya paa huwekwa chungu. Ifire – mjinga Nyungu – chungu Njiu – nyeusi Njewa – nyeupe Ndhinya/nguju – nguvu Kijo nm – chakula Ngwi – kuni Ngwia – mboga za majani/mchicha Mnafu – Mboga ya majani/mchicha Makungu – Makweme. Mmea unao tambaa katika miti na unatambaa kwa urefu mkubwa sana. Mabele – Chakula cha ndizi na magimbi yaitwayo maruma. Mghubva – Muwa Ipodo – Parachichi Makafi – Ndizi zilizo menywa na kukaushwa juani na kisha kutwangwa katika kinu tayari kwa kutoa unga. Ibada – Ni ugali upikwao kwa unga wa ndizi (ibada) Mwindu – Shami Mara – 1.Majani 2.mate Mkunga – Samaki aina ya kambale Kyaru – kiatu Ipere – Samaki aina ya perege Bvughai – Ugali Maruma – Aina ya magimbi yalimwayo Ugweno Ngumba – Kiazi kitamu Ghira – Zaa Unyonge – ujauzito Mda – mimba Kibvocha – motto mchanga Agha – jenga Mshomo – mnon`gono Ukunga – yowe Kia – kiazi kitambaacho katika miti bali huenda chini zaidi ardhini na kuzaa kiazi. Kichumbi – kiti Mghombo – Ni mmea utumikao kutibu magonjwa kama malaria/homa Mthabvi – mchawi Logha – Loga Kigoda – Kiti kidogo kikaliwacho jikoni Mshombe – supu Embea – kuchunga Mrungu/rubva – Mungu Mfumwa – Bwana Mwiri - Mkwe Wau – Mke mwenza Chamwi – 1.Sura 2.Paji la uso Marwi – Masikio Mitho – Macho Mumu – Mdomo Mbua – Pua Mamua –Kamasi Mithori - Mchozi Maghegho – Meno Mara – Mate Mabvoko – Mikono Mnyu – Kidole Njwala – Kucha Mbafu – Kifua Mbari – Mbavu Mabvele – Matiti Ndenyi – Tumbo Ndii - Magoti Ngobvori – Kishikizo cha mzinga Njuki – Nyuki Kolo – Ndevu Irende – Mguu Mrwe – Kichwa Mwiri -Mwili Munyu – Chumvi Mwaru – Mzinga Mnyuka – Dawa ya kutibu tumbo Mri – 1.Mti 2. Mji Mrinyi – Mjini Mwera – Mvua M`mbari – Jua Mkuta – Upepo Lukungu – Ukungu Thari – Samadi Maumagho – Mkojo Ighwe – Jiwe Maobva – Maua / iobva-ua Mghomba – Mgomba Irughu - Ndizi Lugho – Ungo Mwinu – Mtwangio Kitela – Chungu kidogo (hutumika kupikia mboga) Kichinga – Kijinga Mriko – Mwiko Figha – Figa Mti – Moshi Maifu – Majivu Mtiri – Masinzi Mlale – Kilui – Vumbi Ubvuva – Sokoni Kali - Dari Logha – Loa Irinda – Gauni Makuru – Mavi ya kuku Marufi – Mavi/kinyesi Kenyi – Nyumbani Bvuki – Asali Kala – Zamani Bvuwaji – Ugonjwa Nganda – Ukuta Ghari – Chumba Mtiru – Msitu Ighwe – Jiwe Ndege – Ndeghe Kitonga – Zawadi Mbuta – Faini Shina – Kitininyi Maemba – Mahindi Ingobe – Barage Mafura – Mafuta Moro – Moto Kithungi – Kiyota Mdegho – Mtego Teri – Udongo Mfwa –M`ba Mbeghu - Mbegu Kaka – Zamani Ibore – Yai Mshundi – Yai bovu Ighua – Mfupa Iboho – Zizi Mbinga – Kibuyu Mbingu – Hirizi Ngwaru – Kata M`bala – Magadi Ishamba – Shamba Mwaka – Mpaka (mpaka wa shamba) N`ganda – Ukuta Matanonyi – Njia panda Irabva – Kuti Ifumburughu – Bundi Choti/mlango - Mlango Lungo – Ungo Kirero – Msemo Njafi – Pombe Itondo – Tope Mbirimbiri – Pilipili Ibata – Bata Idungunya – Nyanya Ibvula – Utumbo Bvwarimu – Wazimu Mkwaju – Mkongojo Ndhata – Fimbo Ngalawa – Boti Mwenyi – Mwenyeji Ibwe – Ndizi moja Kiringo – Kichane Imwaran`ga – Mfwi – Mshale Bvura – Upinde
Majina ya rangi Nyiu – Nyeusi Njewa – Nyeupe Mrotoma – Nyekundu
Kuhesabu siku/majira. Icho – Juzi Ithanya – Leo Ngama – Kesho Ighuo – Jana Lubvaha – Sasa Ikero-kakero – Asubuhi Mthaghari – Mchana Ikindia - Jioni
Kuhesabu namba Ibvoka – Moja Ibvi – Mbili Iraru – Tatu In`nya – Nne Ithwanu – Tano Thita – Sita Thaba – Saba Mnane – Nane Kenda – Tisa Ikumi – Kumi
Kuhesabu miezi Mwiri webvoka – Mwezi wa kwanza Mwiri wa kabvi – Mwezi wa pili Mwiri wa kararu – Mwezi wa tatu
Kuhesabu makumi Ikumi yebvoka – Kumi Ikumi ya kabvi – Ishirini Ikumi ya kararu – Thelathini Ikumi ya kana – Arobainoi Ikumi ya kathwanu – Kumi na tano Ikumi ya thita – Kumi na sita Ikumi ya thaba – Kumi na saba Ikumi ya mnane – kumi na nane Ikumi ya kenda – Kumi na tisa Maghana/ighana (umj) – Mia moja
Kuhesabu mamia (kwa wingi na umoja) Ma/ighana yebvoka – mia moja Ma/ighana abvi – mia mbili Ma/ighana kararu – Mia tatu Ma/ighana kanya – Mia nne Ma/ighana athwanyu – Mia tano Ma/ighana thita – Mia sita Ma/ighana thaba – Mia saba Ma/ighana mnane – Mia nane Ma/igihana makenda – Mia tisa Maelfu yebvoka
Matunda Ibera – pera Mkwachu – ukwaju Ipapayu – Papai Mkwachu – Mkwaju Mbvambarau – Zambarau
Wadudu Nditi – Sisimizi Machichi – Chungu Thafu – Siafu Mthaghu – Mchwa Kimae – Malkia/mama wa mchwa Madude – Funza Maenje – Mende Mandhi – Mainzi Kirawi – M`bu
Wanyama Itara nm - chatu Njoka nm – nyoka Mlula nm – chui Kite nm – mbwa Ngubve nm – Nguruwe Mbebva nm – Panya Kinyau nm – Paka Kisheghe/mrondwe nm – Kicheche Kibiba nm – Panyabuku Iobo nm – Nyani Kichakoro nm – Njefu nm – Tembo N`gumbe nm – N`gombe Mburi nm –Mbuzi Ngache nm – Ndama Igonji nm – Kondoo
Maeneo Barebarenyi – Barabarani Mbai – Chini Ughu – Juu Botonyi – Bondeni Mfonyi – Mtoni Mtiru – Msitu Fumbu – Jangwa/eneo wazi Ubvanja – Uwanja Bwan`ga – Nje Bvoshi – Ndani
Maneno takribani yote hayahusiani kabisa na Kipare bali yanakaribiana sana na Kichaga cha Rombo.
Tazama pia
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wapare kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |