Jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta duniani
Jumuiya ya nchi zinazozalisha mafuta duniani (Kiing. Organization of the Petroleum Exporting Countries), kwa kifupi pia OPEC ni shirika la kimataifa linalounganisha nchi zinazozaa mafuta ya petroli. Makao makuu yako Vienna (Austria).
Kwa pamoja nchi hizi zina takriban asilimia 75 za akiba ya mafuta duniani katika ardhi yao. Kwa sasa zinalisha asilimia 40 ya mafuta yanayotolewa kila mwaka. Kutokana na kupungua kwa akiba za nchi zisizoshiriki katika OPEC inaonekana ya kwamba athira ya nchi za OPEC itakua.
Nchi wanachama
haririOPEC ina nchi wanachama 13 ambazo ni
- Algeria
- Angola
- Ecuador
- Indonesia
- Iran
- Iraq
- Kuwait
- Libya
- Nigeria
- Qatar
- Ufalme wa Uarabuni wa Saudia
- Falme za Kiarabu
- Venezuela
Kiini cha OPEC ni nchi za Waarabu.
Indonesia imetangaza ya kwamba inatarajia kuondoka katika OPEC kwa sababu mahitaji yake ya mafuta yanazidi kiasi cha mafuta inayozalisha.
Nchi muhimu zisizo wanachama
haririKati ya nchi muhimu ambazo zinatoa mafuta mengi duniani kuna idadi ambazo si mwanachama kama vile Urusi, Marekani, China, Mexiko, Kanada, Norwei na Uingereza.
Shabaha
haririNchi wanachama walijumuika kwa majukumu yafuatayo:
- Kulinda shauku za pamoja za nchi zinazolisha mafuta ya petroli
- Kujikinga dhidi mabadiliko ya bei ya mafuta ya petroli ya mara kwa mara
- Kuhakikisha mblimbiko wa kutegemea kwa nchi wateja
- Kuhakikisha ya kwamba nchi zinazolalisha mafuta yanapokea mapatoy a kutosha kwa mahitaji yao
- Kuwa pamoja kuhusu siasa za mafuta
Mara nyingi OPEC haikufaulu kushikamana kwa nchi zote.
Kiasi cha mafuta kilichokubaliwa kwa kila mwanachama
haririNchi wanachama zimepatana kati yao kiasi kwa kila nchi kinachotolewa na kuuzwa. Kipimo chake ni "mapipa kwa siku" na "pipa" moja ni swa na lita 158,98 za mafuta ya petroli. Kusudi la siasa hii ni nia ya kuzuia bei isishuke kwa sababu kama nchi moja inayohitaji hela inaanza kutoa mafuta mengi kumbe bei ya mafuta ingeshuka chini.
Nchi | Kiasi kinachokubaliwa (7/1/05) | Uzalishaji (1/07) | Uzalishaji unaowezekana |
---|---|---|---|
Algeria | 894 | 1,360 | 1,430 |
Angola | 1,900 | 1,700 | 1,700 |
Ekuador | 520 | 500 | 500 |
Iran | 4,110 | 3,700 | 3,750 |
Iraq | 1,481 | ||
Kuwait | 2,247 | 2,500 | 2,600 |
Libya | 1,500 | 1,650 | 1,700 |
Nigeria | 2,306 | 2,250 | 2,250 |
Qatar | 726 | 810 | 850 |
Saudia | 10,099 | 8,800 | 10,500 |
Falme za Kiarabu | 2,444 | 2,500 | 2,600 |
Venezuela | 3,225 | 2,340 | 2,450 |
Jumla | 31,422 | 30,451 | 32,230 |
Viungo vya Nje
hariri- OPEC official site Ilihifadhiwa 7 Agosti 2006 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |
- ↑ Quotas as reported by the United States Department of Energy