Prudensi wa Troyes

Prudensi wa Troyes (kwa Kilatini: Prudentius; kwa Kifaransa: Proliant, Pruiant, Prudence; Aragon, leo nchini Hispania - Troyes, leo nchini Ufaransa, 6 Aprili 861) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 843, baada ya kuishi miaka mingi katika ikulu kama mwandishi.

Mt. Prudensi alivyochorwa.

Kama askofu alitunga muhtasari wa sala za Zaburi kwa wasafiri, alikusanya maagizo ya Biblia kwa wanaojiandaa kuwa mapadri na alirekebisha umonaki[1].

Maandishi yake mengi yanapatikana katika Patrologia Latina CXV, 971–1458, ila tenzi zake zimo katika Monumenta Germaniae Historica Poetæ Lat., II, 679 sq.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Aprili[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Girgensohn, Prudentius und die Bertinianischen Annalene (Riga, 1875)
  • Freystedt, Ueber den Prädestinationsstreit in Zeitschrift für wissenschaftl. Theologie (1893), 315 sq., 447 sq.
  • Breyer, Les vies de St. Prudence Evéque de Troyes, et de St. Maura, vierge (Troyes, 1725)
  • Meddeldorff, De Prudentio et theologia Prudentiana commentatio in Zeitschrift für histor. Theol., II (1832), 127-190

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.