Petro wa Kapitolias

Petro wa Kapitolias (alifariki Capitolias, katika Batanea, leo nchini Yordani, 715) alikuwa padri aliyefia dini ya Ukristo mwanzoni mwa utawala wa Waislamu sehemu za Syria.

Kwa kuwa alitangaza Injili barabarani, alikatwa ulimi, mikono na miguu, na hatimaye alisulubiwa[1][2] [3] kama alivyotamani sana.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Januari [4] au 4 Oktoba.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.