Asiti
Ndege wadogo wa Madagaska wa familia Philepittidae
(Elekezwa kutoka Philepitta)
Asiti | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Asiti mweusi
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 2, spishi 4:
|
Asiti (kutoka Kimalagasi: asity) ni ndege wadogo wa familia Philepittidae. Wanatokea misitu ya Madagaska. Manyoya ya madume ni meusi na/au buluu na spishi mbili zina tumbo njano. Wana ngozi tupu kuzunguka macho yenye rangi ya buluu au majani. Majike wana rangi ya kahawa au majivu. Spishi za Neodrepanis zina domo lililopindika kama lile la chozi. Asiti wana mkia mfupi na ulimi uliogawanyika sehemu mbili. Hula matunda hasa lakini mbochi pia na pengine wadudu. Tago lao limefumika kwa manyasi, vitawi na nyuzinyuzi na lina umbo wa parachichi. Jike huyataga mayai 2-3.
Spishi
hariri- Neodrepanis coruscans, Asiti-chozi (Common Sunbird-asity)
- Neodrepanis hypoxantha, Asiti-chozi Tumbo-njano (Yellow-bellied Sunbird-asity)
- Philepitta castanea, Asiti Mweusi (Velvet Asity)
- Philepitta schlegeli, Asiti Tumbo-njano (Schlegel's Asity)
Picha
hariri-
Asiti-chozi
-
Asiti-chozi tumbo-njano
-
Asiti tumbo-njano