Mpunga
(Oryza sativa)
Mpunga
Mpunga
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja tu)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama kongwe)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo na mnasaba na nyasi)
Jenasi: Oryza
Spishi: O. sativa
L.

Mpunga wa kiasia ni mmea wa familia ya manyasi katika ngeli ya monokotiledoni. Mbegu au punje za mpunga zikisafishwa huitwa mchele na mchele ukipikwa ni chakula cha wali. Wali ni chakula muhimu cha watu katika sehemu nyingi za dunia hasa Asia lakini pia Afrika na penginepo.

Mama anatoa miche ya mpunga kabla ya kuipanda shambani
Shamba la mipunga huko Bangladesh
Mipunga iliyoiva (Marekani)[[1]]
Mpunga kabla ya mavuno nchini Japani
Mavuno ya mpunga nchini Hispania
Oryza sativa[[2]]

Historia ya mpunga

hariri

Asili ya mpunga iko katika Asia. Wataalamu huamini ilipatikana mwanzoni ama China ya kusini au Uhindini. Wengine huona ya kwamba manyasi ya aina Oryza sativa yaliendelezwa na wakulima China na Uhindi kila mahali bila kutegemeana. Wakulima waliona manyasi yenye mbegu nzito kushinda manyasi mengine waliteua yale yaliyokuwa kubwa hasa na kuyapanda kwenye matuta ya bustani. Kwa njia hiyo manyasi yenye nafaka nzito yalipatikana. Wataalamu wa akiolojia walitambua alama za mpunga na matumizi yake katika mabaki yenye asili ya mwaka 6000 KK katika China na mwaka 5000 katika Uhindi.

Mnamo karne ya 3 KK mpunga ulipelekwa Japani kutoka China na kuwa chakula kikuu.

Afrika

hariri

Aina nyingine ya Oryza (k.m. O. glaberrima na O. barthii) zilikuzwa katika Afrika ya Magharibi. Baadaye Waarabu walileta aina ya kiasia iliyopandwa zaidi kutokana na mavuno makubwa. Hata sasa mpunga wa kiafrika (O. glaberrima) hupandwa kidogo kidogo. Tangu miaka ya 1990 haibridi za O. sativa na O. glaberrima zinakuzwa zinazoitwa "Nerica" (New Rice for Africa).

Uenezaji

hariri

Kutoka Bara Hindi mpunga ulipelekwa magharibi. Waroma wa Kale walijua mpunga wakala wali iliyolimwa Misri. Baadaye Waarabu walipeleka mpunga wa aina ya O. sativa katika sehemu mbalimbali za Afrika.

Wahispania na Wareno walipeleka mpunga hadi Amerika walipoulima katika koloni zao.

Kilimo

hariri

Hadi leo maeneo makuu ya kilimo cha mpunga yako Asia hasa China, Bara Hindi na Asia ya Kusini-Mashariki. Asilimia 95 ya mavuno ya dunia hupatikana huko. Maeneo mengine ya maana ni kusini ya Marekani na Italia ya Kaskazini. Penginepo mavuno hayana maana ya kimataifa hata kama kilimo cha mpunga kwenye nchi kama Tanzania au Kenya ina umuhimu fulani wa kimahali.

Mpunga hulimwa hasa kwa njia mbili:

  • "bichi" kwenye mashamba yanayogharikishwa na mpunga unapandwa katika maji.
  • "kavu" kwenye mashamba ya kawaida kwa kutegemea mvua

Kwenye mtindo "bichi" mpunga hupandwa katika maji na mimea hukua kwenye maji vilevile. Maji huzuia majani ya kando yasiyotakiwa na wadudu wengi. Wakulima wengine wanatumia mabwawa yale pia kwa kukuza samaki kwenye shamba wakati wa mafuriko. Wakati wa kuiva maji huondolewa ili mpunga upate kukauka kabla ya mavuno.

Mpunga

hariri

Mpunga ni mbegu ya mmea wa jamii ya monokotiledoni ya mmea wa Oryza sativa. Ukiwa ni miongoni mwa nafaka, ni chakula kikuu kwa sehemu kubwa duniani, hasa Mashariki, Kusini na Kusini Mashariki mwa Asia, Kati na Masharik mwa Amerika ya Kusini na India Mashariki. Ni nafaka inayolimwa kwa wingi zaidi duniani baada ya mahindi.

Kwa sababu mahindi hulimwa kwa makusudi mbalimbali mbalina matumizi ya binadamu, nafaka iliyomuhimu kwa binadamu kwa maana hiyo hubakia kuwa mpunga huku ikichangia zaidi ya kalori ya moja ya tano ya kalori inayotumika duniani kote.

Kama chakula cha asili huko Afrika, mpunga husaidia kuinua na kuboresha mlo, kuongeza ulinzi wa chakula, kukuza maendeleo ya eneo husika na kusaidia maendeleo endelevu ya ardhi ya eneo husika. Mpunga marra zote hukuzwa kama zao la mwaka mmoja, japo mara kdhaa katika maeneo ya tropiki huweza kudumu kwa miaka mingi, hata kwa miaka ishirini. Mpunga hukua kufikia urefu wa mita 1 -1.8 ka kimo, na hutegemea hasa aina ya udongo na rutuba yake. Mmea huwa na majani marefu kufikia hata sentimita 50 – 100 kwa urefu na upana wa sentimita 2 – 2.5. Maua madogo yanayochvushwa kwa upepohuzalishwa, na hujishikiza kwenye fimbo ndefu zenye urefu wa sentimita 30 – 50. Mbegu yenyewe huwa na urefu takribani milimita 5 – 12 na upana milimita 2 -3.

Kilimo cha mpunga kinafanikiwa sana kwenye maeneo yenye ufanyaji kazi rahisi na kiwango kikubwa cha mvua, sababu ulimaji wake ni kazi kubwa na huhitaji mvua ya kutosha. Mpunga kwa kawaida unaweza kulimwa popote, hata kwenye kilima kikali au hata milimani haswa. Japokuwa mimea yake ya asili imetokea huko Kusini mwa Asiana sehemu Fulani za Afrika, biashara na safari za kale zimeufanya utawanyike mahali pengi duniani.

Kitamaduni, njia itumikayo kuzalisha mpunga ni kujaza maji shambani, huku au baada ya kuweka vimea vya mpunga kuanzisha shamba jipya. Njia hii rahisi huhitaji mpango na huduma ya umwagiliaji, lakini pia hupunguza idadi ya magugu na magonjwa yasiyostahimili hali ya ubichi na kuzama majini kwa muda mrefu. Wakati kukuza mpunga ndani ya maji ikiwa si lazima, njia zote nyingine huhitaji uangalizi mkubwa sana wa magugu na magonjwa ya mimea pamoja na namna mbalimbali ya kuweka mbolea katika mimea. Maandalizi kama chakula.

 
Wauzaji wa mpunga mnamo 1820 huko Japani.
 
Namna ya kale ya ukoboaji wa mpunga.

Katika kaskazini mwa Iran, katika Gilan Province, aina nyingi mchele indica ikiwa ni pamoja na Gerdeh, Hashemi, Hasani, na Gharib wamekuwa bred na wakulima.[1]

Mpunga ndiyo chakula kinacholiwa zaidi duniani. Mbegu za mpunga hukobolewa kuondoa maganda yake ya nje na kupata mchele. Mchele uliokobolewa sana hata kuondoa sehemu ya kahawia ya mchele na kupata mchele mweupe husababisha ugonjwa wa beriberi. Mchele mweupe huweza kuchanganywa na virutubisho vingine ili kuuongezea kiwango cha virutubisho na kuufanya uwe bora zaidi kwa afya ya mlaji.

 
Kilimo cha umwagiliaji cha mpunga katika vilima vya Indonesia.

Huko India mchele hupikwa kwa kuchanganywa na maziwa na kuongezewa vionjo vingine na chakula huitwa ‘payash’ au ‘ksheer’. Mchele mbichi pia huweza kusagwa kuwa unga na kutumika katika matumizi mbalimbali, ikiwa pamoja na kutengeza vinywaji mbalimbali kama vile amazake, horchata, na sake.

Mpunga ni chanzo kizuri cha protini na ni chakula kikuu katika maeneo mengi duniani, japo si protini kwa asilimia mia: haina kiasi chote cha aside za amino muhimu kwa afya, na hulazimika kuchanganywa na vyanzo vingine vya protini kama vile maharagwe, samaki na nyama.

Upishi

hariri
 
Mchele kabla ya kupikwa.

Mchele hupikwa kwa kawaida kwa kuchemsha au kuvukiza mvuke, na kufyonza maji. Inaweza kupikwa kulingana nakisi cha maji inachoweza kuchukua, au kiasi kikubwa cha maji inachokifyonza kabla ya kupikwa. Siku hizi kuna majiko maalumu ya kupikia mchele, yanayofanya kazi kuwa rahisi zaidi.

Mchele pia waweza kutumika kupikia uji kwa koungeza maji mengi kuliko kawaida, ili kwamba wali unaopikwa unakuwa na maji mengi zaidi na kutanuka zana na kuwa laini mno. Uji huu hutumika mara nyingi kama kifungua kinywa na ni chakula cha asili kwa wagonjwa.

Uzalishaji wa mpunga duniani

hariri
Faili:2005rice (paddy).PNG
Kiwango cha uzalishaji wa mpunga duniani.

Uzalishaji wa mpunga duniani [25] kiliongezeka sana kutoka tani milioni 200 mnamo 1960 mpaka tani milioni 600 mwaka 2004. Wazalishaji wanaoongoza ni China (26% ya mazao ya dunia), India (20%), Indonesia (9%) na Bangladeshi (5%).

Marejeo

hariri
  1. Pazuki, Arman; Sohani, Mehdi (2013). "Phenotypic evaluation of scutellum-derived calluses in 'Indica' rice cultivars" (PDF). Acta Agriculturae Slovenica. 101 (2): 239–247. doi:10.2478/acas-2013-0020. Iliwekwa mnamo Februari 2, 2014. {{cite journal}}: Unknown parameter |lastauthoramp= ignored (|name-list-style= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons