Nyukibambi
Malkia wa Bombus lapidarius
Malkia wa Bombus lapidarius
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba)
Familia ya juu: Apoidea (Hymenoptera kama nyuki)
(bila tabaka): Anthophila
Familia: Apidae
Nusufamilia: Apinae
Kabila: Bombini
Jenasi: Bombus
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Spishi >250, 5 katika Afrika:

Nyukibambi (kwa Kiing. bumblebees) ni nyuki wakubwa kiasi wa jenasi Bombus katika family [[Apidae] ] ya oda Hymenoptera walio na nywele nyingi. Ingawa wana jina la Kiswahili, hawapatikani Afrika kusini mwa Sahara. Wanatokea zaidi Ulaya, Asia na Amerika. Katika Afrika ya Kaskazini, haswa Aljeria, Maroko na Tunisia, kuna spishi 5[1]. Hawa ni nyuki wa kijamii[2] wanaotengeneza viota vyao kwenye machimbo yaliyopo ardhini au matundu mitini au juu ya ardhi kwenye nyasi nzito[3]. Spishi za nusujenasi Psithyrus ni vidusia wa kijamii ambao hunyakua viota vya nyuki wengine ambao wafanyakazi wao hulea majana ya mnyakuzi[4].

Maelezo hariri

Nyukibambi kwa ujumla wana urefu wa mm 10-25 kulingana na spishi na tabaka[5], ingawa spishi kubwa kabisa, Bombus dahlbomii, inaweza kufikia mm 40 na pengine huitwa panya anayeruka. Ukubwa hutofautiana ndani ya spishi na malkia wa B. terrestris kuwa mm 22, madume mm 16 na wafanyakazi mm 11-17. Nyuki hawa ni imara kuliko nyuki-asali na ncha ya fumbatio yao ni mviringo zaidi. Wana nywele nyingi. Rangi ya kutikulo yao ni nyeusi na nywele nyingi ni nyeusi lakini kuna milia ya nywele za rangi, kwa kawaida nyeupe, njano, machungwa, nyekundu au pinki. Hizi ni rangi za onyo ambazo zinaonyesha kuwa majike wanaweza kutoa mchomo uletao uchungu. Kwa sababu ya ndimi zao ndefu nyukibambi wanaweza kukusanya mbochi kutoka kwa maua ya kina kirefu kuliko nyuki-asali.

Spishi za Afrika hariri

  • Bombus mocsaryi
  • Bombus lapidarius
  • Bombus ruderarius
  • Bombus ruderatus
  • Bombus terrestris

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. http://www.atlashymenoptera.net/page.aspx?id=169
  2. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2022-11-03. Iliwekwa mnamo 2022-11-03.
  3. Bumblebee nests. Bumblebee Conservation Trust. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-09-22. Iliwekwa mnamo 2022-11-03.
  4. https://www.bumblebee.org/cuckoo.htm
  5. https://www.orkincanada.ca/pests/bees/bumblebees/