Nyoka-kijiti
Nyoka-kijiti | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Nyoka-kijiti kusi (Thelotornis capensis)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 4:
|
Nyoka-kijiti ni spishi za nyoka wa jenasi Thelotornis katika familia Colubridae. Wakikaa tuli mtini wanafanana na kijiti au kitawi kilichokauka.
Nyoka hawa ni wembamba sana na warefu kiasi: kwa wastani sm 90-130 na kipeo cha m 1.4-1.6 kulingana na spishi. Kichwa kina umbo wa mshale na mboni zina umbo wa tundu la ufunguo. Rangi yao ni kijivu au kahawia lakini kichwa ni kijani kabisa au juu yake tu.
Nyoka-kijiti huishi mitini ambapo huwinda mijusi, vyura na ndege wadogo. Mara nyingi hukaa chini kiasi ili waweze kushambulia mawindo yaliyo ardhini.
Chonge zao ni meno ya nyuma kabisa lakini wanaweza kuingiza sumu waking'ata mtu. Kwa bahati nzuri nyoka hawa ni waraufu na hawang'ati kwa kawaidi. Hata hivyo sumu hii ni toksinidamu kali na hakuna makata na mara nyingine watu hufa baada ya kuumwa. Nyoka hawa wakitishwa shingo yao inafura na kuonyesha mabaka meusi au kahawia.
Spishi
hariri- Thelotornis capensis Nyoka-kijiti Kusi (Savanna vine snake)
- Thelotornis kirtlandii Nyoka-kijiti Misitu (Forest vine snake)
- Thelotornis mossambicanus Nyoka-kijiti Mashariki (Eastern vine snake)
- Thelotornis usambaricus Nyoka-kijiti wa Usambara (Usambara vine snake)
Picha
hariri-
Kichwa cha nyoka-kijiti kusi
-
Nyoka-kijiti ikiwa na shingo iliyofura
-
Nyoka-kijiti misitu
-
Kichwa cha nyoka-kijiti mashariki
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-kijiti kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |