Pasienti wa Lyon (alifariki 480 hivi) alikuwa askofu mkuu wa mji huo, leo nchini Ufaransa [1] kuanzia mwaka 450 hivi.

Pamoja na kupambana na uzushi, alionyesha ukarimu mkubwa hasa njaa ilipoenea nchini naye alitumia mali zake zote kulisha watu wa jimbo lake na nje yake pia[2][3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Septemba[4].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.