Nyenje (Grylloidea)

Nyenje
Nyenje mkia-upanga (Triconidium sp.)
Nyenje mkia-upanga (Triconidium sp.)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Orthoptera (Wadudu wenye mabawa nyofu)
Nusuoda: Ensifera (Wadudu kama nyenje)
Familia ya juu: Grylloidea (Nyenje)
Laicharting, 1781
Ngazi za chini

Familia 6 (4 katika Afrika):

Nyenje ni wadudu wa familia ya juu Grylloidea katika oda Orthoptera au wa familia ya juu Cicadoidea katika oda Hemiptera. Wana jina moja labda kwa sababu sauti zao zinafanana. Wale wa Cicadoidea huitwa nyenje-miti pia. Makala hii ni kuhusu wale wa Grylloidea.

Maelezo

hariri

Sifa zinazotofautisha nyenje katika familia ya juu Grylloidea kutoka spishi nyingine za nusuoda Ensifera ni vipapasio virefu kama nyuzi, tarsi zenye pingili tatu, serki nyembamba zinazoweza kuhisi kwenye ncha ya fumbatio na nywele za hisia kwenye serki. Ni wadudu pekee wanaoshiriki mchanganyiko huu wa sifa.

Mwili wa nyenje una umbo la mcheduara katika takriban spishi zote za Grylloidea, lakini kwa nyingine ni kama duaradufu. Vipapasio ni virefu na kama nyuzi. Pronoto haina mkuku na sahani za mgongo ni bapa na hazina mabamba au miiba. Tarsi zina pingili tatu na tibia za miguu ya mbele hubeba viungo vya kugundua sauti (timpano). Mabawa ya mbele ya dume hubeba viungo vya kupiga sauti. Sauti hutengenezwa wakati tupa kwenye bawa moja inasuguliwa na kikwaruzo kwenye bawa jingine. Kuna serki mbili kwenye ncha ya fumbatio na hakuna stili kwenye sahani ya chini ya kizazi.

Mwainisho

hariri

Familia zinazofuata zimeshirikisha katika familia hii ya yuu: