Nyamugali ni kata ya Wilaya ya Buhigwe katika Mkoa wa Kigoma, mpakani mwa Tanzania na Burundi.

Kata hii imeundwa na vijiji viwili: Nyamugali na Burimanyi.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 7,405 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 10,705 waishio humo.[2]

Hali ya hewa ya Nyamugali ni joto kiasi wakati wa masika na baridi kiasi kwa kiangazi; hii hutokea pekee majira ya asubuhi, wakati mchana jua huwa kali.

Shuguli za kiuchumi ni kilimo, usafirishaji, ufugaji, biashara pamoja na ufundi kama ushonaji wa nguo na unyoaji nywele. Kilimo kama shuguli kuu inayofanywa karibu na asilimia 90 ya wakazi wa Nyamugali bado hakijaendelea sana kwani vifaa duni ndizo nyenzo zinazotumiwa.

Ugali wa mhogo ndio chakula kikuu kwa wakazi wa kata hii; vyakula vingine ni pamoja na viazi vitamu, maharage na ugali wa mahindi.

Elimu katika kata hii imekuwa ikiongozeka siku hadi siku huku ikikumbwa na uhaba wa shule za msingi na sekondari, shule ya sekondari Buha ikiwa ndiyo sekondari pekee inayohudumu kata hii pamoja na vijiji jirani vya Biharu na Kigege.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Buhigwe - Mkoa wa Kigoma - Tanzania  

Biharu | Buhigwe | Bukuba | Janda | Kajana | Kibande | Kibwigwa | Kilelema | Kinazi | Mkatanga | Mubanga | Mugera | Muhinda | Munanila | Munyegera | Munzeze | Muyama | Mwayaya | Nyamugali | Rusaba

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kigoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyamugali kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.