Nyoka-miti Kichwa-kipana
Nyoka-miti kichwa-kipana | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 2:
|
Nyoka-miti kichwa-kipana ni nyoka wa jenasi Toxicodryas katika familia Colubridae. Amepewa jina hili kwa sababu hukaa mitini takriban masaa yote na kichwa ni kipana kuliko nyoka-miti wengine.
Nyoka hawa ni warefu, hadi m 2.8 lakini m 1-2 kwa kawaida. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia juu na njano au pinki chini.
Kama jina lao linadokeza huishi mitini ambapo hukamata vyura, mijusi, vinyonga, ndege, mayai ya ndege, wagugunaji wa miti na popo.
Chonge ni meno ya nyuma. Sumu yao inaweza kuwa na hatari kwa watu lakini mifano ya shida kubwa haijulikani. Hata hivyo inaambilika kuzuia kung'atwa na nyoka hawa.
Spishi
hariri- Toxicodryas blandingii, Nyoka-miti wa Blanding (Blanding's tree snake)
- Toxicodryas pulverulenta, Nyoka-miti wa Fischer (Fischer's tree snake)
Marejeo
hariri- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-miti Kichwa-kipana kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |