Mpunga
(Elekezwa kutoka Oryza)
Mpunga (Oryza spp.) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mpunga wa kiasia
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mpunga ni aina ya mimea katika familia ya manyasi (Poaceae). Spishi kadhaa zinapandwa katika sehemu mbalimbali za dunia, lakini mpunga wa kiasia ni ile ya kawaida.
Mpunga ni chanzo cha chakula kwa watu wengi duniani. Punje (mbegu) zake ni nafaka na huitwa mchele. Mchele uliopikwa ni wali.
Spishi
hariri- Oryza barthii, Mpunga-porini wa Afrika (African wild rice)
- Oryza glaberrima, Mpunga wa Afrika (African rice)
- Oryza longistaminata, Mpunga stameni-ndefu (Longstamen rice)
- Oryza rufipogon, Mpunga mwekundu (Red rice)
- Oryza sativa, Mpunga wa Asia (Asian rice)
- Oryza nivara, Mpunga-porini wa Uhindi (Indian wild rice)
Picha
hariri-
Mpunga wa kiasia (maua)
-
Mashamba ya mpunga huko China
-
Mashamba ya mpunga nchini Kenya