Peleo, Nilo na wenzao
Peleo, Nilo na wenzao (walifia dini Phunon, karibu na Petra, leo kusini mwa nchi ya Yordani, 310) walikuwa Wakristo waliochomwa moto kwa ajili ya imani yao kutokana na dhuluma ya kaisari Dioklesyano wa Dola la Roma.
Peleo na Nilo walikuwa maaskofu nchini Misri, Elio alikuwa padri. Kati ya wengine (labda 50 au 150, wakiwemo mapadri wengi) anatajwa Patermusi[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao inaadhimishwa tarehe 19 Septemba[2][3].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |