Eneo la utawala

(Elekezwa kutoka Ngazi za utawala)

Eneo la utawala ni sehemu ya nchi iliyotengwa kwa madhumuni ya utawala. Kwa kawaida kuna ngazi tofauti za ugatuzi kama vile mkoa, wilaya, tarafa, kata/shehia na kijiji na kila moja ina madaraka yake.

Madaraka ya utawala

hariri

Madaraka ya kila ngazi ya utawala hutegemea katiba na siasa ya nchi.

  • katika kila mfumo kuna uwezekano kwamba maeneo ya ngazi ya chini kama manisipaa, miji, kata au vijiji huwa na madaraka ya pekee yanayotajwa katika katiba ya nchi.

Ngazi za utawala

hariri

Majina ya vitengo vya kiutawala hutofautiana kati ya nchi na nchi. Kwa kusudi la kulinganisha hutajwa mara nyingi kufuatana na ngazi chini ya serikali kuu

  • ngazi ya kwanza: eneo lililo moja kwa moja chini ya ngazi ya kitaifa; mfano mikoa ya Tanzania, kaunti za Kenya, majimbo ya Marekani
  • ngazi ya pili: ni vitengo chini ya eneo ngazi ya kwanza; mfano ni wilaya za Tanzania, sub county za Kenya. Katika nchi nyingi miji mikubwa hupangwa hapa
  • ngazi ya tatu: ni migawanyo ya maeneo ya ngazi ya pili; mfano ni tarafa za Tanzania
  • ngazi ya nne na ya tano ni migawanyo tena ya maeneo katika ngazi za juu. Mara nyingi vijiji, miji midogo au maungano ya vijiji hupangwa hapa. Mfano ni kata na vijiji au mitaa katika Tanzania.
  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eneo la utawala kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.