Nyoka-miti mweusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Colubrinae
Jenasi: Thrasops
Hallowell, 1857
Ngazi za chini

Spishi 4:

Nyoka-miti weusi ni spishi za nyoka za jenasi Thrasops katika familia Colubridae. Wanafanana na kukwi-miti lakini rangi yao ni nyeusi badala ya kijani.

Nyoka hawa ni warefu kuliko kukwi: kwa kipeo m 2-2.5 kulingana na spishi na kwa wastani m 1.4-1.8. Magamba ya mgongo ya T. jacksoni na T. schmidti yana miinuko lakini yale ya spishi nyingine ni laini. Magamba ya tumbo ya spishi zote yana miinuko pia inayosaidia nyoka hawa kupanda juu ya miti. Rangi yao ni nyeusi lakini koo ni kijivu, jeupe au njano mara nyingi.

Nyoka-miti weusi huishi mitini ambapo huwinda mijusi, vinyonga na vyura. Mara nyingi hukamata mamalia na ndege wadogo na hula mayai ya ndege pia. Pengine hukamata chura ardhini.

Nyoka hawa hawana sumu na hawang'ati kwa kawaida, lakini wanafanana sana na namna nyeusi ya ngole na kwa hivyo jihadhari. Wakitishwa hujaribu kutoroka na mara nyingi huruka chini, hata katika maji. Shingo yao inafura wakitegwa.

Spishi hariri

Marejeo hariri

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka-miti Mweusi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.