Puju
Puju madoadoa (Naso brevirostris)
Puju madoadoa (Naso brevirostris)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Perciformes (Samaki kama ngege)
Familia: Acanthuridae (Samaki walio na nasaba na kangaja)
Bonaparte, 1832
Jenasi: Naso
Lacépède, 1801
Spishi: Spishi 20:

Puju au puju pembe ni samaki wa baharini wa jenasi Naso katika familia Acanthuridae wa oda Perciformes. Kama ndugu wao kangaja wana jozi za miiba kwa umbo la vijembe kwenye kila upande wa msingi wa mkia. Lakini rangi zao si kali kama zile za kangaja. Spishi fulani huitwa karanzaga au sange pia.

Maelezo

hariri

Spishi kadhaa za puju zina kivimbe kirefu kwenye paji. Kwa wengine hufanana na kangaja lakini huwa ni wakubwa zaidi. Puju mkia-ncha-nyeupe anaweza kufika urefu wa m moja. Wana jozi moja, mbili au tatu za vijembe. Hula miani kwenye miamba ya matumbawe.

Puju hupendwa na wavuvi kwa mkuki na kwa kawaida hubanikwa wazima.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Puju kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.