Tandaraka

(Elekezwa kutoka Oryzorictes)
Tandaraka
Tandaraka Mkubwa (Tenrec ecaudatus)
Tandaraka Mkubwa
(Tenrec ecaudatus)
Uainishaji wa kisayansi
Domeni: Eukaryota
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda ya juu: Afrotheria (Wanyama wenye asili ya Afrika)
Oda: Afrosoricida (Wanyama kama tandaraka)
Nusuoda: Tenrecomorpha (Wanyama kama tandaraka)
Familia: Tenrecidae (Wanyama walio na mnasaba na tandaraka)
J. E. Gray, 1821
Ngazi za chini

Nusufamilia 4:

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tandaraka (kutoka Kimalagasi: tandraka) ni wanyama wadogo wa familia Tenrecidae. Takriban spishi zote zinatokea Madagaska tu. Tandaraka mkubwa anatokea Komori, Morisi, Reunion na Shelisheli pia. Tandaraka wana maumbo mbalimbali; wengine wanafanana na kalunguyeye, wengine na virukanjia, vipanya, oposumu na hata na fisi-maji. Hii ni kwa sababu ya convergent evolution. Spishi ndogo kabisa ina urefu wa sm 4.5 na uzito wa g 5, ile kubwa kabisa urefu wa sm 25–39 na uzito wa zaidi ya kg 1. Ingawa mfanano, tandaraka hawana mnasaba na kalunguyeye, vipanya na wanyama wengine ambao wanafanana nao. Wana mnasaba na fuko-dhahabu na sengi na wamo katika jamii ya Afrotheria pamoja na pimbi, wahanga, tembo na nguva. Kinyume na mamalia wengine tandaraka wana funuo moja tu (kloaka) ili kupisha mavi, mikojo na watoto. Hukiakia usiku na hawawezi kuona vizuri, lakini wasikia sauti na harufu vizuri sana. Wanaweza kusikia sana kwa manyoya ya masharubu pia. Hula vitu vingi lakini invertebrata hasa.

Spishi

hariri

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.

  Makala hii kuhusu "Tandaraka" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili tandraka kutoka lugha ya Kimalagasi. Neno (au maneno) la jaribio ni tandaraka.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.