Pandeolwa
Pandeolwa (pia wanda; kwa Kiing. dimension) ni dhana katika hisabati na fizikia inayoeleza tabia za kiolwa katika nafasi kilichomo. Kwa maarifa yetu ya kawaida tunatofautisha pandeolwa tatu ambazo ni upana, urefu na kina / kimo.
Kwa maana hiyo mstari una pandeolwa mmoja, eneo kama mraba au mviringo huwa na pandeolwa mbili, gimba kama mchemraba au tufe huwa na pandeolwa tatu.
Ulimwengu mara nyingi huelezwa kuwa na pandeolwa nne, yaani urefu, upana, kimo na wakati.
Katika hisabati kuna nafasi ya kuangalia pandeolwa nyingine na zaidi.
Tofauti ya pandeolwa hutajwa mara nyingi kwa kifupi cha Kiingereza kama "2-d" au "3-d" yaani "2 dimensions" au "3 dimensions".
Istilahi
haririHadi sasa hakuna mapatano kamili kuhusu istilahi inayoweza kutaja "dimension" ya Kiingereza. KAST ilitumia "wanda, mawanda"[1]. Masomo yanayoandaliwa na mtandao wa TESSA[2] hutumia "pandeolwa".
Marejeo
hariri- ↑ linganisha KAST 1995, uk. 354
- ↑ Moduli 2: Kuchunguza Maumbo na Uwazi, Sehemu ya 3: Kuchunguza maumbo yenye pande 3, iliangaliwa Agosti 2022
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pandeolwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |