Nge-bila-mkia

(Elekezwa kutoka Pseudoscorpiones)
Nge-bila-mkia
Aina ya nge-vitabu (Chelifer cancroides) akionyesha magando yake
Aina ya nge-vitabu (Chelifer cancroides) akionyesha magando yake
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Nusungeli: Dromopoda
Oda: Pseudoscorpiones
Ngazi za chini

Familia 6 za juu:

Nge-bila-mkia ni arithropodi wa oda Pseudoscorpiones katika ngeli Arachnida. Kinyume na nge wa kawaida wadudu hawa hawana mkia, kwa hivyo jina lao. Ukubwa wao ni mdogo sana: mm 2-8; spishi kubwa kabisa (Garypus titanius) ina mm 12 tu. Wanatokea mahali popote ambapo wanaweza kukamata wadudu wadogo: chini ya gamba la miti, katika takataka za majani, katika ardhi, chini ya mawe, katika nyufa za miamba, katika mapango na katika pwaji ya ufuko. Kama arakinida wote wana miguu minane. Pedipalpi zao zinafanana na zile za nge zenye magando ambayo yana kidole kinachoweza kusogea. Kidole hiki kina tezi ya sumu inayoingizwa katika mawindo. Maji ya umeng'enyaji yakamuliwa kwa windo na baada ya kumeng'enya chakula myeyuko ufyondwa. Nge-bila-mkia wanaweza kusokota hariri kama buibui lakini matezi hayapo katika mwisho wa fumbatio lakini katika kelisera (chelicerae). Kwa hariri hii hutengeneza kifukofuko kwa umbo wa sahani kinachotumika kwa kupandana, kuambua au kungoja mwisho wa hali ya hewa baridi.

  Makala hiyo kuhusu "Nge-bila-mkia" inatumia jina ambalo halijakuwepo kwa lugha ya Kiswahili. Jina hili linapendekezwa kwa jina la mnyama huyu au wanyama hawa amba(ye)(o) ha(wa)na jina kwa sasa.

Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili hazina jina kwa mnyama huyu au wanyama hawa.