Paul Kipsiele Koech

Paul Kipsiele Koech (alizaliwa mnamo 1981 katika Cheplanget) ni mwanariadha wa Kenya katika mbio za Mita 3000 kuruka viunzi na maji. Alishinda Nishani ya shaba katika mbio hizi katika mashindano ya Olimpiki ya 2004.

Paul Koech

Maisha ya Utoto

hariri

Alizaliwa mnamo 1981 katika sehemu ya Cheplanget, karibu na Mji wa Sotik, Wilaya ya Buret. Alifuzu kutoka Shule ya Sekondari ya Cheplanget mnamo 1999 Alitia fora katika Mbio za kitaifa za Masafa marefu na akaalikwa kukimbia Barani Uropa, akajiunga na Timu iliyokuwa ikisimamiwa na James Chepleton[1]. Licha ya kuwa mwanariadha wa kasi zaidi katika mbio hizo, Koech ameshindwa mara kadhaa katika majaribio ya kufuzu kwa Mashindano ya Dunia au Olimpiki kutoka Kenya. [2]. Alishiriki katika Finali za Dunia za All Seven zilizoandaliwa na IAAF.[3]. Pia alijenga Shule ya Msingi karibu na nyumbani kwake Yeye pia huwapa mafunzo ya Riadha Wanariadha chipukizi, akiwemo bingwa Chipukizi wa Dunia Mercy Cherono[4]. Koech ameoa na ana mtoto aliyezaliwa mnamo 2004.[1] na mdogo wa Kiume[2].

Mafanikio

hariri
Mwaka Shindano Mahali pa maandalizi Matokeo Habari ya Ziada
2003 Michezo ya Bara Afrika Abuja, Nigeria nafasi ya 2
Finali za IAAF Monte Carlo, Monaco nafasi ya 2
2004 Michezo ya Olimpiki Athens, Greece nafasi ya 3 Mita 3000 kuruka viunzi na maji
Finali za IAAF Monte Carlo, Monaco nafasi ya 3
2005 Ubingwa wa Dunia Helsinki, Finland 7th Mita 3000 kuruka viunzi na maji
finali za dunia za Riadha Monte Carlo, Monaco Mshindi
2006 Ubingwa wa bara Afrika Bambous, Mauritius mshindi
Finali za Dunia za Riadha Stuttgart, Ujerumani Mshindi
Kombe la Dunia la IAAF Athens, Greece nafasi ya 2
2007 Finali za Riadha za IAAF Stuttgart, Ujerumani Mshindi
2008 Mashindano ya Ubingwa ya Ndani Valencia, Spain Nafasi ya 2 mita 3000
Finali za riadha za IAAF Stuttgart, Ujerumani Mshindi
2009 Ubingwa wa Dunia Berlin, Ujerumani 4th mita 3000 kuruka viunzi na maji
Finali za Riadha za IAAF Thessaloniki, Greece Nafasi ya 2 3000 m kuruka viunzi na maji

matokeo bora zaidi kwake

hariri

Tazama Pia

hariri

Riadha Shirikisho la Riadha Duniani

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 21 Agosti 2004: Focus on Africa - Paul Kipsielei Koech (KEN) Ilihifadhiwa 1 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
  2. 2.0 2.1 The Standard, 12 Agosti 2009: Kipsiele Ako na Matumaini ya Ushindi Berlin Ilihifadhiwa 13 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine.
  3. IAAF, 24 Septemba 2009: World Athletics Final û a statistical farewell
  4. x]



Sporting positions
Alitanguliwa na
  Saif Saaeed Shaheen
Mita 3000 kuruka viunzi na Maji kwa wanaume, Matokeo bora zaidi ya Mwaka
2007
Akafuatiwa na
Incumbent